Mwalimu Nyerere: Matatizo makubwa ya Tanganyika katika miaka ya baadaye itakuwa Zanzibar

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
481638_02_203_julius_nyerere.jpg

"Kama ningeweza kukivuta kisiwa hicho katikati ya Bahari ya Hindi, ningefanya hivyo."

Alisema kwamba anafikiri mojawapo ya matatizo makubwa ya Tanganyika katika miaka ya baadaye itakuwa Zanzibar. Hapana, sifanyi mzaha," alisema

Aliyasema hayo katika tafrija ya chakula cha jioni jijini Dar es Salaam mwaka mmoja au miwili kabla ya uhuru wa Tanganyika.
Screenshot_20240329_162954_Facebook.jpg

Julius Nyerere akiwa na Haile Selassie I
 
Mwalimu alifanya makosa makubwa sana kutuunganisha na Wazanzibari, ambao kimsingi ni watu wasio na faida yoyote ile kwa Tanganyika mpaka sasa.
Unajua at the time mambo ya Vita Baridi na Mabeberu wa Kweli (sio wa sasa wa kufikirika) security-wise Zanzibar kwa Bara ilikuwa Threat kiasi gani ?

Mbili kwa mtu / watu waliokuwa na Ndoto ya kuunganisha Afrika nzima let alone East-Africa unadhani jirani yako wa karibu ni nani ?
 
Wewe kubali tu Mwalimu alikurupuka. Hiyo vita baridi ilikuwa inapiganwa kati ya Eastern Bloc chini ya USSR dhidi ya Western Bloc iliyokuwa chini ya Marekani na nchi za Ulaya Magharibi!

Sasa nikuulize Tanganyika ilikuwa upande gani kipindi hicho mpaka aiogope vita baridi, na hivyo kuiingiza Tanganyika kwenye huu Muungano wa kipuuzi wa changu changu, chako changu?
 
Zanzibar ni kama jikoni kwako wewe upo Chumbani..., Zanzibar walikuwa wametoka Masultan na wanaona hapo ni kwao Kumbuka hata Dar es Salaam (Bandari ya Salama ni Jina kutoka kwa Masultan)....

Tukija unaongelea vita baridi iligombaniwa huko Eastern Bloc !???? Uliza kina Kwame Nkurumah, Sankara au Patrice Lumumba..., Yes CIA was involved in most of those.... CIA was known kusaidia Coups na kuweka vibaraka wake the world over... In short those were hard times kwa Kiongozi yoyote mwenye msimamamo tofauti (Hususan ukiwa against The Colonials Companies)
 
Sasa mtu kama Nyerere alikuwa na msimamo gani! Maana wakati wa uongozi wake alikuwa akijifanya kuwaponda mabepari na mfumo wa ubepari! Na hapo hapo akawakumbatia wakomunisti na mfumo wake wa nadharia wa ujamaa!

Lakini mara kibao tu alionekana kwenye hizo nchi za kibepari mfano Marekani, nk. kwenda kuomba msada. Tena ndiyo Nyerere huyu huyu aliyesifiwa kuwa na urafiki wa karibu na Rais wa Marekani John F. Kennedy miaka ya 1960's.
 
Twende polepole aliwakumbatia wakomisti like how..., au kuwapiga na kuwakatilia makampuni ya Kigeni kuwapa vitu kwenye silver platter ndio kuwaponda mabepari..., kuhimiza self reliance ndio kuwaponda mabepari... Kupinga NBC isipewe kwa watu kama pipi ndio kuwaponda mabepari ? Kuikatalia IMF mikopo yao yenye masharti ya ajabu (kukamua ng'ombe bila kumpa chakula ndio kuuponda Ubepari) ?

View: https://youtu.be/wYP_nfGVxwo?si=WcFiOE5RSeX01_kG

By the way Ubepari na Ujamaa 100% ni nadhari za kwenye vitabu hakuna nchi 100 percent ya Kibepari au Kijamaa zote ni mixed economies na naweza kusema nchi kama UK at the moment au USA ni wajamaa kuliko hata sisi...
Lakini mara kibao tu alionekana kwenye hizo nchi za kibepari mfano Marekani, nk. kwenda kuomba msada. Tena ndiyo Nyerere huyu huyu aliyesifiwa kuwa na urafiki wa karibu na Rais wa Marekani John F. Kennedy miaka ya 1960's.
Nyerere alikwenda Marekani kuomba misaada ? Misaada ya kitu gani unaweza kuweka agenda zilizokuwepo ? Nyerere mara nyingi alikuwa anakwenda huku na huko kipindi kile sio kwa ajili ya Tanzania pekee bali Ukombozi wa Africa nzima.... waomba misaada ni hawa wa sasa ndugu yangu... Jina la Masikini Jeuri kwa Nyerere halikuja kwa bahati mbaya....
 
Mwalimu alifanya makosa makubwa sana kutuunganisha na Wazanzibari, ambao kimsingi ni watu wasio na faida yoyote ile kwa Tanganyika mpaka sasa.
Mkuu, wewe umri si umeenda kidogo? Hujui kwanini Nyerere na mwenzake waliafiki muungano? Nia ilikuwa ni nini na kwanini dhambi kubwa ndani ya ccm ni kujaribu kuuvunja muungano?
 
Vita baridi haipo tena, vipi zanzibar waoneshwe mlango wa kutokea wakajisimamie wenyewe na mambo yao kwa amani tu watoke. Ishu ni zile ole zilizotolewa na mwalimu kwamba sisi watanganyika, wale ni wazanzibar, na wazanzibar nao watagawanyika na kuwa waunguja na wapemba, hiyo dhambi inatisha sana kwa kizazi hiki kuanzia cha mwalimu hadi hichi cha sasa. Labda kije kizazi kisichosikia ole za mwalimu kwa atakayevunja muungano ndicho kitakachovunja muungano
 
Ndio tatizo la utapeli ,palikuwa hakuna hja ya kuchukua kisiwa wakati wao hawataki...Nafikria kama zenji ingesimama pekee hata tamaduni zao zingeheshimika maana hapa bado unafikiria wale ni wenzenu
 
Back
Top Bottom