Wabunge 55 walioidai Tanganyika mwaka 1993 walikuwa Watanzania au walitoka sayari ya Mars?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Hakuna bin-adam yeyote awe kiongozi ana raia asiyekua na mapungufu,viongozi wote walikuwa nayo uzuri ni kwamba walifanya mengi mazuri kuliko mabaya ndio maana tunakubali kwamba walikuwa the greatest,lakini mapungufu yao yapo na yanajadilika sana na yanafahamika sana,lakini leo 2024 yatatusaidiaje kama taifa?

Tukimkumbuka Hayati Rais Mstaafu,Ali Hassan Mwinyi,katika awamu yake kuliibuka hoja ya Serikali tatu,lakini hoja hiyo haikuanzia kwake tu,ilianzia katiba ya Zanzibar 1985,G55,katiba ya Zanzibar 2010,ikaishia UKAWA 2015.

Maoni yangu ni kwamba,haya mambo ya kudai serikali tatu yataendelea kujirudia rudia nia kama namba inayojirudia, yaani hata ikiganyika vipi itaibuliwa upya tu.Reference sasa zitakuwa ni nyingi yaani hati za Muungano,katiba ya Zanzibar 1985,G55, Katiba ya Zanzibar 2010,UKAWA,kwani kwa bahati mbaya historia ni vigumu kufutika,hivyo hata kama italazimika kuendelea kwa serikali mbili kwa wakati huu kwa mfano,lakini suala hili litajirudia tu! Kwa faida ya nyakati,niseme tu Mwalimu Julius Nyerere alikuwa sahihi,wakati ule,hoja ilipoibuliwa isingewezekana kupitishwa kwa kutumia Bunge kuleta Serikali tatu,

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alishauri CCM na Serikali yake kufuata procedures tu,hakugoma kuwa na Serikali tatu ingawa alipendelea mbili,utaratibu ulifuatwa mwaka 2014 kwa kuanzisha rasimu ya katiba,Watanzania waliulizwa,wakatoa msimamo,wengi walitaka serikali tatu,hivyo ndivyo Mwalimu alitaka utaratibu ufuatwe,hicho ndicho kilichokuwa tofauti ya mwalimu na mengi yanayozungumzwa,lakini inaweza kuwa hoja moja sawa sawa kama inavyoombwa na Chadema.lakini utofauti wa Mwalimu Julius Nyerere na mwanzilishi wa hoja ya Serikali tatu Mh Njelu Kasaka,wao walitaka serikali tatu kupitia bunge bila kupata maoni ya wanaCCM na Watanzania kwa jumla.

-Mwalimu Julius Nyerere,aliizima ndoto ya kundi la G55 lililotaka Serikali tatu.

Baada ya kung'atuka Uraisi mwaka 1985 na Uenyekiti wa CCM mwaka 1990, Mwalimu bado aliwezaje ku'influence' maamuzi matatu mazito na ya kihistoria lakini kama Kiongozi mstaafu.

Kwanza, aliwezaje kuwakemea viongozi wa chama na serikali walioonekana kujitatiti kuzuia upepo wa mageuzi na kuwaonya wasithubutu kwani hawangefanikiwa na wao wakamsikiliza (kumtii ?)

Pili, peke yake aliwezaje kuizima hoja wa wabunge (G55) ya kuidai serikali ya Tanganyika na kuikemea serikali ya Ali Hasan Mwinyi iliyoonekana imeelemewa na hivyo kusalimu amri kwa G55.lakini kwa mtazamo mwingine tujiulize,kama ni hivyo Je Mwalimu alishindwaje kuzima Azimio la Zanzibar linalosemekana ndilo lililioizika Azimio la Arusha ? Rafiki yangu William kule jamii forum uwa anasema Mwalimu aliweza kuizima ile hoja kwa sababu yeye ndiye aliyekua masterminder wa ile hoja,uwa anasema mkipata nafasi muulizeni Kasaka Njelu kwa nini alikuwa hakamatwi wakati anadai hoja ambayo kisheria ya Jamhuri yetu ilikuwa ni uhaini? Badala ya kukamatwa uwa anaishia kupewa Uwaziri Mdogo wa kilimo na kuishi Kilimanjaro Hotel!

Mwaka 2014,Nilimsikia Mh Njelu Kasaka,kinara wa G55 akisema,"Nilipeleka hoja bungeni, ikaungwa mkono na Matheo Qares, Arcado Ntagazwa, Mussa Nkhangaa, William Mpiluka (marehemu), Sebastian Kinyondo (marehemu) na Jenerali Ulimwengu. Kwa ujumla niliungwa mkono na wabunge 55, ingawa baadaye wabunge karibu wote walituunga mkono tukaambiwa halimo katika sera za CCM," alisema.

Kwa mujibu wa mwanasiasa huyo, serikali tatu au mabadiliko ya muundo wa Muungano kutoka wakati huo hadi sasa hayaepukiki.Kwamba, mtazamo wa Wazanzibari wanasema wapo tayari kutofautiana katika mambo yote kisiasa au kiitikadi lakini hoja ya Uzanzibari (identity ya nchi) haifi hadi utakapomwondoa Mzanzibari wa mwisho.

-Orodha ya G55,wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,walioidai Serikali ya Tanganyika.

1) Njelu Kasaka
mbunge wa Lupa mkoani Mbeya.
2) Lumuli Alipili Kasyupa
mbunge wa Kyela.

3) William Mpiluka
Wa Mufindi.

4) Mateo Tluway Qares
mbunge wa Babati

5) Jared Gachocha
mbunge wa Ngara.

6) Dr Mganga Titus ole Kipuyo
mbunge wa Arumeru Magharibi.

7) Phillip Sanka Marmo
Alikuwa mbunge wa Mbulu mkoani Arusha.

8) Arcado Ntagazwa

9) Patrick Silvanus Qorro (marehemu)
mbunge wa Karatu.

10) Japhet Sichona
Mbozi.

11) Jenerali Twaha Khalfan Ulimwengu
mbunge wa Taifa.

12) Abel K. Mwanga .
mbunge wa Musoma mjini.

13) Prof Aaron Eben Japhet Massawe
mbunge wa jimbo la Hai.

14) Shashu Lugeye
mbunge wa Solwa.

15) Sebastian Rweikiza
mbunge wa Bukoba vijijini.

16) Phares Kashemeza Kabuye
mbunge wa Biharamulo

17) Mbwete Polile Hombee
mbunge wa Rungwe.

18) Kisyeri Werema Chambiri
mbunge wa Tarime.

19) John Byeitima
mbunge wa Karagwe.

20) Abdallah Saidi Nakuwa
wa Lindi.

21) Dr Ndembwela Ngunangwa
mbunge wa Njombe Kusini.

22) Mathias Michael Kihaule
mbunge wa Ludewa na Naibu Spika wa Bunge.

23) Alhaji Mussa Nkhangaa
mbunge wa Iramba.

24) Edward Oyombe Ayila
Alikuwa mbunge wa Rorya.

25) Adam Karumbeta
Wa Mbeya huyu.

26) Halimeshi Mayonga
mbunge wa Kigoma vijijini.

27) Dr John Katunzi
Wa Geita.

28) Ismail Ivwata
Mbunge wa Manyoni Singida.

29) Tobi Tajiri Mweri
mbunge wa Pangani.

30) Aidan Livigha
mbunge wa Ruangwa .

31) Tabitha Ijumba Siwale (mama)
mbunge wa taifa.

32) Obel Mwamfupe
Mbeya.

33) Othman Ahmed Mpakani
Iringa magharibi.

34) Evarist Mwanansao
Nkasi.

35) Paschal Degera
Kondoa kaskazini.

36) Erasto Losioki
Wa Simanjiro.

37) Nassoro Malocho
mbunge wa Mtwara.

38) Charles Kagonji
mbunge wa Mlalo Lushoto.

39) Venance Francis Ngula
mbunge wa Taifa.

40) Benedict Kiroya Losurutia
mbunge wa Kiteto.

41) Dr Deogratias Mwita
Wa Serengeti.Yuko.

42) Phineas Nnko
Wa Arumeru Mashariki.

43) John Peter Mwanga
mbunge wa Moshi mjini na alikuwa miongoni mwa wabunge vijana
alishinda ubunge akiwa anasubiria graduation yake pale Mzumbe. Ushindi wa 1990 dhidi ya Brigedia Muhiddin Kimario ( alikuwa waziri wa mambo ya ndani)

44) Chediel Yohana Mgonja
mbunge wa Same .

45) Guntram Amani Itatiro
mbunge wa jimbo la Ifakara.

46) Captain Paschal Kulwa Mabiti
mbunge wa jimbo la Mwanza.

47) Edith Mallya Munuo (mama)
mbunge wa Taifa akiwakilisha umoja wa Wanawake.

48) Raphael Shempemba
Wa Lushoto.

49) Lt Col John Mhina
Wa Lushoto.

50) Balozi George Maige Nhigula
Mbunge wa Kwimba,

51) Captain Theodos James Kasapira
mbunge wa Ulanga magharibi,

52) Charles Kinuno
Alikuwa mbunge wa Nyanghwale.

53) Christian Fundisha

54) Samuel Ruangisa
Alikuwa mbunge wa Bukoba Mjini.

55) Dr Maria Josephine Kamm (mama)
Huyu alikuwa mbunge wa taifa.

Heshima kwenu mashujaa,ninyi mlikua Wanaume na Wanawake washoka kwelikweli,wazo la saa ya ukombozi wa Tanganyika walilitekeleza kwa vitendo....nafikiria je wangefanikiwa ingekuwaje? Nani angekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya watu wa Tanganyika? Je ni Njelu Kasaka kutoka Mbeya,Je ni Gachocha mbunge wa Ngara,Je ni Phares Kashemeza Kabuye wa Biharamulo,Je ni Sebastian Rukiza Kinyondo kutoka Bukoba vijijini,Je ni John Elikana Byeitima kutoka Karagwe! au ni Samwel Ntambala Luangisa kutoka Bukoba mjini au ni Jenerali Ulimwengu aliyeingia bungeni kama mbunge wa Taifa!

Mwalimu alitoa maoni yake toka kijijini kwake Butiama,mkoani Mara akisema wanaotaka serikali 3 wafuate utaratibu maana siyo sera ya CCM na anayepingana na hilo ajitoe CCM.

..wale G-55 hawakuwa tayari kutoka CCM na kuipigania Tanganyika.

..utekelezaji wa azimio la bunge ulisitishwa, na hoja ya Tanganyika ikarudishwa kwa wanachama wa CCM kupigiwa kura ya maoni.

..kilichoendelea ndani ya CCM hakijulikani mpaka leo, kitu ambacho nadhani at best ni ubabashaji.

..nadhani kilichofanyika ni kuahirisha tatizo tu, lakini tunaelekea kulekule kwenye serikali ya Tanganyika, this time kwa shinikizo la wa-Zanzibari.

Ni jukumu la wote waliochaguliwa kufuatilia katiba Mpya kutanguliza maslahi ya taifa ili historia iwakumbuke kama hawa G55 watakumbukwa kama watapitisha rasmu yenye maoni ya wananchi na siyo vyama vyao!

Historia inawakumbuka na kuwaenzi G55,pamoja na wengine wote waliopigania kwa vitendo kurudi kwa serikali ya Tangayika including Wajumbe wa tume ya Judge Francis Nyalali,wajumbe wa Tume ya Judge Robert Kisanga,bila kumsahau Mch. Christopher Shukrani kwa namna ya pekee ziende kwa Hayati Ali Hassan Mwinyi kwa hekima na busara alizotumia kuweza kuliruhusu jambo hilo la kudai Serikali tatu kufika bungeni na hatimae kuamriwa lirudi kupata baraka za Chama Cha Mapinduzi, naamini ndoto ya Serikali mbili kuelekea moja ilikuwa nzuri lakini ndoto ya Serikali tatu kuelekea moja ni nzuri zaidi.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Hongera saba kwa kuwa na kumbukumbu iliyo sahihi,ni mhimu sana kuweka mambo sawa,kwa sababu kila jambo linapaswa kusemwa kama lilivyo.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa, "kama ingekuwa inawezekana kuwa na Serikali moja, hilo ningeliunga mkono, lakini Wazanzibari hawatakubali".

Mwalimu Nyerere aliona wazi hoja ya kuwa na Serikali 3 au 1, na alijua wazi kuwa Serikali mbili ni nadharia danganyifu, lakini alikuwa na hofu katika machaguo mawili yaliyokuwa halisia:

Serikali 3, Mwalimu alisema ni hofu yake kuwa Muungano unaweza kuvunjika, na yeye hakuwa tayari hilo litokee. Akasema kuwa unapokuwa na Serikali 2, moja ya nchi kubwa kama Tanganyika, na nyingine ya nchi ndogo, pungufu ya wilaya ya Sengerema, ni vigumu muungano wa namna hiyo kuendelea.

Kwenye serikali moja, ambayo ingeifanya Zanzibar, hata kwa upendeleo, kuwa na mikoa labda 2 au 3, Wazanzibari wasingekubali, na huenda wangeona afadhali kujitoa kwenye muungano, na Mwalimu hakutaka kabisa muungano ufe, hata kama wananchi wote wasingeutaka.

Kwa sasa Mwalimu hayupo, mazingira yamebadilika. Tungeweza kuamua kuwa na serikali 1, wazanzibari wasipokubali, tukazanie kuwa na Federation ya East Africa, na Zanzibar iingie humo kama nchi.
 
Tanganyika kamwe haiwezi kufa hata kama kutakuwa na kitu kisichokuwepo kinachoitwa uhuru wa Tanzania Bara bado Tanganyika lilikuwa koloni la mjerumani na chini ya uangalizi wa Umoja wa mataifa kupitia Malikia.
 
Hakuna bin-adam yeyote awe kiongozi ana raia asiyekua na mapungufu,viongozi wote walikuwa nayo uzuri ni kwamba walifanya mengi mazuri kuliko mabaya ndio maana tunakubali kwamba walikuwa the greatest,lakini mapungufu yao yapo na yanajadilika sana na yanafahamika sana,lakini leo 2024 yatatusaidiaje kama taifa?

Tukimkumbuka Hayati Rais Mstaafu,Ali Hassan Mwinyi,katika awamu yake kuliibuka hoja ya Serikali tatu,lakini hoja hiyo haikuanzia kwake tu,ilianzia katiba ya Zanzibar 1985,G55,katiba ya Zanzibar 2010,ikaishia UKAWA 2015.

Maoni yangu ni kwamba,haya mambo ya kudai serikali tatu yataendelea kujirudia rudia nia kama namba inayojirudia, yaani hata ikiganyika vipi itaibuliwa upya tu.Reference sasa zitakuwa ni nyingi yaani hati za Muungano,katiba ya Zanzibar 1985,G55, Katiba ya Zanzibar 2010,UKAWA,kwani kwa bahati mbaya historia ni vigumu kufutika,hivyo hata kama italazimika kuendelea kwa serikali mbili kwa wakati huu kwa mfano,lakini suala hili litajirudia tu! Kwa faida ya nyakati,niseme tu Mwalimu Julius Nyerere alikuwa sahihi,wakati ule,hoja ilipoibuliwa isingewezekana kupitishwa kwa kutumia Bunge kuleta Serikali tatu,

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alishauri CCM na Serikali yake kufuata procedures tu,hakugoma kuwa na Serikali tatu ingawa alipendelea mbili,utaratibu ulifuatwa mwaka 2014 kwa kuanzisha rasimu ya katiba,Watanzania waliulizwa,wakatoa msimamo,wengi walitaka serikali tatu,hivyo ndivyo Mwalimu alitaka utaratibu ufuatwe,hicho ndicho kilichokuwa tofauti ya mwalimu na mengi yanayozungumzwa,lakini inaweza kuwa hoja moja sawa sawa kama inavyoombwa na Chadema.lakini utofauti wa Mwalimu Julius Nyerere na mwanzilishi wa hoja ya Serikali tatu Mh Njelu Kasaka,wao walitaka serikali tatu kupitia bunge bila kupata maoni ya wanaCCM na Watanzania kwa jumla.

-Mwalimu Julius Nyerere,aliizima ndoto ya kundi la G55 lililotaka Serikali tatu.

Baada ya kung'atuka Uraisi mwaka 1985 na Uenyekiti wa CCM mwaka 1990, Mwalimu bado aliwezaje ku'influence' maamuzi matatu mazito na ya kihistoria lakini kama Kiongozi mstaafu.

Kwanza, aliwezaje kuwakemea viongozi wa chama na serikali walioonekana kujitatiti kuzuia upepo wa mageuzi na kuwaonya wasithubutu kwani hawangefanikiwa na wao wakamsikiliza (kumtii ?)

Pili, peke yake aliwezaje kuizima hoja wa wabunge (G55) ya kuidai serikali ya Tanganyika na kuikemea serikali ya Ali Hasan Mwinyi iliyoonekana imeelemewa na hivyo kusalimu amri kwa G55.lakini kwa mtazamo mwingine tujiulize,kama ni hivyo Je Mwalimu alishindwaje kuzima Azimio la Zanzibar linalosemekana ndilo lililioizika Azimio la Arusha ? Rafiki yangu William kule jamii forum uwa anasema Mwalimu aliweza kuizima ile hoja kwa sababu yeye ndiye aliyekua masterminder wa ile hoja,uwa anasema mkipata nafasi muulizeni Kasaka Njelu kwa nini alikuwa hakamatwi wakati anadai hoja ambayo kisheria ya Jamhuri yetu ilikuwa ni uhaini? Badala ya kukamatwa uwa anaishia kupewa Uwaziri Mdogo wa kilimo na kuishi Kilimanjaro Hotel!

Mwaka 2014,Nilimsikia Mh Njelu Kasaka,kinara wa G55 akisema,"Nilipeleka hoja bungeni, ikaungwa mkono na Matheo Qares, Arcado Ntagazwa, Mussa Nkhangaa, William Mpiluka (marehemu), Sebastian Kinyondo (marehemu) na Jenerali Ulimwengu. Kwa ujumla niliungwa mkono na wabunge 55, ingawa baadaye wabunge karibu wote walituunga mkono tukaambiwa halimo katika sera za CCM," alisema.

Kwa mujibu wa mwanasiasa huyo, serikali tatu au mabadiliko ya muundo wa Muungano kutoka wakati huo hadi sasa hayaepukiki.Kwamba, mtazamo wa Wazanzibari wanasema wapo tayari kutofautiana katika mambo yote kisiasa au kiitikadi lakini hoja ya Uzanzibari (identity ya nchi) haifi hadi utakapomwondoa Mzanzibari wa mwisho.

-Orodha ya G55,wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,walioidai Serikali ya Tanganyika.

1) Njelu Kasaka
mbunge wa Lupa mkoani Mbeya.
2) Lumuli Alipili Kasyupa
mbunge wa Kyela.

3) William Mpiluka
Wa Mufindi.

4) Mateo Tluway Qares
mbunge wa Babati

5) Jared Gachocha
mbunge wa Ngara.

6) Dr Mganga Titus ole Kipuyo
mbunge wa Arumeru Magharibi.

7) Phillip Sanka Marmo
Alikuwa mbunge wa Mbulu mkoani Arusha.

8) Arcado Ntagazwa

9) Patrick Silvanus Qorro (marehemu)
mbunge wa Karatu.

10) Japhet Sichona
Mbozi.

11) Jenerali Twaha Khalfan Ulimwengu
mbunge wa Taifa.

12) Abel K. Mwanga .
mbunge wa Musoma mjini.

13) Prof Aaron Eben Japhet Massawe
mbunge wa jimbo la Hai.

14) Shashu Lugeye
mbunge wa Solwa.

15) Sebastian Rweikiza
mbunge wa Bukoba vijijini.

16) Phares Kashemeza Kabuye
mbunge wa Biharamulo

17) Mbwete Polile Hombee
mbunge wa Rungwe.

18) Kisyeri Werema Chambiri
mbunge wa Tarime.

19) John Byeitima
mbunge wa Karagwe.

20) Abdallah Saidi Nakuwa
wa Lindi.

21) Dr Ndembwela Ngunangwa
mbunge wa Njombe Kusini.

22) Mathias Michael Kihaule
mbunge wa Ludewa na Naibu Spika wa Bunge.

23) Alhaji Mussa Nkhangaa
mbunge wa Iramba.

24) Edward Oyombe Ayila
Alikuwa mbunge wa Rorya.

25) Adam Karumbeta
Wa Mbeya huyu.

26) Halimeshi Mayonga
mbunge wa Kigoma vijijini.

27) Dr John Katunzi
Wa Geita.

28) Ismail Ivwata
Mbunge wa Manyoni Singida.

29) Tobi Tajiri Mweri
mbunge wa Pangani.

30) Aidan Livigha
mbunge wa Ruangwa .

31) Tabitha Ijumba Siwale (mama)
mbunge wa taifa.

32) Obel Mwamfupe
Mbeya.

33) Othman Ahmed Mpakani
Iringa magharibi.

34) Evarist Mwanansao
Nkasi.

35) Paschal Degera
Kondoa kaskazini.

36) Erasto Losioki
Wa Simanjiro.

37) Nassoro Malocho
mbunge wa Mtwara.

38) Charles Kagonji
mbunge wa Mlalo Lushoto.

39) Venance Francis Ngula
mbunge wa Taifa.

40) Benedict Kiroya Losurutia
mbunge wa Kiteto.

41) Dr Deogratias Mwita
Wa Serengeti.Yuko.

42) Phineas Nnko
Wa Arumeru Mashariki.

43) John Peter Mwanga
mbunge wa Moshi mjini na alikuwa miongoni mwa wabunge vijana
alishinda ubunge akiwa anasubiria graduation yake pale Mzumbe. Ushindi wa 1990 dhidi ya Brigedia Muhiddin Kimario ( alikuwa waziri wa mambo ya ndani)

44) Chediel Yohana Mgonja
mbunge wa Same .

45) Guntram Amani Itatiro
mbunge wa jimbo la Ifakara.

46) Captain Paschal Kulwa Mabiti
mbunge wa jimbo la Mwanza.

47) Edith Mallya Munuo (mama)
mbunge wa Taifa akiwakilisha umoja wa Wanawake.

48) Raphael Shempemba
Wa Lushoto.

49) Lt Col John Mhina
Wa Lushoto.

50) Balozi George Maige Nhigula
Mbunge wa Kwimba,

51) Captain Theodos James Kasapira
mbunge wa Ulanga magharibi,

52) Charles Kinuno
Alikuwa mbunge wa Nyanghwale.

53) Christian Fundisha

54) Samuel Ruangisa
Alikuwa mbunge wa Bukoba Mjini.

55) Dr Maria Josephine Kamm (mama)
Huyu alikuwa mbunge wa taifa.

Heshima kwenu mashujaa,ninyi mlikua Wanaume na Wanawake washoka kwelikweli,wazo la saa ya ukombozi wa Tanganyika walilitekeleza kwa vitendo....nafikiria je wangefanikiwa ingekuwaje? Nani angekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya watu wa Tanganyika? Je ni Njelu Kasaka kutoka Mbeya,Je ni Gachocha mbunge wa Ngara,Je ni Phares Kashemeza Kabuye wa Biharamulo,Je ni Sebastian Rukiza Kinyondo kutoka Bukoba vijijini,Je ni John Elikana Byeitima kutoka Karagwe! au ni Samwel Ntambala Luangisa kutoka Bukoba mjini au ni Jenerali Ulimwengu aliyeingia bungeni kama mbunge wa Taifa!

Mwalimu alitoa maoni yake toka kijijini kwake Butiama,mkoani Mara akisema wanaotaka serikali 3 wafuate utaratibu maana siyo sera ya CCM na anayepingana na hilo ajitoe CCM.

..wale G-55 hawakuwa tayari kutoka CCM na kuipigania Tanganyika.

..utekelezaji wa azimio la bunge ulisitishwa, na hoja ya Tanganyika ikarudishwa kwa wanachama wa CCM kupigiwa kura ya maoni.

..kilichoendelea ndani ya CCM hakijulikani mpaka leo, kitu ambacho nadhani at best ni ubabashaji.

..nadhani kilichofanyika ni kuahirisha tatizo tu, lakini tunaelekea kulekule kwenye serikali ya Tanganyika, this time kwa shinikizo la wa-Zanzibari.

Ni jukumu la wote waliochaguliwa kufuatilia katiba Mpya kutanguliza maslahi ya taifa ili historia iwakumbuke kama hawa G55 watakumbukwa kama watapitisha rasmu yenye maoni ya wananchi na siyo vyama vyao!

Historia inawakumbuka na kuwaenzi G55,pamoja na wengine wote waliopigania kwa vitendo kurudi kwa serikali ya Tangayika including Wajumbe wa tume ya Judge Francis Nyalali,wajumbe wa Tume ya Judge Robert Kisanga,bila kumsahau Mch. Christopher Shukrani kwa namna ya pekee ziende kwa Hayati Ali Hassan Mwinyi kwa hekima na busara alizotumia kuweza kuliruhusu jambo hilo la kudai Serikali tatu kufika bungeni na hatimae kuamriwa lirudi kupata baraka za Chama Cha Mapinduzi, naamini ndoto ya Serikali mbili kuelekea moja ilikuwa nzuri lakini ndoto ya Serikali tatu kuelekea moja ni nzuri zaidi.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
Maelezo mazuri ya historia na umenikumbusha watu ambao nilikwisha anza kuwasahau! Nakushukuru sana. Ila katika orodha hiyo wengi wamesha kwenda mbele ya haki na siyo wale uliowataja peke yao. Pili, hoja ya G 55 ilianza baada ya jaribio la Zanzibar kutaka kujiunga na OIC bila kuihusisha Serikali ya Muungano; hiyo hoja haikuzuka tu. Tatu ni watu wachache sana wenye uelewa wa kumsoma Nyerere. Binafsi naona kama Nyerere alitumia mwanya huo wa hoja ya G 55 kuchagiza Serikali ya Awamu ya tatu iwe na watu gani. Alipowapata alifurahi sana lakini baadaye alijuta! Ni mawazo yangu tu baada ya kusoma hoja nzuri uliloandika.
 
Back
Top Bottom