Nimejiridhisha Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anastahili kuwa Mtakatifu

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Bahati mbaya vijana wengi waliozaliwa mwaka 2000 hawakuwahi kumwona wala kumwelewa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Mimi niliyezaliwa 1980 nilibahatika kidogo nyakati hizo nikiwa shule ya Msingi bungo pale Morogoro,nilipokuwa kiongozi wa chipukizi, nilipeana naye mkono mara moja japo alikuwa amestaafu lakini ni kama vile bado alikuwa Mwenyekiti wa heshima ndani ya CCM na bado aliendelea kutoa ushauri kwa Rais na Serikali kila mara mambo yalipoenda kombo,nilipata pia kuvisoma vitabu vyake vichache,na wakati fulani kuyasikia maneno yake kwenye matukio mbalimbali rasmi ya kiserikali, Mwalimu Julius Nyerere ni alama ya baraka tele kwa taifa letu adhimu.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa na hekima, busara na mashauri ambayo kiuhalisia alipaswa kuwa nayo kila mtu ambaye anajiita Mtanzania. Mwalimu aliishi, anaishi na ataendelea kuishi,japo mwili wake upo ardhini,Viongozi wengine waliishi na kisha wakafariki mwili, roho na fikra, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,tunakukumbuka sana, kwa sababu ya uadilifu, ukweli kwa nafsi yako, upendo wako wa kweli kwa Taifa lako,kama walivyo wanadamu wote, pamoja na mengi mazuri uliyoyatenda, yawezekana kuna mahali ulipungukiwa, la wewe mwenyewe ulivyowahi kunena "Tulifanya mazuri lakini tulifajya makosa pia. Tusifanye makosa, sisi ni malaika?" Mungu wetu, uliye tajiri wa msamaha,pale mtumishi wako alipopungukiwa, umjalie msamaha kamili anapokwenda kuwa miongoni mwa watakatifu wanaoizunguka meza yako,wakikusujudia na kukusifu usiku na mchana,sala za mja wako alizowahi kusali zikawe manukato mbele yako na zikalete baraka kwa Taifa la Tanzania alilolipenda bila hila bali kwa moyo uliokamili usio na unafiki,

Ungana nasi Mwalimu Julius Nyerere tunapoomba Mungu aliepushe Taifa letu la Tanzania dhidi ya viongozi wanafiki na walaghai wanotaka waliongoze Taifa letu kwa hila,uwongo,vitisho na ulaghai,uovu wowote waufanyao,ukawe adhabu yao ya Duniani na Mbinguni. Mwalimu alikuwa maskini wa duniani,lakini angetaka angeweza kuwa tajiri kupindukia kutokana na mazingira ya wakati huo,lakini aliwatazama zaidi Watanzania kuliko kujitazama yeye na familia yake,niliwahi kushiriki chakula cha jioni pamoja na Mwalimu nyumbani kwake Butiama,akiwa amestaafu, hakika kuanzia mazingira, mpaka chakula chenyewe,killikuwa cha kawaida sana ambacho mwanakijiji wa kawaida anamudu kukipata, Mwalimu hakuwahi kujiona bora kuliko wanadamu wengine,kaunda suti zake zilikuwa zikishonwa na fundi cherahani pale Kariakoo, hakuna Rais hata mmoja,baada yake aliyeamua kuishi kama wananchi wake wanavyoishi, wote waliofuatia, kwa kiasi fulani, nafasi ya Urais ilionekana ni nafasi ya kuwaingiza familia zao, ndugu zao, marafiki na wanafiki wa kusifia,kwenye nafasi za uongozi.

Mwalimu Julius Nyerere alitumia fedha za nchi (taifa) kusaidia nchi za kusini kupambana na ukoloni (Wazungu) huu ni upendo wa dhati,alijaliwa uweza wa kuwajali wengine kuliko yeye na Taifa lake,alipenda Tanzania ikiwa na amani basi Afrika nzima iwe na amani, Tanzania ikiwa huru basi afrika nzima iwe huru.japo shukrani ya punda ni mateke leo mtanzania akienda South Afrika anatimuliwa.Taifa letu hatujalipwa hata ndururu wala kurudishiwa wema na SA,Angola,na nchi nyingine tulizozisaidia,nchi hizo zina uchumi mkubwa kuliko Tanzania kwa sasa,Wakati Mwalimu Julius Nyerere anatumia rasilimali za Tanzania kuhudumia nchi nyingine ili zipate uhuru,nchi ya Kenya ilikuwa inajenga viwanda na miundombinu,sisi kama nchi tulikuwa tuna matatizo mengi kama Elimu,Afya,Miundombinu lakini tuliona tuwasaidie kwanza wenzetu waliokuwa kwenye mapigqno makali ya mkoloni,tunaweza kusema Kiongozi wa nchi aliyependa nchi nyingine na raia wake pia,watu wengi wanasema hawaoni faida za Muungano alioanzisha Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume kati ya Tanganyika na Zanzibar,Watu wanasema rasilimali nyingi za Tanganyika zinainufaisha Zanzibar ikiwemo viongozi wa Zanzibar kuwa viongozi kwenye ardhi ya Tanganyika wakati Watanganyika hawawezi kutawala hata wilaya moja huko Zanzibar,nilitetee hili kwa mtazamo wangu hii ni kwa sababu Zanzibar ilikuwa taifa dogo kulinganisha na eneo la Tanganyika lililokuwa kubwa maradufu,

Viongozi wa kizazi hiki hatuwezi kukaribia hata robo ya personality ya Mwalimu Julius Nyerere,kama viatu vya Hayati Rais John Magufuli havitutoshi basi viatu ya Mwalimu Julius Nyerere tutafanya nyumba ya kulala kabisa,naongea kwa viongozi wote pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani nchini,nimzungumzie kidogo Hayati Rais John Pombe Magufuli,yeye nae hakuwa mtu wa kawaida,mwaka 1992 kwenye jubilee ya kanisa katoliki Mwanza,kipindi cha uongozi wa Mhashamu Baba Askofu Antony Mayalla,alikuwepo Rais Ali Hassan Mwinyi,Hayati Benjamin Mkapa,Dkt William Shija,Baba wa Taifa alipoitwa kusema neno,aliinuka na kusema neno na mwishoni aliita Ally,kuna kijana mmoja hapa anaitwa John,yupo hapa?,huyu kijana yupo nyanza,Rais Ali Hassan Mwinyi akainuka akamwita Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati huo Dkt William Shija,akauliza huyo kijana unamjua?,akasema labda John Pombe magufuli,Mwalimu Nyerere akajibu ndio,John Pombe Magufuli akainuka toka nyuma kanisani,alipofika madhabahuni Mwalimu akainua fimbo na kusema huyu ni zao la Kanisa,mseminari,kijana hongera sana kwa kujitoa mhanga na kupambana na wahujumu wa nyanza,Tanzania inahitaji wazalendo kama wewe,

Upande wa siasa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na wapigania uhuru wote kote duniani,walilenga kuwafanya mataifa yao kuwa huru,sio tu kutoka kwenye minyororo ya ukoloni,bali katika kilajambo ikiwemo la Uafrika na u Tanzania wetu ikiwemo tamaduni zetu,ni jambo la kusikitisha unaposikia baadhi ya viongozi wa juu kabisa kisiasa wakishangilia na kushabikia matamko kutoka 'Washington' ambayo kimsingi si tu yanawanyang'anya uhuru wetu kama nchi,lakini pia yanatufanya tuonekane kama tunajiuza mbele yao,nirejee nukuu hii “Decisions made in Washington are more important to us than those made here in Dar es-Salaam. So, maybe my people should be allowed to vote in American presidential elections”. Julius Nyerere

Nimalizie kwa kusema,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni Kiongozi bora kabisa kupata kutokea duniani,hakuna mfano wake hata Urusi,Cuba na China,aliwazuia Ukoo wake kutengeneza fursa za kiuchumi kupitia jina lake,ukwapuzi kupitia jina lake,vyeo na teuzi kupitia jina lake,kwani kipi kilimzuia?!!!Mwalimu alijengewa nyumba na Serikali maana hela ya kujenga nyumba ya kifahari aliacha iende kwa wengine wasio na uwezo,Ukilinganisha na uongozi wa leo,basi Mwalimu Julius Nyerere kweli ni Mtakatifu.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
sawa, you might be right on your side, but you have to make a thorough research before reaching such a conclusion!

nambie umesoma vitbu gani na vingapi kuhusu Nyerere (to be specifc aliowatende maovu)
 
Bahati mbaya vijana wengi waliozaliwa mwaka 2000 hawakuwahi kumwona wala kumwelewa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Mimi niliyezaliwa 1980...
1700058507763.jpeg
 
Hakuna cha utakatifu. Huyu mshenzi ndiye aliyefanya ukoo wangu Kuwa na maisha magumu na sera zake za kipumbavu.

Mababu zangu walinyang'anywa maduka. Wakapewa kesi ya uhujumu uchumii. Hivi sera za ujamaa kutaka watu Kuwa sawa kiuchumi alizitoa wapi huyu lijinga. Huko aliko aongezee azabu ya moto
 
Hakuna cha utakatifu. Huyu mshenzi ndiye aliyefanya ukoo wangu Kuwa na maisha magumu na sera zake za kipumbavu. Mababu zangu walinyang'anywa maduka. Wakapewa kesi ya uhujumu uchumii. Hivi sera za ujamaa kutaka watu Kuwa sawa kiuchumi alizitoa wapi huyu lijinga. Huko aliko aongezee azabu ya moto
Ujamaa Ni Sera ya Mungu mwenyewe!
Bahati mbaya mwanadamu kiasili ni mbinafsi!
Wanaoweza kutekeleza Sera ya ujamaa Ni malaika na watakatifu mbinguni
 
Ujamaa Ni Sera ya Mungu mwenyewe!
Bahati mbaya mwanadamu kiasili ni mbinafsi!
Wanaoweza kutekeleza Sera ya ujamaa Ni malaika na watakatifu mbinguni
Acha kupotosha watu. Mungu hakuweka mfumo wa ujamaa. Usifananishe Maisha mwanadamu na malaika. Wanadamu tumepewa uhuru wa kufanya jambo lolote tunalotaka hatakama litamuuzi Mungu. Ila malaika wanafanya Kazi Kwa maagizo kutoka kwa Mungu na wanalimits katika majukumu yao.

Ubepali ulikuwepo toka kipindi cha mitume na manabii. Rejea Enzi za mtume Suleimani, nabii Issa bin Mariam. Utaona kulikuwa na matabaka ya KIJAMII.

Na hayo yote Mungu ndiye alikwisha Hukumu
 
Bila shaka wewe utakuwa mkatoliki
Nyerere alikuwa na mambo mengi tu mazuri na mengi tu mabaya hakuna binadamu asiye na mapungufu.
Sasa hapo mapungufu yake ndio yanamfanya akose sifa ya kuitwa mtakatifu nitoe mifano
1.alinyonga
2.alinyang'anya watu mali walizochuma kwa jasho lao kisa siasa ya ujamaa ambayo haijafanikiwa hadi leo
3.Alikuwa mbinafsi wa kifichi mfano akiona una elimu kubwa sana na tishio kwake anatafuta mbinu kwa akili kubwa kukukwamisha ila si kukumaliza
4.Aliongoza wananchi wake kuwafanya kama mazuzu mfano hakuruhusu uhuru wa vyombo vya habari ndio maana akaanzisha SHIHATA enzi zake kuwa na video ilikuwa ni uhujumu
5.alikuwa na mawazo ya kimasikini
6.Makabila yaliyoendelea alikuwa na chuki nayo lakini isiyo wazi wazi.Nitatoa mfano mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa mbele sana kielimu hivyo matokeo ya darasa la saba shule inaweza pita miaka7 haijafaulisha hata mmoja na kukaja neno kuchaguliwa sio kufaulu.Wachaga waliona hilo mapema wakajenga shule zao za private matokeo yake mikoa ile ambayo alikuwa anataka isonge mbele watoto wao wakawa wanakwenda kusoma Kilimanjaro
7. yapo mengi ni siri kubwa
8.Alikuwa hapendi upinzani

Sababu zote hizi zinamnyima sifa ya kuwa mtakatifu.Hii dhana ya kutaka kumtangaza kuwa mwenye heri ni kampeni za kanisa katoliki kutaka sifa kuwa nchi yetu imepata mtakatifu na raisi wa Uganda Museveni naye anapiga sana hili chapuo.
Sifa zote zake nzuri ulizoeleza ziko sahihi kabisa hakuna ubishi kungekuwa na mtakatifu wa siasa hiyo nafasi angestahili Mungu amuweka pema raisi wetu baba wa taifa amelifanyia taifa mambo mengi makubwa
 
Back
Top Bottom