witnessj
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 28,839
- 47,747
Ebwaaana eh...ukianza kuishi kwa kuwasikiliza binadamu wanataka nini kwako hiki ndo chanzo cha kupoteza network...Sad, alikuwa single mom....watu wakachonga sana. Huolewi coz ni Malaya, kama si Malaya mbona umezalishwa hujaolewa...na blah blah kibao.
Akaona isiwe shida kwa kuwa natongozwa ngoja niolewe na yeyote yule ...akajivutia msukuma ambaye si mtumishi bali mkulima.Kumbe msukuma nae kaenda kimalengo. Mwanamke kanunua uwanja kaanza kujenga bwana kaz yake kusimamia mama yupo job. Mara msukuma kaanza mbwembwe, hamtaki mtoto aliyemkuta, anamhasa mkewe ampeleke kwa baba ake. Mke alishatelekezwa muda huyo baba anamtoa wapi.
Mwalimu ikabidi amwambie bas tuachane, mwanaume kamwambia ukitaka tuachane bas tuuze nyumba tugawane pesa ndo tuachane. Mwanamke kasema siuzi coz ni yangu na nimejenga kwa ajili ya watoto. Ugomvi huo umesababisha mwanaume ajifanye ameaga anaondoka kumbe kaenda kunoa panga kitaa. Ndo ivo mwanamke kaoga, ainame apakae mafuta kakatwakatwa kama mnyama.
Sad,sad,sad....yaan kumbe jamaa nae kanywa sumu now tumepata taarifa nae kakata moto huko hospital. SINGLE MOMZ MSIFORCIWE....MABACHERORS MSILAZIMISHE NDOA. MARRIAGE IS NOT EVERYTHING! Inyala mbeya.
Mambo ya kufosi king daah

