Mwalimu mwenzangu kafariki kisa ndoa

Beesmom

JF-Expert Member
May 30, 2016
17,221
28,666
Sad, alikuwa single mom, watu wakachonga sana. Huolewi coz ni Malaya, kama si Malaya mbona umezalishwa hujaolewa na blah blah kibao.

Akaona isiwe shida kwa kuwa natongozwa ngoja niolewe na yeyote yule. Akajivutia msukuma ambaye si mtumishi bali mkulima. Kumbe msukuma naye kaenda kimalengo. Mwanamke kanunua uwanja kaanza kujenga, bwana kazi yake kusimamia mama yupo job. Mara msukuma kaanza mbwembwe, hamtaki mtoto aliyemkuta, anamhasa mkewe ampeleke kwa baba yake. Mke alishatelekezwa muda huyo baba anamtoa wapi.

Mwalimu ikabidi amwambie basi tuachane, mwanaume kamwambia ukitaka tuachane basi tuuze nyumba tugawane pesa ndo tuachane. Mwanamke kasema siuzi coz ni yangu na nimejenga kwa ajili ya watoto. Ugomvi huo umesababisha mwanaume ajifanye ameaga anaondoka kumbe kaenda kunoa panga kitaa. Ndiyo hivyo mwanamke kaoga, ainame apakae mafuta kakatwakatwa kama mnyama.

Sad, sad, sad! Yaani kumbe jamaa naye kanywa sumu, now tumepata taarifa naye kakata moto huko hospital. Inyala Mbeya. Single moms msilazimishwe, mabacherors msilazimishe ndoa, marriage is not everything!
 
Sad,alikuwa single mom....watu wakachonga sana.Huolewi coz ni Malaya,kama si Malaya mbona umezalishwa hujaolewa...na blah blah kibao.
Akaona isiwe shida kwa kuwa natongozwa ngoja niolewe na yeyote yule ...akajivutia msukuma ambaye si mtumishi bali mkulima.Kumbe msukuma nae kaendaMABACHERORS MSILAZIMISHE NDOA.MARRIAGE IS NOT EVERYTHING! Inyala mbeya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom