Mwali: Mmiliki wa DOWANS ni huyu!

Mwali: Mmiliki wa DOWANS ni huyu!

Status
Not open for further replies.
I admire the optimism and faith in your message but CCM have worked waTanzania out. They know what makes them tick and more importantly what it takes to win elections. Ukweli ni kwamba sisi ni Mabwege. Kampeni za 2010 zimeshaanza and I expect by June next year all will have been forgiven and forgotten. Watch this space

I refuse to be so pessimistic because I have seen some hopeful signs, I believe watz si mabwege tena na 2010 utakuwa mwaka mgumu sana for CCM. Mark my words!
 
Anajuana na Dowans, Kagoda
Serikali yamwangalia tu

Na Saed Kubenea
Mwanahalisi~Maslahi ya Taifa Mbele

MWANASIASA na mfanyabiashara Rostam Aziz ana siri kubwa kuhusu makampuni ya Dowans na Kagoda Agriculture Limited yanayotuhumiwa kwa kuhujumu uchumi.

Dowans ambao imekuwa vigumu kujua makazi ya ofisi zao na maofisa wake wanaowasiliana na serikali, imekuwa kampuni kivuli kama ilivyo Kagoda.

Lakini Rostam Aziz alinukuliwa na vyombo vya habari wiki iliyopita akikiri kuwafahamu wamiliki wa kampuni ya Dowans iliyorithi mkataba wa kufua umeme wa Richmond.

Wakati Rostam anakiri kufahamu wamiliki wa Dowans, kwa madai kwamba aliwahi kuwaomba kazi, taarifa zilizopo zinamtaja mfanyabiashara huyo kuwa na mkono katika mkakati wa kukwapua zaidi ya Sh. 40 bilioni kutoka Benki Kuu (BoT) kwa jina la Kagoda.


Kwa mujibu wa taarifa za Wakala wa Usajili wa Makapuni nchini (BRELA), wenye hisa wote wa Dowans wana anwani za nje ya nchi za Costa Rica na Singapore.

Wenye hisa katika kampuni hiyo ni Dowans Holdings SA ya Avenida de la Rosas 3J; CALLE BLANCOS, 1150 ya San Jose, Costa Rica wenye hisa 81.

Wengine ni Portek Systems wenye hisa 19 na Equipment PTE Ltd., wenye hisa 35 na ambao wanatumia anwani moja ya 20 Harbour Drive, #02 01 PSA VISTA ya Singapore.

Hata hivyo ni Dowans Holdings SA ya Costa Rica ambayo hadi sasa imefahamika kutokuwa na ofisi nchini humo; kutokuwa na gari, simu wala sanduku la barua.

Kukiri kwa Rostam kufahamu wamiliki wa Dowans kunamfanya awe mtu muhimu nchini katika kuchunguza tuhuma zinazokabili kampuni hiyo.


Aidha, mmoja wa wafanyakazi katika kampuni ya Rostam Aziz ya Caspian, anadaiwa kuwa mmoja wa watia saini kwenye hundi za malipo yaliyofanywa kwa kampuni ya Zakhem Contractors Limited ya Mbagala, Dar es Salaam iliyojenga msingi wa kuweka mashine za Richmond/Dowans.

Gazeti hili liliwahi kuchapisha kivuli cha moja ya hundi mbili zilizolipwa kwa Zakhem kupitia EuroAfrica Bank (sasa BOA Bank) ambako, hata hivyo, zilirejeshwa bila kulipwa kwa maelezo kuwa akaunti haikuwa na fedha.

Ni Rostam huyohuyo ambaye imethibitika kuwa mmoja wa wafanyakazi wake, John Kyomuhendo, alikuwa mmoja wa waanzilishi wa kampuni ya Kagoda ambayo ilichota mabilioni ya shilingi kutoka BoT.

Namba ya kiwanja na kitalu, Na 87 katika eneo la viwanda Kipawa (Industrial Area) zilizotajwa kuwa makazi ya Kagoda, hazipo kwenye ramani ya jiji.

Wiki mbili zilizopita, wakili Bhyidinka Michael Sanze alinukuliwa na gazeti hili, katika andishi maalum kwa Kamati ya Rais kuhusu wizi kwenye akaunti ya madeni ya nje (EPA), akimtaja Rostam kuwa mtu muhimu katika ukwapuaji wa mabilioni benki.

Sanze alieleza kwa maandishi kuwa aliitwa na Rostam katika ofisi yake iliyoko Mirambo 50 jijini Dar es Salaam, ambako aliambiwa na wakili wake kiongozi, Bered Malegesi kusaini mkataba wa Kagoda wa kuchota mabilioni ya shilingi kutoka BoT.

Kwa mujibu wa Sanze, katika ofisi ya Rostam alikuwemo pia Peter Noni ambaye hivi sasa ni Mkurugenzi wa Mipango Kimkakati wa BoT na shahidi wa serikali katika kesi za ufisadi.


Alisema Rostam alimweleza kuwa ni rais mstaafu Benjamin Mkapa aliyeagiza fedha hizo zichotwe na kukabidhiwa kwake (Rostam) kwa ajili ya kusaidia CCM katika uchaguzi mkuu wa 2005.

Tangu kutangazwa kwa taarifa hizo, si Rostam wala yeyote aliyetajwa katika andishi la Sanze amejitokeza kukana.


Kwa ushahidi uliopo, na kwa kuzingatia kukiri kwake, Rostam ana uhusiano wa karibu na Dowans, Richmond na Kagoda, makampuni ambayo wananchi wanalia nayo kuhusu ufukarishaji wa nchi.

Vilevile Rostam anatajwa kuwa mfuatiliaji mkuu wa malipo ya Richmond/Dowans kutoka Hazina na BoT kila alipoona malipo yanacheleweshwa.

Bali hakuna ushahidi wowote kuhusu juhudi za serikali kutumia mtu huyu, mwenye ukaribu na makampuni haya ya kifisadi, kuchunguza na hata kurejesha asilimia ndogo tu ya fedha zilizoibwa.


Kwa wiki nzima, gazeti limekuwa likimtafuta Rostam kupata kauli yake, lakini simu yake ya mkononi, Na. 0754 555555 imekuwa ikijibu kuwa hapatikani. Hata ujumbe wa maandishi uliopelekwa kwake haukujibiwa ingawa ulionyesha kuwa ulipokelewa.

"Huo ndio umaarufu wa Rostam; biashara zake zenyewe hazionekani lakini yuko kila mahali penye shina la fedha," ameeleza mmoja wa wafanyabiashara wakubwa jijini Dar es Salaam.

Kutoonekana kwa Rostam katika maandishi kuhusu umiliki wa makampuni ya Kagoda, Richmond na Dowans, kumeelezwa kuwa siyo jambo la bahati mbaya kwake.


Rostam Aziz haonekani hata katika New Habari Group iliyonunua kampuni ya Habari Corporation, wachapishaji wa magazeti ya Rai, Dimba, Mtanzania, Bingwa na The African.

Lakini ni Rostam anayetajwa na kufahamika kuwa mmiliki wa kampuni hiyo; mwenye mamlaka ya kuteua na kuajiri menejimenti; kuajiri na kulipa wafanyakazi.
 
Mimi nilisha sema haya, rostam ndio alikua ameshika pesa za uchaguzi, hata wakati mambo yamekua magumu zanzibar, pesa zilitoka nyumbani kwa rostam Dodoma na kupelekwa zenji. Chumba kizima kilikua na masanduku ya pesa. Hizi habari alitoa mbunge mwenye asili ya kiarabu ambaye alikua rafiki mkubwa wa rostam. Inajulikana wazi kabisa kua hata lowassa alichaguliwa na Rostam sio kikwete. Kwasas huyu jamaa amesha kimbiza hela zote dubai kwa mdogo wake, Fatilieni company iko Dubai inaitwa Rostamani. Mtajua ni ya nani.
 
Mimi nilisha sema haya, rostam ndio alikua ameshika pesa za uchaguzi, hata wakati mambo yamekua magumu zanzibar, pesa zilitoka nyumbani kwa rostam Dodoma na kupelekwa zenji. Chumba kizima kilikua na masanduku ya pesa. Hizi habari alitoa mbunge mwenye asili ya kiarabu ambaye alikua rafiki mkubwa wa rostam. Inajulikana wazi kabisa kua hata lowassa alichaguliwa na Rostam sio kikwete. Kwasas huyu jamaa amesha kimbiza hela zote dubai kwa mdogo wake, Fatilieni company iko Dubai inaitwa Rostamani. Mtajua ni ya nani.

omr,

Nafikiri unazungumzia AWRostamani Group of companies. AW Rostamani Building Industries

Kwa mujibu wa jinsi ninavyofanya nao biashara, hawa hawana hata chembe ya uhusiano na Fisadi-papa Rostam
 
Dowans hawana pa kwenda; wamewazuga watu lakini waliozugika wamezugika.. Watu wameacha kuiangalia Dowans.. well tutabadilisha hilo kesho!!!
 
Kwa hiyo tusahau huyu jamaa RA kuguswa maana kama pesa zingine zilitumika kumweka rais Plot no.1 Magogoni kama siku zote tunavyosema ,sasa ataguswa kwa miadi ipi .Na inawezekana hizo hela za kuuzia majenereta ni kwa ajili ya uchaguzi wa mwakani .Ila wanatakiwa wajue mambo hayako vile vile sasa ni hatari kidogo.
 
Kesho patakuwa pachungu Tanzania.. patakuwa hapanogi; yaani kama ni mwali atafunuliwa uso kesho...!! Joto limezidi kupanda..
 
Kesho patakuwa pachungu Tanzania.. patakuwa hapanogi; yaani kama ni mwali atafunuliwa uso kesho...!! Joto limezidi kupanda..

Kesho kwa saa ya wapi mkuu ili niangalie kwenye kasimu kangu wakati nabeba box. Maana sitaki hii issue inipite hata kidogo.
 
Msiwe na wasiwasi... this is bigger; na mwali hamalizwi kuchezwa kesho si unajua tena kwenye vijiji vingine sheria hadi siku saba..!
 
Atatokea hapahapa au uwanja upi? Tunataka kujiandaa mkao wa kula kabisa mkuu!
 
Nyani my friend, I think you could have definitely done a better job, but then Jk doesn't have a standard
but on a more serious note, nakereka sana ninaposikia hoja eti tumchague JK maana hamna chaguo bora zaidi... whaaaat??? Mi nasema hivi kheri hata tumchague Mrema au Mtikila kuliko kuendelea na ufisadi huu ambao unatuangamiza. Tunachekacheka hapa na kufanya kama vile we are helpless, watanzania si mabwege and we have to prove it. Election time is the only time when a citizen can punish bad leaders let's make sure we tell CCM and its terrible leadership that it should go and stand in the corner and put on a dunce hat! Tuwape nafasi wengine, maana sidhani kama kuna mtu anaweza kuchemka kiasi alichochemka JK! He is worse than any opposition leader so far.


From that highlighted line I can tell that revelation has downed on you. My fingers are crossed so that every mdanganyika sees the truth.
 
Mimi nilisha sema haya, rostam ndio alikua ameshika pesa za uchaguzi, hata wakati mambo yamekua magumu zanzibar, pesa zilitoka nyumbani kwa rostam Dodoma na kupelekwa zenji. Chumba kizima kilikua na masanduku ya pesa. Hizi habari alitoa mbunge mwenye asili ya kiarabu ambaye alikua rafiki mkubwa wa rostam. Inajulikana wazi kabisa kua hata lowassa alichaguliwa na Rostam sio kikwete. Kwasas huyu jamaa amesha kimbiza hela zote dubai kwa mdogo wake, Fatilieni company iko Dubai inaitwa Rostamani. Mtajua ni ya nani.

Mkuu kuhusu Kampuni hio ya Rostamani naona utaanza kupoteza ushahidi mapema...kama huna Hakika na jambo waache wengine wanaojua...na si kudhani...

Huenda kuna kampuni ingine...sio hio ulotaja...Tafiti then Jadili
 
I refuse to be so pessimistic because I have seen some hopeful signs, I believe watz si mabwege tena na 2010 utakuwa mwaka mgumu sana for CCM. Mark my words!

Mimi ninafikiri itakuwa Bora kama Opposition waungane either practically na kuingia kama Chama Kimoja or Technically kumuunga Mkono Prof Ibrahim Lipumba, then CUf wawa support vyama vingine kutegemeana na Mgombea mwenye nguvu sehemu fulani eg Chadema sehemu walipo na Nguvu, UDP sehemu walizo na Nguvu na hata wabunge wa CUF sehemu walizo na Nguvu, na wakakubaliana Eg wakishanda So and So atakuwa PM toka Chama kingine, Waziri waFedha wa Chama kingine, na hata ku-crate Deputy PM etc etc, bila hivyo ushindi hauwezi kuwa Mnono
 
Rostam Azizi.

Who is Rostam Azizi? Why Rostam Azizi? Where is Rostam Azizi?

Millions of Tanzanians against one - Rostam Azizi. Just one!.

How?
 
Tukatae zile fomula mbili za amani na utulivu


Hatuna hamani na utulivu hstuns kabisaa. Najaribu kuvuta pumzi, najiandaa kuangalia uwezekano wa kujitoa muhanga. is better nife na angalau mafisadi kadhaa kuliko watanzania mamilioni watoto, akina mama, wazee, na vijana wanakufa kwa vifo vinavyo zuilika huku mafisadi wakikomba kila kitu. HAPANA, HAPANA. Namkumbuka sana John Garang kunawakati alisema Vita huleta Kuheshimiana. Amani na Utulivu ni Ujinga wa Tanzania, ni kivuli cha woga wetu! Plz watanzania hivi vita ndo vimeanza kila mmoja atumie silaha anayoona inamfaa.
Kama ni sheria sawa, kama ni rungu na panga sawa, kama ni bomu la kujitoa mhanga na angalau hata kuua fisadi mmoja poa tu. Tutakutana mbele kwa mbele. tumegeuzwa Mazezeta kwa muda mrefu sana. NO! NO! NO! ITS OVER! Wana JF tutakutana mbele ya safari, iwe bongo, mbinguni au Jehanami. kila laheri katika vita hivi vizito!!!!!!!!
 
Msiwe na wasiwasi... this is bigger; na mwali hamalizwi kuchezwa kesho si unajua tena kwenye vijiji vingine sheria hadi siku saba..!

Wengine hatulali mwanakijiji tuinasubiri huyo mwali. Tunaomba mungu mwali atukute taa zetu zina mafuta(tuweze kuzifanyia kazi taarifa) na na za mafisadi hazina mafuta (wazarau kama kawaida yao mpaka moto uwachome)

Pamoja na hamu kubwa tuliyonayo ya kumwona huyo mwali lakini bado tuko wavumilivu kwani mambo mazuri huwa hayaitaji haraka, hivyo chukua muda unaoona unafaa ili nguvu yako ispotee bure.

Mimi binafsi napenda kukushukuru kwa nguvu kubwa unayoitumia kutetea wanyonge na ni lengo langu kukuiga ili nami niwe na moyo huo wa kutetea wanyonge actually diyo agizo kuu la Yesu ( Mpende Jirani yako kama nafsi yako)
 
Nimeona kichwa cha habari kuu ya MwanaHalisi la leo lakini hakijanipa picha ya mwali. Kimeendeleza yale yale ya mkanganyiko kuhusu nani anamiliki Dowans. Ngoja nilitafute gazeti lenyewe nione kama kweli mwali yupo au Champaign imekataa kulipuka!
 
Nimeona kichwa cha habari kuu ya MwanaHalisi la leo lakini hakijanipa picha ya mwali. Kimeendeleza yale yale ya mkanganyiko kuhusu nani anamiliki Dowans. Ngoja nilitafute gazeti lenyewe nione kama kweli mwali yupo au Champaign imekataa kulipuka!

Dark City


mimi nimesoma na habari yenyewe ni mpya na inafanana na habari alizokuwa anatupa kwa vipande mwanakijiji ingawa kicha cha habari siyo kizuri sana kinaonekana kama mwendelezo wa habari za nyuma zilizozoeleka wakati maelezo ya ndani ni kitu kipya kabisa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom