Mkandara haya mambo yanachanganya kweli,ndio maana nimepitia hii thread na nimekuta member huyu "Maskini Mimi" ambaye slogan yake inasema "Lakini tutafika" Kweli najiuliza maswali mengi sana...Hivi tutafika? Kama alivyosema halisi hapo nyuma...Nadhani inabidi tujitolee muhanga kwaajili ya next generation,kwasababu mabadiliko yatakuwa magumu sana na kwasababu hiyo jitihada za ziada zinahitajika...Hatuwezi kusema biashara ya unga for instance ni mbaya na wakati mizungu ya unga inavyopeta kila mtu anataka kuwa zungu especially vijana wanaokua...Sasa ni the same kama alivyosema Halisi...Hata watoto wanadhani ufisadi ni jambo zuri kwani maisha ni mswanu,yani mtoto anaweza akawa anasoma huku akiwa anataka kuwa fisadi when he/she grows up. Ni lazima tubadili,lazima watoto wasikie fisadi liko jela ama limehukumiwa kifo nk...Hapo nd'o utakuwa mwanzo. Other than that mkuu kizazi kijacho kitajiuliza na sisi tunataka mabadiliko ili wasije kujiuliza kuwa tulifanya nini baada ya babu zetu kugombea uhuru.