Mwakyembe apanda treni kwenda Bungeni Dodoma

Mwakyembe apanda treni kwenda Bungeni Dodoma

Ninafikiri sio suala la kumshangaa na kumshambulia kuwa anatafuta cheap popularity. Ni vyema tukampa nafasi ya kusikia. hata kwa kusafiri na treni, naamini hata asiposema kitu, basi wenye mamlaka na walio katika wajibu huo tayari tumbo moto, kama ilikuwa hakuna usafi watasafisha, at least hilo pia ni hatua. Kwa hiyo suala la shangingi kwenda dodoma au la sio issue, hapo ni kutaka kuona uhalisi wa huduma tunazopata, ikifika mahali wakaleta watoto shule za kawaida, shule za kata, dispensary za vijijini basi huduma itaingizwa katika mjadala wa kuona nini kifanyike. Tusihukumu, tusubiri tusikie nini kitatoka katika safari hiyo, na hatua zitakazochukuliwa. Ndilo tunalosubiri...
 
itakuwa imeenda tupu, halafu watanzania walivyo wepesi kuchotwa akili wamemuona boooonge la waziri
wamemuona zaidi ya waziri na wataona huyu ndiye kumbe changa la macho watu wanajiandaa na 2015
 
Meneja kutembelea eneo lake la kazi kwa wakati wowote, kwa staili yeyote ni sawa. Kujifunza matatizo ya eneo lako la kazi ni sawa. Taarifa zinapatikana kwa njia mbalimbali. Kupata first hand info pia ni sawasawa kabisa. Lakini safari haiishii hapo tu! Ni nini kitafanyika baada ya kupata taarifa ndio kitakachoonyesha kama Dr. Mwakyembe yuko serious ama la. Bado tunasubiri. Reli itafufuka? Shirika la ndege litafufuka? Bandari itafufuka?
 
According to Clouds FM,
Dr Harrison Mwakyembe amefanya supprise visit na kusafiri kwa treni kutoka Dar kuelekea Dodoma kuhudhuria kikao cha bunge. Mud si mrefu tutafahamu alichokusudia kufanya hiyo suprise.

hii yote ni mkakati wa 2015.
 
Huyo nilikuwa namuamin sana lkn kumbe nayeye gamba tu mfano.TAZARA kuna mafisad nane walifukuzwa na omar nundu wazir aliyemtangulia sasa mwakyembe,body na baraza la mawazir wanataka wawarudishe sababu hawajaiba sana nayeye atupishe...ALUTA KONTINUA
 
Nasubiri kauli yake kuhusu ile idadi kubwa ya abiria ambao huwa wanasimama na wengine kukaa hadi vyooni kwa kukosa viti. Inawezekana kabisa ndani ya hizi treni zetu watu wanaosimama huwa ni wengi kuliko hata waliopata viti na kukaa!
 
me sion cha ajabu hapa,,,,,tujiulize kwanin amepanda train,,,ili iweje labda tuanzie hapo

Mkuu tujifunze kuwa na mawazo chanya. Yeye ni waziri wa uchukuzi hivyo kaamua kwenda kuangalia hali halisi ya usafiri ndani ya TRL kukiko kusubiri kuambiwa. Kumbuka huu ni usafiri unaotumiwa na watu wengi sana wa kipato cha chini na cha kati. kwa maneno mengine "Kitanda usichokilalia hujui kunguni wake". Tuachane na hypothetical thinking
 
Ni jambo la kawaida kwa raia lakini ni jambo la ajabu kwa waziri kupanda treni Tanzania.
 
Kulikua na sababu ya kuwaambia waandishi wa habari? Huyo jamaa yako ni mpenda sifa za kipuuzi!
Mkuu tujifunze kuwa na mawazo chanya. Yeye ni waziri wa uchukuzi hivyo kaamua kwenda kuangalia hali halisi ya usafiri ndani ya TRL kukiko kusubiri kuambiwa. Kumbuka huu ni usafiri unaotumiwa na watu wengi sana wa kipato cha chini na cha kati. kwa maneno mengine "Kitanda usichokilalia hujui kunguni wake". Tuachane na hypothetical thinking
 
Good example, hata kama anatafuta kuuza sura kwenyr news bado ni mfano mzuri sana na wa kuigwa tunahitaji viongozi wanaokwenda kwenyr roots za matatizo, big up

Na unaamini kabisa kabisa kuwa huko ndiko kwenye root ya tatizo? Kama yeye anafikiria kama wewe, then hataweza kutatua taizo la shirika la Reli, hukokuna outcome tu ya tatizo, taizo liko ndani jengo la wizara yake ambapo ofisi zake zipo. Angeanzia hapo, huku kwingine ni kutafuta huruma ya wananchi tu, ni kama JK anavyohudhuria misiba na kubeba masanduku ya wafu. Hayo yoote ni mema but hayawezi kuisaidia nchi kupunguza deni la taifa toka trillion 22, hayatapunguza mfumuko wa bei, hayatapunguza mabehewa machafu na huduma mbovu ndani ya treni, hayatajenag reli mpya, hayataleta engine mpya za kuweza kuvuta mabehewa mengi ya mizigo sana sana kuwepo kwake kutawatisha wafanyakazi na wahudumu na kuwafanya watoe huduma ya woga na ya unafiki kwa kuwa waziri yupo ndani ya treni
 
Nasubiri mjengoni hawa jamaa watatoka na lipi ili kudhihirisha wanachotuaminisha.
 
Na unaamini kabisa kabisa kuwa huko ndiko kwenye root ya tatizo? Kama yeye anafikiria kama wewe, then hataweza kutatua taizo la shirika la Reli, hukokuna outcome tu ya tatizo, taizo liko ndani jengo la wizara yake ambapo ofisi zake zipo. Angeanzia hapo, huku kwingine ni kutafuta huruma ya wananchi tu, ni kama JK anavyohudhuria misiba na kubeba masanduku ya wafu. Hayo yoote ni mema but hayawezi kuisaidia nchi kupunguza deni la taifa toka trillion 22, hayatapunguza mfumuko wa bei, hayatapunguza mabehewa machafu na huduma mbovu ndani ya treni, hayatajenag reli mpya, hayataleta engine mpya za kuweza kuvuta mabehewa mengi ya mizigo sana sana kuwepo kwake kutawatisha wafanyakazi na wahudumu na kuwafanya watoe huduma ya woga na ya unafiki kwa kuwa waziri yupo ndani ya treni
Na akijichimbia kwenye jengo la wizara yake tu mtasemaje? I guess itakuwa hivi..."Waziri mwenyewe anajifungia ofisini tu hajui hali halisi ya reli Tanzania"...wakuu hata kama tunaichukia CCM saaaana, vitu vingine tujaribu kuvitazama tukiwa na fikra huru. Waziri wa Nishati naye alizuka tanesco akakutana na madudu,magufuli hata hatuna haja ya kumsema maaa barabara anazisimamia mwenyewe...Huko wizarani ndiyo makao makuu ya kazi yake mwakyembe , kuna ubaya gani kuingia field kidogo na kujionea hali halisi?
 
kaenda kutujazia tuu treni wakati bado gari yake itaenda dodoma kwa gharama zile zile.
Kama yupo serious akifika huko dodoma atumie daladala na siku ya kurudi arudi tena na treni.
 
Hakuna tofauti na ziara za Jakaya Kwenye ofisi za wizara. Matatizo ya hizo treni yako kwenye ofisi huku makao makuu, muache atafute cheap popularity, atapoteza vyote viwili, mtoto na mbeleko.
Inapotokea Waziri kuanza kufuatilia Taasisi ambazo ziko chini ya Wizara yake nakutaka kufahamu changamoto zinazowakabili basi hilo ni jambo jema,sikuzote hauwezi kutoa maamuzi kwa kitu ambacho haukijui Dr Mwakyembe amechukua hatua za makusudi mazima kufanya jambo hili tena ni kwa manufaa ya Watanzani wote,hhebu tumpe hongera zake na ninadhani hatafuti popularity! Yeye tayari yuko popular toka enzi za Richmond kilichobaki kwake ni kuchapa kazi tu Honger sana DR Mwakyembe!
 
urais unatafutwa kwa nguvu zote!

kwangu mimi siyo swala la Urais. Walitakiwa viongozi wetu wote wafanye the same. Huwezi tatua kero za wananchi kama utakuwa kwenye viyoyozi. Ni lazima watest flavor zetu ndo watoe ushauri na maamuzi sahihi. You cant understand roaches life through microscope. You have to live like a roach in order to know how it feels.
 
2015 nini??!!unafkiri akidaka uongozi slaa utalalia godoro la dhahabu,kutafuta kwako mafanikio ndiko kutakutoa kimaisha,hivi kupiga kwao kelele mpaka kukauka sauti unadhani ni kwa maslahi ya wananchi kweli??!!
siasa ni mchezo mchafu wanaujua wanasiasa wenyewe tu,chambo ni mwananchi ni kama mkimbiza mwenge wakubwa wanakula mafao wananchi wanaambulia kuhema tu.
 
Wewe sasa umechanganyikiwa watu wasifanye kazi kisa wanatafuta urais kwa hiyo ulitaka matatizo ya Reli ayajue vipi bila kusafiria treni acheni utoto

ujuha tu unaanza kuwa na wasiwasi na urais umeona unaemtaka anazi kuishiwa! watu wasifanye kazi eti urais! Mwakyembe we chapa kazi humu JF kuna watu wengine ninadhani ndio ajira zao kuja kufanya kazi ili jioni walipwe!
 
Back
Top Bottom