kwa hiyo shangingi linabaki dar au?
kweli tunastahili umaskini tulio nao. kama tunamponda mwakyembe kwa kupanda treni hii ni hatari
Sion cha ajabu lamda angapanda tingatinga
Sifa za kijinga.
According to Clouds FM,
Dr Harrison Mwakyembe amefanya supprise visit na kusafiri kwa treni kutoka Dar kuelekea Dodoma kuhudhuria kikao cha bunge. Mud si mrefu tutafahamu alichokusudia kufanya hiyo suprise.
Mpwa amepanda first class halafu sasa hiyo surprise ameitoa wapi na booking najua pale mpaka wiki 2 ndio unapata nafasi !
kwa hiyo shangingi linabaki dar au?
urais unatafutwa kwa nguvu zote!
Shida ya wanasiasa hasa wa bongo usanii umezidi, tafakari yangu, nafikiri atakua amechoka kuapata kiyoyozi cha VX V8 au ndege, nikawaida starehe ikizidi binaadamu hutafuta karaha kwakua hua anikosa kukamilisha balansi.
Mkuu ulilolisema ni kweli kabisa, kweli kabisa, kweli kabisa, kweli kabisa,Kweli duniani hakuna jema! Mwakyembe akila kuku katika uwaziri wake mtasema ooh, mzembe huyu, wanapeana tu uwaziri hawa CCM. Akichapa kazi, oooh, huyu bwana anatafuta uraisi kwa nguvu zote!
Jamani Watanzania, hivi mnajua mnachotaka kweli? Mie nadhani mnataka mkoloni arudi atutawale, kila mtu akose. Maana sasa naanza kuhisi kama haya mambo yote ya CM Vs Chadema hakuna lolote bali ni fitina wivu na majungu tu, si uzalendo kwa ajili ya nchi yetu. Hamna jema litafanyika mkasifia, bali kutafuta visababu tu vya kumsema mtu. Nina uhakika hata Chadema wakichukua nchi nyie hao hao mnaoshabikia Chadema leo mtakuwa wa kwanza kupiga kelele!
Hebu msikie aibu mara nyingine kusema watu ili mradi basi tu mseme.
Msimamo wangu uko pale pale, huyu Jamaa ni Mmoja kati ya wanasiasa waongo katika Taifa hili, ni mmoja kati ya wanasiasa wanaotafuta sifa zisizo na msingi wowote ule, na katika hili anatafuta cheap popularity.
Mpaka sasa kitu pekee nachojua anaweza kukifanya kwa ufanisi mkubwa ni kutengeneza uongo na kuchafua watu wengine, Mpaka siku atakapoliambia Taifa ni mambo gani kamati yake ya Richmond iliyaficha kwenye report yake ndio naweza nikaanza kumsikiliza.
Mtu yeyote makini ni lazima ajiulize, kwa nini CCM inashindwa kumfukuza Lowasa with all the damage kamati ya mwakyembe ilimfanyia ni lazima aquestion credibility ya huyu jamaa.