Tumedanganywa kiasi cha kutosha pia.Mimi siku ya kwanza kumfahamu Kitwana Kondo miaka ya 1990 aliingia kwenye daladala al maarufu chai maharage akashuka Makumbusho,japo niliambiwa watoto wake walikuwa wakitembelea M/benzi wakati huo huo.Mwakyembe anaingia kwenye rekodi ya Wachekeshaji wa CCM: Augustine Lyatonga Mrema alikamata VIGOGO Dar International Airport,hadi leo takribani miaka zaidi ya 20 hajataja jina!JK alisema wala rushwa na vigogo wa madawa ya kulevya anawajua kwa majina na hadi leo hajataja hata initials za jina la mmoja akiwa yeye ni Amiri Jeshi Mkuu!Mwakyembe alishajiuzulu Bodi ya NBC Ltd akitii pia DHAMIRI yake kabla ya kuwa MBUNGE.Mwenzie mtoto wa MKULIMA alikataa shangingi moja tu lililonunuliwa kwa indhini ya ofisi yake,akiwa pia ameidhinisha mengine mengi kwa ajili ya Waheshimiwa wengine,hii ni chini hata ya kiwango cha uchekeshaji,maana inatia huruma(soma aibu)
Kama anataka kuthibitisha kwamba ana uchungu na TAIFA HILI athubutu kufanya haya:
Aaachane na Serikali ya CCM ambayo kwa utafiti maarufu wa Kamati ya Bunge kuhusu Richmond,ilithibitishwa kuwa ya kifisadi kiasi cha kuanguka,ukiacha kwamba yeye na waheshimiwa wenzake ktk kamati ile waliamua kuficha(soma kudanganya) kuhusu mambo mazito zaidi yaliyohusu Richmond:
Apime wapi kuna wapambanaji wa kweli aungane nao siyo lazima kama mbunge ama kiongozi katika kudai haki za kimsingi ikiwemo katiba na miliki za nchi kwa uwezo mkubwa alionao akiwa mbobezi ma mzamivu kwenye maeneo hayo kisheria
Afanye kazi ya mzee wa falsafa SOCRATES,ARUDI UDSM au maeneo kama hayo ili aelimishe vijana na kuwasemea waliozibwa midomo wapate haki zao za msingi
Athubutu kumtaja hadharani kwa majina matatu aliyeunganisha mission ya yeye kutegeshewa sumu ma kuumia kimwili kiasi hicho,UKWELI huu utamweka yeyey na wananchi na huyo haramia huru!
Hii ya kukesha na wasafiri waliokwama TAZARA ama kupanda treni ya karne ya 17 Ulaya haitasaidia kuleta treni za kisasa ,bandari ya kisasa wala kuifufua ATCL,UDA,TRL, wala TAASISI za aina hiyo.NA JUU ya hayo haiwezi kuwa mbinu ya kuwadanganya watanganyika wote wakati wote kwamba yeye ni bora kuliko mfumo wa kifisadi uliomfikisha hapo alipo na ambao kwa ujasiri mkubwa wa.....ameamua kuutumikia hata kwa gharama ya kichwa chake!