Mvua kubwa Dar usiku huu kuamkia 20 Jan 2024. Je maeneo yenu kuna maafa?

Jumamosi hii wanaoenda kazini wanalaani hatari, ila ambao hawaendi kazini ni kulala hadi njaa iume kisawasawa ndo waamke kupika.

Hongereni kwa hali ya hewa nzuri, pole kwa wanaoishi maeneo ya chini ya usawa wa bahari maana mafuriko hayatawaacha salama.

Huwa sielewi kwanini Tanesco hawapatani na mvua, ikinyesha tuu umeme usipokatika basi hilo eneo limebahatika.

Poleni kwa yote, ndo maisha.
Tunachkua tahadhari kabla ya hatari ndugu mteja. Maeneo ya makaz miundombinu huwa inaweza kuwa na shida
 
Sijawahi kuogopa radi za Dar mpaka nilipofika mkoa fedenge ilipiga nikajikuta uvunguni aroo nilijua bati limetoka lote. Ile ilikua sio radi bwana vigagula wanatoa na dedication humohumo wanaongezea mlio
Radi zenu watu wa dar. Njoo katavi huku uelewe shoo. Asubuh Asubuh tetemeko na ikinyesha unahiz kufa kufa maana inabomoa radi kama hasira.kwa maeneo yote yenye madini vitu vya kawaida
 
Mimi ni muoga wa radi kuliko kitu chochote ilikua radi zikianza usingizi unakata mazima ntatoa macho mpaka ziishe. Sasa nikanunua ear plugs ambazo kukiwa na radi nazipachika masikioni zinakata sauti sisikii chochote! Balaa lake ni kwamba unalala usingizi kama mfu yaani husikii chochote hata nyumba ikiungua we lazima utafia humo 🙁
Mkuu una uoga mpaka uoga wenyewe unaogopa kukusogelea😀
 
Back
Top Bottom