Mvua kubwa na radi jijini Dar es Salaam na Pwani yote. Mtaani kwako kwema?

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,664
Unaweza kusema ndio mvua kubwa tangu tuanze mwaka 2020 na imeanza kwa kasi kubwa tangu saa kumi usiku na bado inapiga, nimepita mitaa ya Mlandizi, Kibaha, Mbezi Mwisho, Ubungo hadi nafika katikati ya Jiji mvua inatwanga tu.

Njia zote zimejaa maji na hasa pale Jangwani na maeneo mengi, hii sikuisikia jana TMA wakiitangaza nadhani hawakuiona kwenye rada zao.

Pia mvua hii imeungana na radi kubwa kiasi cha wale ambao hawakuzoea kuwatisha kiasi na miale ya radi.

Vipi mtaani kwako kuko salama? Hakuna maafa?

DART inatoa taarifa kwa umma kuwa sehemu ya Jangwani katika barabara ya Morogoro haipitiki kwa sababu ya mafuriko yanayotokana na mvua iliyonyesha usiku wa kuamukia leo, Alhamis, Januari 16, 2020.

Tunawashauri wasafiri wa mabasi ya Mwendokasi wanaotokea Kimara kuelekea mjini-kati kuwa watumie mabasi hayo mpaka Morocco halafu wachukue usafiri mbadala ikiwemo daladala mpaka mjini-kati, Kariakoo na sehemu nyingine za jiji.

Hivyo hivyo, wale wanaotokea mjini-kati kwenda Kimara wachukue usafiri mbadala mpaka Morocco ambapo wanaweza kuendelea na usafiri wa mabasi ya Mwendokasi kuelekea Kimara na nyingine za jiji.

Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani jijini Dar imefungwa baada ya maji kujaa kutokana na mvua kubwa inayonyesha jijini Dar
1579160621827.png

Hali ilivo jijini Dar baada ya barabara ya Jangwani kufungwa
1579160722450.png

Hapa ni daraja la Kitunda kuelekea Banana Stand, jijini Dar es salaam.
1579160758671.png

Foleni Barabara ya Bagamoyo kuelekea maeneo ya Kinondoni & katikati ya Jiji asubuhi hii. Tatizo la msongamano wa magari katika bararaba kuu za jiji la Dar Es Salaam huongezeka wakati wa mvua, sababu moja ikitajwa kuwa ni ubovu wa barabara ndogo ambazo hazifai kutumika wakati huo.
1579160834635.png

Hali ya foleni ya magari katika kipande cha barabara kati ya Morocco na Victoria Jijini Dar es Salaam. Mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji hilo zimesababisha baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii kusimama kwa muda.
1579160887143.png

Mvua inayoendelea kunyesha Dar es salaam hali halisi baadhi ya maeneo ulivyo hapa Ni sinza darajani

Video ya kwanza ni eneo la Bamaga barabara ya Shekilango jijini Dar es Salaam ambao maji yamejaa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Video ya 2 hali ilivyo kwa sasa barabara ya TAZARA daraja la Mfugale na Video ya 3 ni barabara ya kuelekea Mikocheni kutokea Morocco.


 
Mvua ni kubwa sanaa
Katika maeneo ya Mbagala na barabara hii ua Kilwa road kwa sehemu ya Mbagala imejaa maji upande wa kutokea zakiemu kuelekea Mbagala, Chamazi, Kisewe Charambe, Maji Matitu mvua ipo lkn haina madhara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unaishi Mlandizi unafanya kazi town au umetoka safari?

Kama unaishi Mlandizi nakufanya shughuli zako mjini daily sipati picha gharama za usafiri.
 
Back
Top Bottom