Muswada wa kuzuia Maandamano nchini waja...

Nchimbi chupi inamvuka imefika magotini,mlianzisha mwongozo wa spika mmechemka,mkaanzisha kanuni na taarifa kwa spika mkizani mtawadhibti cdm badala yake mmeshindwa mmebaki kufikiria kutunga miswada ya kijinga hivi ni PhD ya lumumba?Mkifuta maandamano TUTATEMBEA,mkifuta kutembea tutakimbia,mkifuta kukimbia tutatambaa mbunge mmoja wa cdm ni sawa na wabunge 30 wa magamba.
 
...na hii yaweza kudhihirisha kuwa Tawala wameishagundua kuwa wameishachelewa meli ya kuikalia kidharau nchi hii tena baada ya 2015.
 
Katika hali ya kusikitisha na kushtusha Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi ameliambia bunge jioni hii kwamba serikali ya CCM imeridhia kuleta mswada bungeni ili itungwe sheria ya kuzuia maandamano kote nchini.

Nchimbi amesema hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoa uvunjifu wa amani nchini unaofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa.Waziri amesema mswada huo utaletwa wakati wowote kuanzia sasa akimaanisha tayari umeshakamilika.Nchimbi alikuwa akishangiliwa sana na wabunge wa CCM wakati alipokuwa akitamka maneno hayo.

Hili litakuwa ni pigo kubwa kwa demokrasia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Ikumbukwe ni hapo jana tu Chadema kilidai kunasa mpango wa siri wa serikali ya CCM wa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ili kukidhibiti Chadema na kukiimarisha CCM.

Kazi kweli kweli.

watakuwa wanakiuka haki za binadamu ambazo Tanzania ilisaini azimio hilo la UN
 
Huyu jamaa anafaa kuwa PM kwenye Serikal ya Brother Edo lowassa!
 
Jamani jamani kwa nini mnapenda kupotosha mambo! Amesema sheria ya kuweka uaratibu mzuri na muafaka wa maandamano... Ambayo itaonyesha yanaruhusiwa kwa mfano siku zipi? Muda gani na barabara zipi kwa mfano,... Wanaopokea maandamano au wakusanyikie wapi? Nadhani nia
kwa mfano haingii akilini ati maandamano kupitia mtaa Kongo pale kariakoo m2 aniambie nia hii Ina tatizo gani?
 
hiyo itaishia mdomoni hawezi kutunga sheria inayopingana na katiba,

mkuu sonotorious, hiyo sheria ili ifanye kazi itabidi na katiba nayo ifanyiwe ifanyiwe amendment. huwezi kutunga sheria ambayo inapingana na sheria mama ambayo ni katiba nchi. maccm ni mashetani mabaya sana. they think that they will be in power forever, never!
 
Hakuna mtu mwenye haki ya kufuta haki ya Kikatiba ya mtu mwingine. Zaidi zaidi akitokea mtu huyo basi atakuwa anatumia ubabe ambao hauna tija katika taifa hili changa ambalo bado linachemea kimaendeleo hasa kiuchumi. Haki ya kuandamana ni haki ya kimsingi hususani kwa watu wanyonge ambao malalamiko yao yanabezwa. Na kuandamana sio tu kuenda against na serikali inavyotaka bali ni kudemonstrate matatizo flani ambayo jamii inakumbana nayo, au maadhimisho ya kumbukumbu flani na wakati mwingine yanatokea wakati jamii inaunga au kupinga jambo flani, Mpaka hapo sijaona ubaya wa maandamano. Napata shida sana kumuelewa Nchimbi.
 
mkuu. si kila viongozi wa upinzani wanafurahia maandamano. wengine wanachukia kweli. binafsi sijawahi kumuona zitto kabwe akihamasisha au kushiriki maandamano. hutoa hoja zake kwa ufasaha na anaeleweka sana. ila hawa wengine ni janga la taifa. kwa vile wameshindwa darasani ndo hata uwezo wa kufikiri kwa busara hawana

VIPI BADO HUJAWAHI KUMUONA AU na inaeleka wewe ni mtoto sana wa sisa za BONGO laiti ungejua kuwa maandamano ndio yalio mweka ZITTO hapo alipo leo baada ya kufukuzwa Bungeni usingesema hayo.( ni mekukumbusha unakumbuka?)
j3%2022.jpg
 
Hizi ni dalili za uchovu wa fikra.

Hivi kwa yanayoendelea hapa nchini badala waziri husika kufikiri ufumbuzi ni kitu gani, anaamka na kufikiri jinsi ya kuzuia maandamano. Hizi ni kama ndoto za mchana

Nachelea kusema kwamba we have tired guys in position.

Vichwa vinavyosolve tatizo huwa vinafikiria karibu na tatizo na sio kuleta solution ambazo hazihusiani na tatizo lililopo.
 
Nchimbi hajui alama za nyakati, anaweza kuleta mswaada huo na ukapita kwa sababu tu ya uwingi wa wabunge wa CCM. Lakini hajui madhara ya kufunga mwanadamu mdomo, angejua hilo asingewaza kitu kama hicho. Binadamu sio robot, na ulimwengu mzima watu nchi zinahamasisha freedom of press, ambayo ni pamoja na kuonyesha hisia zake ikiwa ni pamoja na maandamano. Leo hii anafikiria kuzuia maandamano, nchi yenyewe bajeti inategemea wafadhili, wakigoma kwa sababu ya kukandamiza demokrasia, haipumui. Kuzuia maandamano ni udikiteta na kushindwa kwa serekali na hivyo kutafuta njia ya kutokea. Kwanza miswaada ya nini wakati katiba mpya inaandikwa? Kweli CCM inatapatapa. By the way, eti Nchimbi naye alikuwa kwenye list ya wanaoutaka uraisi?
 
CDM mmekuwa mnatumia maandamano kuwa ni chanzo cha kuvunja AMANI na UTULIVU nchini. Siasa za majukwaani bila fujo hamziwezi hivyo bila maandamano CDM katika jeneza

Magamba mnashida kweli. Taabu yenu sio wabunifu, mtapelekeshwa hadi mbaki makalio wazi. CDM wanatumia strategy mbalimbali kuendesha siasa zake ambazo kila kukicha uungwaji mkono unazidi kuongozeka. Mnakumbuka kuwa Dr Slaa aliwaambia kuwa kwao maandamano ni moja ya strategy zao za kizamani? Mtaishia kushika manyoya ya mkiani wakati mwendo ukizidi kushika kasi.

Lakini nimishauri Magamba, brashi hizi za chuma ndizo zitakazokujakutumika wakati huo mkiwa upande wa pili. Uzuri ni kuwa sisi tunazidi kuieneza CDM bila kugawa kadi wala mikutano, kwani tunaisimika miyoyoni mwetu bila hata hayo maandamano na mikutano.

Endeleeni na mibunge yenu isiyo na kichwa ndani ya vikao vya bunge kwani kwetu ni mtaji mkubwa kuliko hayo maandamano kuwaonyesha Watanzania jinsi Magamba yalivyo.

Du, leo niliicheki Migamba yote bungeni, angalao niliyemuona kama muwakalishi wa Watanzania alikuwa Sitta. Hapo, tunahitaji maandamano ya nini? Labda ya kufanya standardisation ya matokeo ya kidato cha nne, kufisha udhaifu wa serikali!
 
katika hali ya kusikitisha na kushtusha waziri wa mambo ya ndani emmanuel nchimbi ameliambia bunge jioni hii kwamba serikali ya ccm imeridhia kuleta mswada bungeni ili itungwe sheria ya kuzuia maandamano kote nchini.

Nchimbi amesema hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoa uvunjifu wa amani nchini unaofanywa na watu wasiolitakia mema taifa.waziri amesema mswada huo utaletwa wakati wowote kuanzia sasa akimaanisha tayari umeshakamilika.nchimbi alikuwa akishangiliwa sana na wabunge wa ccm wakati alipokuwa akitamka maneno hayo.

Hili litakuwa ni pigo kubwa kwa demokrasia katika ukanda huu wa afrika mashariki.

Ikumbukwe ni hapo jana tu chadema kilidai kunasa mpango wa siri wa serikali ya ccm wa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ili kukidhibiti chadema na kukiimarisha ccm.


kazi ya kichwa sio kufugia nywele ni kufikiria pia= attony general
 
Ukipita Tanzania inakuwa nchi ya kidikteta kubaka haki za kibinadamu
 
Badala ya kufikiri majangili yakabiliwe vipi unafikiri maandamano. Anyway zuieni maandamano lakini BALAA linalokuja TUSILAUMIANE.
 
Back
Top Bottom