Muswada wa kuzuia Maandamano nchini waja...

Muswada wa kuzuia Maandamano nchini waja...

hapo ndo utaamini viongozi wanaongoza kwa hisia na si kutumia medulaoblangata.usishangae baadae ikaja na mswada wa kutakiwa kulala ifikapo saa kumi kamili jioni.
 
Democrasia ya wapi hiyo, Au ya Nchimbi katika nchi ya wagagagigigogo!

Ila wajue maandamano ni moja ya njia ambayo wananchi hudai haki Yao Na kutuliza hasira zao.

Wakikataa maandamano basi wajiandae kwa mengineyo
 
Katika hali ya kusikitisha na kushtusha Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi ameliambia bunge jioni hii kwamba serikali ya CCM imeridhia kuleta mswada bungeni ili itungwe sheria ya kuzuia maandamano kote nchini.

Nchimbi amesema hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoa uvunjifu wa amani nchini unaofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa.Waziri amesema mswada huo utaletwa wakati wowote kuanzia sasa akimaanisha tayari umeshakamilika.Nchimbi alikuwa akishangiliwa sana na wabunge wa CCM wakati alipokuwa akitamka maneno hayo.

Hili litakuwa ni pigo kubwa kwa demokrasia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Ikumbukwe ni hapo jana tu CHADEMA kilidai kunasa mpango wa siri wa serikali ya CCM wa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ili kukidhibiti CHADEMA na kukiimarisha CCM.


Ni ulevi tu wa MADARAKA,kwa kauli hii ya Nchimbi na nyengine zilizokwisha kutolewa na Serikali kupitia watendaji wake ni kuwa wameialalisha nchi hii kuwa ya WATAWALA na sio ya viongozi.Wakithubutu wananchi watadai Tanganyika yao ya Mwalimu Jullius Nyerere.
 
Back
Top Bottom