Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,200
Endapo CCM kitatafuta 'kufingia kabatini' Haki za Binadamu' ikiwemo haki ya mtu au kikundi kuchagua kuandamana ama kwa kuonyesha kutokupendezewa au kule kufurahishwa, basi hadi hapo kuna uwezekano mkubwa Tanzania tukatengwa na jumuiya ya kimataifa tena kwa uchungu mkali na gharama kubwa pia.
Mswada huu ni batili tayari kwa kuwa inapingana na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na UN Human Rights Charter.
Miongozo hiyo miwili zote zinaasisi na kutetea kwa kinywa kipana HAKI NA UHURU WA
(1) raia kujumuika pamoja kuzungumzia yale yanayowahusu;
(2) raia wanazo haki za kukusanyika pamoja na kutumia fursa ya kuelezea kutokuridhishwa kwao na jambo lolote na kuhitajika kupewa ulinzi pindi wanapofanya hivyo.
NB: Hadi leo hii wala sijasikia popote kama taifa letu limejiondoa kufuata sheria na mikataba ya kimataifa ambayo tulitilia sahihi kwa hiari yetu wenyewe.