Muswada wa kuzuia Maandamano nchini waja...

Muswada wa kuzuia Maandamano nchini waja...

Huo utakuwa mwisho wa CDM kisiasa waliozoea kuendesha harakati za kisiasa kupitia maandamano yanayoharisha ustawi wa nchi yetu. Tena ikibidi zoezi hili lianzie Arusha Mjini


Wakati wenzenu wanaharakatika kupata haki mbalimbali mfano elimu na afya wenyeakili fupi hufikilia kudhibiti madai hayo.

Taifa linaangamia, watoto wanafeli kwa takwimu za kutisha, Afya na matibabu ni hali mbaya sana na uhusiano wetu kama watanzania upo mashakani.

Je? haki ya kudai mahitaji ya msingi kwa manufaa ya taifa letu na vizazi vyetu itapatika vipi?

Fikiria maisha ya wajukuu na vituu vyako, ndugu na jamaa zako huko vijijini kabla ujacheuwa mawazo ya ajabu hapa jamnvini.
 
Huo utakuwa mwisho wa CDM kisiasa waliozoea kuendesha harakati za kisiasa kupitia maandamano yanayoharisha ustawi wa nchi yetu. Tena ikibidi zoezi hili lianzie Arusha Mjini


komaa kabisa KICHWA MAJI UBONGO MATOPE.
 
Kwani yatazuiwa maandamano ya upinzani pekee au wote. Kila siku naona maandamano ya kumpongeza mwenyekiti, matembezi (maandamano) ya mshikamano, maandamano ya kupinga kauli ya fulani......so sidhani kama kuna upande utadhurika kuliko mwingine.
 
  1. Kama hujui tatizo siyo chadema kama wao wanyofikiri. Tatizo ni matendo ya CCM kwa watanzania
  2. Kama ni elimu ya uraia Chadema wameshafanya kazi yao na wantanzania wa leo wameshakuwa welevu vya kutosha labda tu hao wenye wanaishi kwa mgongo wa dhulma za CCM
  3. Jingine serikali inajua fika kuwa hali kwa sasa si shwari (WaTZ wameshaikinai serikali hii) na wakiacha mambo yajiendeshe yenyewe kuna uwezekano mtu akatolewa magogoni bila kutarajia.
  4. Hata rafu za kuwatishia na kuwanyazisha wanasiasa, wanaharakati, waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari ni kwasababu wanajua wasipofanya hivyo hawatasalimika
  5. Hakuna kitu kigumu duniani kama kupingana na ukweli/Hali halisi.

Asante kaka majege a.k. a mifupa, umewapa makavu live!!
 
Last edited by a moderator:
Waulete huo mswada na ukipitishwa basi kila Raia wa TZ anakuwa Mhalifa Maana Tafsiri ya Maandamano ni nini si ni watu zaidi ya wawili kutembea barabarani siyo.

Waandae Lupango za Kutosha kuwajaza WaTZ Zaidi ya Milioni 30 wanaopinga dhulum dhidi ya CCM na serikali yake.

Maandamano ya kwanza na Mwisho yatakuwa kuipinga serikali ya CCM kama italeta Muswada huo na ndiyo itakuwa mwisho wake.

Lakini sishangai maana Ziara za Jamaa kwenye nchi zinazoongozwa na Madikteta zimezidi, kila siku mwaliko mwaliko, wa Kazo gani??
 
Mswada huu ni batili tayari kwa
kuwa inapingana na
katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
pamoja na
UN Human Rights
Charter
.

Miongozo hiyo miwili zote zinaasisi na kutetea kwa kinywa kipana HAKI NA
UHURU WA

(1) raia kujumuika pamoja kuzungumzia yale yanayowahusu;

(2) raia wanazo haki za kukusanyika pamoja na kutumia fursa ya kuelezea
kutokuridhishwa kwao na jambo lolote na kuhitajika kupewa ulinzi pindi
wanapofanya hivyo.

NB: Hadi leo hii wala sijasikia popote kama taifa letu limejiondoa
kufuata sheria na mikataba ya kimataifa ambayo tulitilia sahihi kwa
hiari yetu wenyewe.

tatizo hamjui undani wa hili. maandamano ya halali hayawezi kuzuiwa. kitakachozuiwa ni yale maandamano yasiyo na vibali. sheria pia itawapa vyombo vya dola kuwakamata na kuwashitaki wale wote watakaohusika na kupanga na kutekeleza maandamano hayo
 
sera ya ccm hiyo siyo ya serikali!! ana wasiwasi wakiitisha maandamano ya ccm hatatokea mtu hivyo wanaona bora kusiwe na maandamano kwa wote!!! tuna haki ya kuandamana ili mradi yawe maanadamo ya amani!!!!2015 will justify the means
 
Niudhaifu wa serikali tu wala si maandamano. kwani la Arusha na Zanzibar lilichukua roho za watu lilitokana na maandamano?
 
Huo utakuwa mwisho wa CDM kisiasa waliozoea kuendesha harakati za kisiasa kupitia maandamano yanayoharisha ustawi wa nchi yetu. Tena ikibidi zoezi hili lianzie Arusha Mjini

Kwani Arusha wameandamana mara ngapi mkuu.
 
Maandamano wacha yasimamishwe ni kawaida, lakini mikutano iongezewe ulinzi. sawa nchimbi??
 
Kama
ni uwezo wao mdogo wa kufikiri mbona nyie wenye uwezo mkubwa wa
kufikiri linawapa shida???,Hivi kweli wabunge watu wazima wamekaa
bungeni kwamba maandamano yanavunja amani wana nia ya dhati kutatua
matatizo ya Mtanzania? wamekosa cha kufikiri kitakachomkomboa Mtanzania
hadi waone wakizuia maandamano ndio uchumi wa Tanzania utakua??? Akili
ndogo kwa wabunge wote na supporters wao woote humu jf


mkuu. si kila viongozi wa upinzani wanafurahia maandamano. wengine wanachukia kweli. binafsi sijawahi kumuona zitto kabwe akihamasisha au kushiriki maandamano. hutoa hoja zake kwa ufasaha na anaeleweka sana. ila hawa wengine ni janga la taifa. kwa vile wameshindwa darasani ndo hata uwezo wa kufikiri kwa busara hawana
 
Huo utakuwa mwisho wa CDM kisiasa waliozoea kuendesha harakati za kisiasa kupitia maandamano yanayoharisha ustawi wa nchi yetu. Tena ikibidi zoezi hili lianzie Arusha Mjini

Maandamano yako dunia nzima we kilaza,hiyo sheria yenu ya kipumbavu haitazuia maandamano,vilikuwepo vyama vya kibabe dunia nzima na vikatoweka sembuse sisiemu?ila tutafika tu iwe kwa mwendo wa farasi au kinyonga,yote yanawezekana.
 
Hivi kwani waliwahi kuruhusu? Sina historia wala kumbukumbu ya utekelezaji wa haki hiyo ya Kikatiba ktk Tanzania.

I see no difference with or without it on current status.

Kwa watawala "Maandamano halali" huwa ni yale ya '...kumpongeza Rais wetu kwa kuteua Baraza la Mawaziri...' pia yale ya Mei Mosi na yenye kufanana na hayo. Wafute ila wajue tu siku wakikaa pembeni nchi hii itabadilika sana.
 
Vyombo vya habari .e.g Habari Leo wameeleza kuwa watuhumiwa wa tukio la Arusha wako 6 wakiwemo Wasaudia wawili. Kwa maelezo ya gazeti, Wasaudia waliingia nchini Jumamosi kupitia uwanja wa ndege KIA na baada ya tukio walikimbilia Kenya kwa kutumia usafiri wa barabara.

Kwa maana hiyo basi, watuhumiwa wa mkasa huu mkubwa na wenye kutia doa sifa ya Tanzania, hawakuwa kwenye maandamo! Vivyo hivyo, muuaji wa Padri Mushi kule Zanzibar au mtu aliyemwagia tikikali Sheikh Soraga huko Zanzibar hakuwa kwenye maandamo! Wahanga wa meno na kucha hawakuwa kwenye maandamano.Wabeba twiga hawakuwa kwenye maandamano!

Na ukitazama kwa makini matukio yote makubwa hayana uhusiano na maandamano. Nchimbi anaelewa tatizo linaloikabili taifa hili? Na kama hajaelewa kwanini asichukuwe siku walau kidogo ili akisimama mbele ya bunge atoe kauli zenye matumaini?

Watu wakiandamana maana yake kuna tatizo, na hivyo wanapaza sauti kwa mtindo ambao wanaona ndio utawafanywa walengwa kusikiliza kero zao. Kwanini Nchimbi asitafute suluhu ya kero za wananchi halafu aone kama wataandamana? Ukisilikiza hoja za wabunge (baada ya taaraba zao) kila mmoja ana kero za wapiga kura wake, mwaka hadi mwaka, maji, huduma za afya, usalama hafifu, ardhi, huduma za afya, barabara mbovu, ubadhirifu kwenye Halmshauri, matokeo mabaya n.k. Hivi majibu ya haya yote kuzuia maandamano?

Mimi ningempa Nchimbi ushauri tofauti, hebu siku moja akisikia kuna maandamano, aembe kuwa kushiriki kwa maana ya kuyapokea hayo maandamo na kusikiliza wanataka nini? Hili tu! Hii nguvu kubwa inayotumika kuleta sheria inazidi kuiweka serikali na hasa CCM mbali na wananchi, Gharama yake ni kubwa kwa CCM. Pokea maandamano na sikiliza hoja. Huo ndio uongozi bora na wa kimekrasia!
baadhi ya viongozi wetu wakienda kwa madokta wa magonjwa ya akili kupimwa akili watakutwa hawana akili timamu.
 
Kwanza siamini kwamba watanzania wanaweza kuvumilia kukaa kimya kuiona serikali ya ccm ikianzisha sheria ya kijinga kama hiyo.

Pili, kama wakilazimisha na kufanikiwa kutungwa kwa sheria hiyo tutapata njia mbadala ya kuwasiliana na wananchi. Akili ya mwanadamu siku zote inafikiria namna ya kujinasua na vikwazo vilivyopo, tena wakizuia maandamano ndio watakuwa wameturahisishia kazi ya kuwang'oa madarakani.
 
Katika hali ya kusikitisha na kushtusha Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi ameliambia bunge jioni hii kwamba serikali ya CCM imeridhia kuleta mswada bungeni ili itungwe sheria ya kuzuia maandamano kote nchini.

Nchimbi amesema hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoa uvunjifu wa amani nchini unaofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa.Waziri amesema mswada huo utaletwa wakati wowote kuanzia sasa akimaanisha tayari umeshakamilika.Nchimbi alikuwa akishangiliwa sana na wabunge wa CCM wakati alipokuwa akitamka maneno hayo.

Hili litakuwa ni pigo kubwa kwa demokrasia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Ikumbukwe ni hapo jana tu Chadema kilidai kunasa mpango wa siri wa serikali ya CCM wa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ili kukidhibiti Chadema na kukiimarisha CCM.

Yaani Maandamano ndiyo yaliyomleta Msaud Arabia kufanya MPANGO wa kulipua Kanisa la Wakatoliki pekee???
 
Katika hali ya kusikitisha na kushtusha Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi ameliambia bunge jioni hii kwamba serikali ya CCM imeridhia kuleta mswada bungeni ili itungwe sheria ya kuzuia maandamano kote nchini.Nchimbi amesema hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoa uvunjifu wa amani nchini unaofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa.Waziri amesema mswada huo utaletwa wakati wowote kuanzia sasa akimaanisha tayari umeshakamilika.Nchimbi alikuwa akishangiliwa sana na wabunge wa CCM wakati alipokuwa akitamka maneno hayo.Hili litakuwa ni pigo kubwa kwa demokrasia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.Ikumbukwe ni hapo jana tu Chadema kilidai kunasa mpango wa siri wa serikali ya CCM wa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ili kukidhibiti Chadema na kukiimarisha CCM.
Itakuwa ajabu kufanya hivi. Unatatua tatizo kwa kutengeneza tatizo! CCM wanasahau kuwa nao waweza kuwa wapinzani na sheria hiyo hiyo ikawarejea. Lakini haihitaji wao kuwa wapinzani tu kuathiriwa na sheria hii bali hata wakiwa madarakani. Sasa hivi tunamwona Katibu mkuu wa chama chao hakizunguka kufanya mikutano mikoani. Hawahitaji kuangaika na suala hili kwani watu hawalazimishwi baadaye haya yataisha. Wape uhuru watu watajitawala.
 
Huyu Nchimbi naonaga kichwa yake haina wazo la kufikiri chochote zaidi ya ujinga wa maneno isiyo na tija anayoropoka tu!
Anatumia masaburi yake kuwaza na kutoa kauli jinga kama hiyo!

chimbi ndio kiboko ya slaaaa
 
Back
Top Bottom