Kuna uwezekano mkubwa wa kuleta mswada huo na ukapitishwa kwa kura nyingi za wabunge wa maccm. Hii nikutokana wsbunge wengi na mawaziri kusimama wakiongea propaganda nyingi kupinga maandamano.
Tunchopaswa kujua nikuwa ccm iko tayari kufanya lolote (liwalo na liwe) ikiwa ni pamoja na kuvunja katiba na mikataba ya kimataifa walioisaini wao wenyewe ilimradi waendelee kushika dola.
Ushauri wangu: Kuanzia sasa mpaka apo mswada huo utakapopitishwa kuwa sheria tufanye haraka kuwambia wtzn mkakati huu wakiovu dhidi ya haki za raia
CDM itoke na plan 'B' in case ugaidi huo umehararishwa: mikutano (ambayo kwa tafsri wao wataiona kama maandamano maana maelfu yanatembea kwenda na kutoka mikutano hiyo), vipeperushi vya elimu ya uraia-vinaweza kusambazwa na elikopita, magari nchi nzima,
Kwakuwa ccm na vyombo vyake wanaonekana tayari kutumia ngvu za dola- hali hii iendelee kuelezwa kwa msisitizo sana kwa watanzania kuonesha ccm ubaya wao ktk kuivuruga amani ya tzn
Kwakuwa cdm haina jeshi wala vifaa vya kijeshi bali nguvu yake ni watu ( tena waliomasikini) basi chama hicho kiakikikishe watu wanajiandikisha na kuwatayari kupiga kura kwa wingi wao ilikuiondoa madarakani ccm 2015. Hapa napo najua kutakuwa na vikwazo vingi-ikiwa ni serikali kujivuta ktik kuandikisha kuboresha dafutari la wapiga kura. Kinachowezakufanyika hapa ni cdm pia kuikumbudha serikali kutimiza wajibu wake...kelele hizi ziende sambamba na kuonesha jamii ya kimataifa-wakiwemo nchi jirani juu ya ujuma hizi dhidi ya raia.
Msimamo wangu mara zote umekuwa: kama mtu hawezi na hataki, kwa makudi tu kuukubali ukweli unaoonekana machoni pa wengi (ndani na nje ya nchi) basi nguvu itumike kumfanya akubaliane na ukweli huo kwa faida ya wengi.