Muswada wa kuzuia Maandamano nchini waja...

Muswada wa kuzuia Maandamano nchini waja...

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Katika hali ya kusikitisha na kushtusha Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi ameliambia bunge jioni hii kwamba serikali ya CCM imeridhia kuleta mswada bungeni ili itungwe sheria ya kuzuia maandamano kote nchini.

Nchimbi amesema hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoa uvunjifu wa amani nchini unaofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa.Waziri amesema mswada huo utaletwa wakati wowote kuanzia sasa akimaanisha tayari umeshakamilika.Nchimbi alikuwa akishangiliwa sana na wabunge wa CCM wakati alipokuwa akitamka maneno hayo.

Hili litakuwa ni pigo kubwa kwa demokrasia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Ikumbukwe ni hapo jana tu CHADEMA kilidai kunasa mpango wa siri wa serikali ya CCM wa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ili kukidhibiti CHADEMA na kukiimarisha CCM.
 
Huyu Nchimbi naonaga kichwa yake haina wazo la kufikiri chochote zaidi ya ujinga wa maneno isiyo na tija anayoropoka tu!
Anatumia masaburi yake kuwaza na kutoa kauli jinga kama hiyo!
 
Huo utakuwa mwisho wa CDM kisiasa waliozoea kuendesha harakati za kisiasa kupitia maandamano yanayoharisha ustawi wa nchi yetu. Tena ikibidi zoezi hili lianzie Arusha Mjini
 
Nchimbi angalia, haya unayoyasema CCM italilia sana nafasi ya kuruhusiwa kuandamana bila kukabwa na polisi pindi mtakapokua mmeshavushwa na sisi wapiga kura kuwa chama cha upinzani.

Usidiriki kutunga sheria kwa 'AKINA WALE' maana msemeno huo huenda ukawakateni huko baadaye.
 
Katika hali ya kusikitisha na kushtusha Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi ameliambia bunge jioni hii kwamba serikali ya CCM imeridhia kuleta mswada bungeni ili itungwe sheria ya kuzuia maandamano kote nchini.

Nchimbi amesema hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoa uvunjifu wa amani nchini unaofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa.Waziri amesema mswada huo utaletwa wakati wowote kuanzia sasa akimaanisha tayari umeshakamilika.

Hili litakuwa ni pigo kubwa kwa demokrasia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Ikumbukwe ni hapo jana tu Chadema kilidai kunasa mpango wa siri wa serikali ya CCM wa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ili kukidhibiti Chadema na kukiimarisha CCM.

Halafu anataka uraisi?
 
Ni jambo la ajabu mtu mzima unaandika kwamba kufuta maandamano ni mwisho wa CDM ni akili za kipumbavu kwani maandamano ni haki ya kikatiba ya raia yeyote kudai haki yake anapoona kwamba hatendewi hiyo haki yake kwa wakati,
Ni wapumbavu kama wakina @Mafilil hivi nyie mtakuwa chama tawala milele? je siku mtakapokuwa chama cha upinzani mtadai hiyo haki ya kuandamana?

Angalieni mpumbavu mmoja kama nyie na chama chenu cha Maccm akiwa madarakani alitunga sheria za kijinga kama mnazozingangania saa hivi ni Rais wa Zambia kwa kuona anawakomoa wapinzani lakini sheria hizo zilikuja kumgeuka akaanza kulia nyie furahieni tu zitawageuka na wala msitegemee kwamba mtatawala milele Watu wamewachoka hamfai na hamuwezi kutawala mmekalia kugawa watu kwa misingi ya ukabila na udini ili muwatawale vizuri na saa hivi kikanda na

CDM mmekuwa mnatumia maandamano kuwa ni chanzo cha kuvunja AMANI na UTULIVU nchini. Siasa za majukwaani bila fujo hamziwezi hivyo bila maandamano CDM katika jeneza
 
hiyo itaishia mdomoni hawezi kutunga sheria inayopingana na katiba,
 
Huo utakuwa mwisho wa CDM kisiasa waliozoea kuendesha harakati za kisiasa kupitia maandamano yanayoharisha ustawi wa nchi yetu. Tena ikibidi zoezi hili lianzie Arusha Mjini


  1. Kama hujui tatizo siyo chadema kama wao wanyofikiri. Tatizo ni matendo ya CCM kwa watanzania
  2. Kama ni elimu ya uraia Chadema wameshafanya kazi yao na wantanzania wa leo wameshakuwa welevu vya kutosha labda tu hao wenye wanaishi kwa mgongo wa dhulma za CCM
  3. Jingine serikali inajua fika kuwa hali kwa sasa si shwari (WaTZ wameshaikinai serikali hii) na wakiacha mambo yajiendeshe yenyewe kuna uwezekano mtu akatolewa magogoni bila kutarajia.
  4. Hata rafu za kuwatishia na kuwanyazisha wanasiasa, wanaharakati, waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari ni kwasababu wanajua wasipofanya hivyo hawatasalimika
  5. Hakuna kitu kigumu duniani kama kupingana na ukweli/Hali halisi.
 
  • Thanks
Reactions: mob
Muswada huo wa kipuuzi unaopingana na katiba ya taifa letu, ukiletwa bungeni nawaomba wabunge wote wanaolipenda taifa letu wasusie bunge siku hiyo, ili wahuni wabaki bungeni ili wapitishe sheria ya kishenzi. Watanzania tusikubali ujinga huo wa maccm!
 
Mswada huu ni batili tayari kwa kuwa inapingana na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na UN Human Rights Charter.

Miongozo hiyo miwili zote zinaasisi na kutetea kwa kinywa kipana HAKI NA UHURU WA

(1) raia kujumuika pamoja kuzungumzia yale yanayowahusu;

(2) raia wanazo haki za kukusanyika pamoja na kutumia fursa ya kuelezea kutokuridhishwa kwao na jambo lolote na kuhitajika kupewa ulinzi pindi wanapofanya hivyo.

NB: Hadi leo hii wala sijasikia popote kama taifa letu limejiondoa kufuata sheria na mikataba ya kimataifa ambayo tulitilia sahihi kwa hiari yetu wenyewe.
 
Wamechelewa sasa hivi wanachopigania kukizuia ni stage ambayo chadema wamekwishavuka, watashangaa harakati zinavyoendeshwa, hawa jamaa wanatembea mahali ambapo chadema wametoka!
 
Huo muswada ukipitishwa ukawa sheria sijui viongozi wa CHADEMA watakula wapi!

Tatizo mna amini kwamba CCM ndio mwisho wa yote Tanzania. Mnasahau kwamba CCM imekuwa kipofu waku toona kwamba itatokea siku moja itaanguka. Hala hala msikate tawi mlilo likalia!

CCM hata ifanye nini, mabadiliko hayazuiliki tena. Tumefikia kwenye "due point", lazima inyeshe hata likiwaka jua. CCM wana paswa kuwa na maono kwamba wakati huu wa kuelekea 2015, kila sheria gandamizi wanayo taka kuianzisha itakula kwao na itakuwa ndio mwisho wa CCM.

Wamejifungia kwenye handaki. MAGAMBA wanaona wao ndio wenye nchi na hawaoni waTanzania wamezichoka siasa za viongozi kujiangalia wenyewe.

UPEPO HAUZUILIWI KWA MIKONO.
 
Ni jambo la ajabu mtu mzima
unaandika kwamba kufuta maandamano ni mwisho wa CDM ni akili za
kipumbavu kwani maandamano ni haki ya kikatiba ya raia yeyote kudai haki
yake anapoona kwamba hatendewi hiyo haki yake kwa wakati,
Ni wapumbavu kama wakina @Mafilil hivi nyie mtakuwa chama tawala
milele? je siku mtakapokuwa chama cha upinzani mtadai hiyo haki ya
kuandamana?

Angalieni mpumbavu mmoja kama nyie na chama chenu cha Maccm akiwa
madarakani alitunga sheria za kijinga kama mnazozingangania saa hivi ni
Rais wa Zambia kwa kuona anawakomoa wapinzani lakini sheria hizo
zilikuja kumgeuka akaanza kulia nyie furahieni tu zitawageuka na wala
msitegemee kwamba mtatawala milele Watu wamewachoka hamfai na hamuwezi
kutawala mmekalia kugawa watu kwa misingi ya ukabila na udini ili
muwatawale vizuri na saa hivi kikanda na

siku zote wanaolilia maandamano uwezo wao wa kufikiri ni mdogo. viongozi wa chadema ni mfano wa hao. viva waziri nchimbi
 
Katika hali ya kusikitisha na kushtusha Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi ameliambia bunge jioni hii kwamba serikali ya CCM imeridhia kuleta mswada bungeni ili itungwe sheria ya kuzuia maandamano kote nchini.

Nchimbi amesema hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoa uvunjifu wa amani nchini unaofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa.Waziri amesema mswada huo utaletwa wakati wowote kuanzia sasa akimaanisha tayari umeshakamilika.

Hili litakuwa ni pigo kubwa kwa demokrasia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Ikumbukwe ni hapo jana tu Chadema kilidai kunasa mpango wa siri wa serikali ya CCM wa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ili kukidhibiti Chadema na kukiimarisha CCM.

Usipate shida, Nchimbi hanamamlaka ya kubadilisha katiba, hata hilo bunge lililopo halina hiyo mamlaka! Hiyo ni haki ya kikatiba, waliolewa madaraka wanatumia matumbo kufikiri badala ya ubongo!!
 
Huo muswada ukipitishwa ukawa sheria sijui viongozi wa CHADEMA watakula wapi!

Na ikitokea CCM ikashindwa uchaguzi then chama kingine kikachukua madaraka hiyo sheria ikaendelea kuwepo. Kilio chao watawasilisha vipi ikitokea wamenyanyaswa , hivi sheria zinatungwa kudhibiti mahaba ya kichama.

Hivi kabisa tumekosa vision au ni mbwembwe tuu ionekane umethibiti upande fulani ilihali hiyo sheria itakuja kukugeukia siku moja . Mfano kuna sheria ya kudhibiti ugaidi duniani,je ugaidi umedhibitiwa na hizo sheria?. Kuna sheria ya kunyonga wauaji je mauaji hayapo ?

Think twice mkubwa USITAFUTE MUWEKEZAJI HADI KWENYE KICHWA CHAKO .
 
Hivi bado hawajapitisha huo muswada?
Wapitishe hata ule wa wananchi kutokupiga kura ktk kumchagua Rais na wabunge & Co.
 
Vyombo vya habari .e.g Habari Leo wameeleza kuwa watuhumiwa wa tukio la Arusha wako 6 wakiwemo Wasaudia wawili. Kwa maelezo ya gazeti, Wasaudia waliingia nchini Jumamosi kupitia uwanja wa ndege KIA na baada ya tukio walikimbilia Kenya kwa kutumia usafiri wa barabara.

Kwa maana hiyo basi, watuhumiwa wa mkasa huu mkubwa na wenye kutia doa sifa ya Tanzania, hawakuwa kwenye maandamo! Vivyo hivyo, muuaji wa Padri Mushi kule Zanzibar au mtu aliyemwagia tikikali Sheikh Soraga huko Zanzibar hakuwa kwenye maandamo! Wahanga wa meno na kucha hawakuwa kwenye maandamano.Wabeba twiga hawakuwa kwenye maandamano!

Na ukitazama kwa makini matukio yote makubwa hayana uhusiano na maandamano. Nchimbi anaelewa tatizo linaloikabili taifa hili? Na kama hajaelewa kwanini asichukuwe siku walau kidogo ili akisimama mbele ya bunge atoe kauli zenye matumaini?

Watu wakiandamana maana yake kuna tatizo, na hivyo wanapaza sauti kwa mtindo ambao wanaona ndio utawafanywa walengwa kusikiliza kero zao. Kwanini Nchimbi asitafute suluhu ya kero za wananchi halafu aone kama wataandamana? Ukisilikiza hoja za wabunge (baada ya taaraba zao) kila mmoja ana kero za wapiga kura wake, mwaka hadi mwaka, maji, huduma za afya, usalama hafifu, ardhi, huduma za afya, barabara mbovu, ubadhirifu kwenye Halmshauri, matokeo mabaya n.k. Hivi majibu ya haya yote kuzuia maandamano?

Mimi ningempa Nchimbi ushauri tofauti, hebu siku moja akisikia kuna maandamano, aembe kuwa kushiriki kwa maana ya kuyapokea hayo maandamo na kusikiliza wanataka nini? Hili tu! Hii nguvu kubwa inayotumika kuleta sheria inazidi kuiweka serikali na hasa CCM mbali na wananchi, Gharama yake ni kubwa kwa CCM. Pokea maandamano na sikiliza hoja. Huo ndio uongozi bora na wa kimekrasia!
 
Back
Top Bottom