Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,720
- 218,268
Dkt Emmanuel Nchimbi ameteuliwa na chama chake kuwa Katibu Mkuu , kwa kadiri ya kumbukumbu zetu , kwa mtu yeyote kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM ni jambo kubwa linalopaswa kuzagaa midomoni mwa wananchi na vyombo vya Habari , hii ni kwa sababu Chama hicho ni kikongwe mno , ikizingatiwa pia kwamba nafasi hiyo wamepita watu wengi maarufu , wakiwemo Philipo Mangula , Yusufu Makamba , Kinana na wengineo , Hivyo tulitarajia kishindo kikuu kwa uteuzi wa Nchimbi .
Lakini kwa Bahati mbaya sana, uteuzi huu wa Nchimbi umekuja katika kipindi kibaya , kipindi ambacho Mwamba wa siasa za Nchi Freeman Mbowe , ametangaza Maandamano ya kupinga miswada mibovu ya sheria za uchaguzi yaliyopangwa kufanyika 24/01/2024 , Tangazo hili la Mbowe limepokelewa kwa kishindo kikuu na wananchi , ambao wameahidi kuunga mkono na kushiriki Maandamano hayo ya Amani .
Kwa kifupi ni kwamba Taarifa za uteuzi wa Nchimbi zimezimwa na Taarifa ya maandamano ya Chadema , Yaani ni kwamba wananchi wanaona kuwa Maandamano ya kupinga miswada mibovu ya sheria za uchaguzi ni Jambo kubwa na muhimu zaidi kuliko Uteuzi wa Nchimbi, yaani Uteuzi wa Nchimbi umepuuzwa na Wananchi kwa vile wanaona kuna jambo kubwa zaidi kuliko uteuzi wake, kisiasa na hasa kwa Nchi kama Tanzania hii ni Progress