Musukuma: Profesa Sospeter Muhongo usomi wake hauna faida kwa Tanzania

Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma amemshukia mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo kwamba usomi wake hauna faida kwa Tanzania. Musukuma amesema ni wakati kwa Serikali kuwaamini wasomi aliowaita wa darasa la saba akidai kuwa wanakulia kwenye kazi.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma leo jioni Jumanne Aprili 13, 2021 katika mjadala wa mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu mwaka 2021/22.

Amebainisha kuwa ni wakati wa Serikali kuwaamini watu wenye elimu ya darasa la saba badala ya kung'ang'ania maprofesa wasiokuwa na maana ambao wakati wote wanasubiri wengine waanzishe halafu wao wabebee ajenda juu kwa juu.

Amemtaja Profesa Muhongo kwamba wakati akiwa waziri wa nishati na madini alishindwa kufanya mambo mazuri lakini anashangaa kuona ameanza kuwa mkosoaji mkubwa.

"Mwaka 2016 nilimuita Profesa Muhongo nikamwambia kwenye haya makinikia tunaibiwa lakini alichukua kipaza sauti akatangaza hadharani kwamba Geita wamechagua mtu wa darasa la saba wamekosea sana," amesema Msukuma.

Amesema baada ya hapo walichukua mchanga wakaenda nao mbele ya rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli na ilibainika kuwa mchanga huo ulikuwa na madini ya thamani kubwa.

Aprili 9, 2021 bungeni mjini Dodoma, Profesa Muhongo alisema uchumi wa gesi pekee ndiyo utakaoifikisha Tanzania kwenye uchumi thabiti na kukosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.

Amesema Tanzania inatakiwa ijikite katika matumizi ya umeme mchanganyiko badala ya kutegemea mabwawa ya maji ambayo wakati wowote yanaweza kukauka.


Mwananchi
tatizo la 7 wanatumia nguvu maprof.wanatumia akili,na mama kasema awamu hii tumieni akili kuliko nguvu
 
Tukubaliane kimsingi mbunge aliyeishia darasa la saba hawezi akajilinganisha na hata mtu aliyeishia form 4 katika uwanja mpana wa kupambanua mambo. Geita wamekula hasara
Msukuma ni la saba ila ana utajiri ambao ukoo wako wote hawawezi kuwa nao pamoja na kumaliza kwao form 4
 
kwenye pointi ya " LA saba wamekulia kwenye kazi" nimemuelewa... ifike mahala tuwajaribu na hawa watu kuliko hao wanaojiita maprofesa...
Huu sasa ndio ujinga wa mtanzania. Mtu wa darasa la saba kweli anakuwa miongoni mwa watunga sheria!
 
Msukuma na wewe ni mganga njaa tu, kama kweli unajua biashara mbona umeishia kununua na kuuza Mbuzi huko huko kwenu? kawekeze Dubai, Ulaya na Marekani basi tukuone !! acha kudharau Elimu za watu - wamezisotea - unafikiri kusoma ni kazi ndogo? mbona we ukaishia la Saba wakati ngombe mlikuwa nazo nyumbani msiuze uendelee na masomo.
Inaonekana huwa unamsikia msukuma kupitia account twitter za lisu na kigogo tu!

Nenda geita ndio utamjua msukuma ni nani
 
Msukuma ana vision kubwa kuliko Muhongo na Muhongo ajiamini kabisa anamaanisha nini maana haeleweki kwa sababu ya kufata upepo...
 
Hii chuki ya waziwazi ya watu ambao hawajasoma sana (wao wanajiita darasa la saba LY) kwa wale wanaoitwa wasomi (nadhani wengi kuanzia degree) mbona kama inazidi kukua kwa kasi sana tatizo nini hasa?! Kwanini kila mmoja asi'appreciate mchango wa mwenzake kwenye maendeleo ya nchi yetu?! Nadhani kila mmoja ana umuhimu wake kwa wakati wake
 
Niliwahi kumtembelea ndugu yangu pale Udom kwenye mabweni yao nikabahatika kuingia chooni,nilistaajabu kukuta kuta za choo zimepigwa Machata kwa kutumia kinyesi nilijiuliza sana juu ya hawa wasomi wetu kwa akiongeacho msukuma nakubaliana nae huenda hata Huyo Prof. Ni jamii ya hawa wachora kuta na kinyesi vyooni, kifupi si kila asomae sana basi jamii au familia yake itanufaika nae.
We binadamu wewe?? Daah!!

Nimecheka saana aisee!!!
 
Ukweli Spika ama anajua anachokifanya au anavuta muda wake nae ufike apumzike tu. Inawezekanaje anaachia hoja mfu zisizo na faida kwa taifa ziendelee kujadiliwa ni sawa na kunajisi jengo letu la kutunga sheria. Kumsikiliza MPush na Lusinde lazima upate zao la Babu Tale na wenzake.
 
kwenye pointi ya " LA saba wamekulia kwenye kazi" nimemuelewa... ifike mahala tuwajaribu na hawa watu kuliko hao wanaojiita maprofesa...
Unataka tuweke maisha yetu rehani kwa hawa waliosoma shule za kayumba wakina Kibajaj? Haiwezekani hao kazi yao ni moja kutumika kama vipaza sauti vya propaganda za ccm!
 
Kwa sasa hakuna yoyote wa maana bungeni wote ni haramu tu,, walipita kwa njia isiyo halali,hata bungeni wataongea pumba,,
Mm mwenyewe mwanaCCM
 
Eti hawezi kulinganisha na mtu wa form 4!! Ni ujinga mtupu!

Musukuma ni darasa la saba lakini ni milionea na ana kampuni la mabasi na biashara nyinginezo na amevipata kabla hata ya kuwa Mbunge sasa kimtazamo tu hiyo ni akili na uwezo wa kupambanua mambo katk kujikwamua.

Haya wewe tuambie nadhani pia wewe ni msomi ongeza na wasomi wenzio uliosoma nao vipi unamfikia hata nusu ya utajiri alionao Musukuma?
Kumiliki mabasi unaita utajiri?
Nioneshe kampuni ya mabasi iliyodumu miaka 40 ukiondoa Simba mtoto ya TANGA
 
Elimu inaongeza haipunguzi...., Hata huyo wa la saba akipata elimu zaidi (elimu sio vyeti) atakuwa bora zaidi na huyo Proffesor bila hio elimu angekuwa bogus zaidi...

Kwenye kuwakilisha / kutoa msaada kwa jamii hakuitaji kisomo, kisomo ni added value (pia kuelewa matatizo yao hao unaowasaidia yahitaji uelewa) ambayo nayo pia ni elimu
 
Msukuma hajui kama Prof Muhongo ndio aliongoza jopo la wajumbe walikwenda uganda kupora project ya EACOP ? sasa mchango upi tena anaousemma yeye
 
Niliwahi kumtembelea ndugu yangu pale Udom kwenye mabweni yao nikabahatika kuingia chooni,nilistaajabu kukuta kuta za choo zimepigwa Machata kwa kutumia kinyesi nilijiuliza sana juu ya hawa wasomi wetu kwa akiongeacho msukuma nakubaliana nae huenda hata Huyo Prof. Ni jamii ya hawa wachora kuta na kinyesi vyooni, kifupi si kila asomae sana basi jamii au familia yake itanufaika nae.
Elimu ya mtu haiondoi upumbafu wake.
 
Tukubaliane kimsingi mbunge aliyeishia darasa la saba hawezi akajilinganisha na hata mtu aliyeishia form 4 katika uwanja mpana wa kupambanua mambo. Geita wamekula hasara
Kwani Bwasheeeee Msukuma anaofauti na Professor Muhongo binadamu wote ni sawa
 
Back
Top Bottom