Musukuma: Profesa Sospeter Muhongo usomi wake hauna faida kwa Tanzania

.....Binafsi nafikiri Msukuma ana hoja apo sikubalinai nae katika kudharau wasomi...Prof Muhongo alikuwa waziri wa Nishati na madini wakati huu mchakato wa kuanzisha mradi wa umeme kwa kutumia maji ukiwa umeshika kasi...kwa nafasi yake yeye alikuwa mshauri mkuu wa Rais..si angemshauri hili la nishati ya gesi na udhaifu wa kutumia umeme wa maji? Kwa nini leo?
 
huwa unawaza
Ndugu wa-Tanzania, ifike wakati tuvitumie viungo vyetu tulivyopewa naMwenyezi Mungu kwa kazi iliyokusudiwa, mathalan tutumie bongo zetu kufikiri na midomo kutamamka yale yaliyo kwishafanyiwa kazi na bongo zetu. Prof. Sospita nimemsikiliza kwa makini sana, ametoa ushauri mzuri tu. Sasa anatokeza mtu ametokea alikotokea anatumia mdomo kufikiri badala ubongo wake. Musukuma na Lusinde, msidhani wa-Tanzania ni wapumbavu sana wa kusikiliza porojo zenu. Ni vyema mara nyingi kukaa kimya endapo huna uwezo wa kuchangia hoja kubwa za kisayansi
kwa kutumia makalia au? unajua huyo muhongo ndo mnufaikaji wa richmond...kwahiyo kwa akili zako unaamini ethipopia hawakuona huo umeme wa gas hadi wakawekeza kwenye maji...unajua hiyo ges inakaa mda gani hadi kuisha..je una mtambo wowote wa kuzalisha umeme wa gas au mnajisahaulisha kua hadi leo gharama kubwa za tanesco zinasababishwa na mitambo ya dowans...watanzania sijui hua tunafikiria kwa kutumia nn
 
Amebainisha kuwa ni wakati wa Serikali kuwaamini watu wenye elimu ya darasa la saba badala ya kung'ang'ania maprofesa wasiokuwa na maana ambao wakati wote wanasubiri wengine waanzishe halafu wao wabebee ajenda juu kwa juu...
Bravo Msukuma

Hapa umeonyesha ujasiri naamini waweza kuangusha mbuyu kwa kisu
 
Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma amemshukia mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo kwamba usomi wake hauna faida kwa Tanzania. Musukuma amesema ni wakati kwa Serikali kuwaamini wasomi aliowaita wa darasa la saba akidai kuwa wanakulia kwenye kazi.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma leo jioni Jumanne Aprili 13, 2021 katika mjadala wa mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu mwaka 2021/22.

Amebainisha kuwa ni wakati wa Serikali kuwaamini watu wenye elimu ya darasa la saba badala ya kung'ang'ania maprofesa wasiokuwa na maana ambao wakati wote wanasubiri wengine waanzishe halafu wao wabebee ajenda juu kwa juu.

Amemtaja Profesa Muhongo kwamba wakati akiwa waziri wa nishati na madini alishindwa kufanya mambo mazuri lakini anashangaa kuona ameanza kuwa mkosoaji mkubwa.

"Mwaka 2016 nilimuita Profesa Muhongo nikamwambia kwenye haya makinikia tunaibiwa lakini alichukua kipaza sauti akatangaza hadharani kwamba Geita wamechagua mtu wa darasa la saba wamekosea sana," amesema Msukuma.

Amesema baada ya hapo walichukua mchanga wakaenda nao mbele ya rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli na ilibainika kuwa mchanga huo ulikuwa na madini ya thamani kubwa.

Aprili 9, 2021 bungeni mjini Dodoma, Profesa Muhongo alisema uchumi wa gesi pekee ndiyo utakaoifikisha Tanzania kwenye uchumi thabiti na kukosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.

Amesema Tanzania inatakiwa ijikite katika matumizi ya umeme mchanganyiko badala ya kutegemea mabwawa ya maji ambayo wakati wowote yanaweza kukauka.


Mwananchi
Halafu tunalaumu MABEBERU kuwa wanatuchelewesha maendeleo wakati ni sisi wenyewe tunajichelewesha. CCM Ina entertain kuwa na sampuli za akina Lusinde, Deo Sanga na Msukuma ili wawe akina NDIYO bwana kwenye maamuzi nyeti.

Kweli nchi yenye vyuo vikuu zaidi ya 20 na annual graduates zaidi ya 30,000 bado tunaruhusu Std 7 aingie Bungeni?? We are not seeious
 
Ndugu wa-Tanzania, ifike wakati tuvitumie viungo vyetu tulivyopewa naMwenyezi Mungu kwa kazi iliyokusudiwa, mathalan tutumie bongo zetu kufikiri na midomo kutamamka yale yaliyo kwishafanyiwa kazi na bongo zetu.

Prof. Sospita nimemsikiliza kwa makini sana, ametoa ushauri mzuri tu. Sasa anatokeza mtu ametokea alikotokea anatumia mdomo kufikiri badala ubongo wake. Musukuma na Lusinde, msidhani wa-Tanzania ni wapumbavu sana wa kusikiliza porojo zenu.

Ni vyema mara nyingi kukaa kimya endapo huna uwezo wa kuchangia hoja kubwa za kisayansi
Tatizo ni ndungai anayewapa airtime ya kutukana watu
 
Eti hawezi kulinganisha na mtu wa form 4!! Ni ujinga mtupu!

Musukuma ni darasa la saba lakini ni milionea na ana kampuni la mabasi na biashara nyinginezo na amevipata kabla hata ya kuwa Mbunge sasa kimtazamo tu hiyo ni akili na uwezo wa kupambanua mambo katk kujikwamua.

Haya wewe tuambie nadhani pia wewe ni msomi ongeza na wasomi wenzio uliosoma nao vipi unamfikia hata nusu ya utajiri alionao Musukuma?
Yeye pamoja na wenzie wamejipumzikia kusubiria Ajira serikarini na hata walichosomea hakiwezi kuwasaidia kujikwamua
 
Niliwahi kumtembelea ndugu yangu pale Udom kwenye mabweni yao nikabahatika kuingia chooni,nilistaajabu kukuta kuta za choo zimepigwa Machata kwa kutumia kinyesi nilijiuliza sana juu ya hawa wasomi wetu kwa akiongeacho msukuma nakubaliana nae huenda hata Huyo Prof. Ni jamii ya hawa wachora kuta na kinyesi vyooni, kifupi si kila asomae sana basi jamii au familia yake itanufaika nae.
chata tu ndio zikakufanya uzarau wasomi mkuu au kuna lingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waendelee tu kuparuana. Kwanza CCM wote hawana faida yoyote ile kwa nchi, zaidi tu ya kuifilisi.
Wanamalizana Wenyewe
Wengine Tutazame Tu Mpaka Wauwane Tukawazike
😀😁😃😄😃😂😅😆😅😄😂😁
 
Sheik Amri Abeid Karume alishawahi Kusema Sisi hatujasoma lakini Tumeelimika... Muhongo Kasoma lakini hajaelimika na ndio wasomi wengi wanaotuongoza serikalini... Huyo Msukuma ni Tajiri sana kwa biashara zake halali lakini Muhongo hatokuja kumfikia labda kama aliiba sana enzi za Jakaya kaficha pesa... na si vinginevyo... Wasomi wengi ni uchwara... Huko Mbele ukisikia Profesa basi kuna vitu alishaanzisha na vinasaidia Dunia Muhongo ni Dalali tu anyamaze tushaambiwa na Kibajaji ccm wengi walikuwa hawachaguliki ndio ukweli tunatao amini Nileteeni Gwajima
 
Msukuma na wewe ni mganga njaa tu, kama kweli unajua biashara mbona umeishia kununua na kuuza Mbuzi huko huko kwenu? kawekeze Dubai, Ulaya na Marekani basi tukuone !! acha kudharau Elimu za watu - wamezisotea - unafikiri kusoma ni kazi ndogo? mbona we ukaishia la Saba wakati ngombe mlikuwa nazo nyumbani msiuze uendelee na masomo.
 
Amesema baada ya hapo walichukua mchanga wakaenda nao mbele ya rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli na ilibainika kuwa mchanga huo ulikuwa na madini ya thamani kubwa.
Hela ya hayo makontena ya makinikia yaliyoshikiliwa ushaiona? thamani kubwa ipi ndugu Msukuma wakati makontena hadi wa leo hayajulikani yalipo.
 
Back
Top Bottom