Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,897
- 941
LEO BUNGENI: MAPENDEKEZO YA MPANGO WA TAIFA KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 - Mchango wa Prof Muhongo
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ameshauri yafuatayo:
*Mipango yetu ya maendeleo ilenge kupunguza umaskini kwa kasi kubwa
*Uwekezaji wetu ulenge kupunguza umaskini kwa kasi kubwa
*Uchumi wetu ukue kwa kasi ya asilimia 8-10 (8-10%) ili kupunguza umaskini kwa kasi kubwa
*Mipango na Bajeti zake vishughulikie mahitaji muhimu ya kila siku ya Wa-Tanzania, k.m. chakula, maji, umeme na matibabu.
*Vipimo vya upatikaji wa huduma muhimu kwa vile maji na umeme, viweke maanani matumizi halisi ya mtu mmoja mmoja kwa mwaka
Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO kutoka Bungeni - imeambatanishwa hapa.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Alhamisi, 9.11.2023