Bunge la 12: Wabunge wamchangia fedha Profesa Jay kumpa pole na kusapoti Taasisi yake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 13, Kikao cha 9, leo Novemba 9, 2023.



Wabunge wamchangia fedha Profesa Jay
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekubaliana kumchangia fedha Mbunge wa zamani wa Mikumi na Msanii wa Bongo Fleva, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ kwa ajili ya kumuunga mkono katika Taasisi yake ya Profesa Jay Foundation na kumpa pole kutokana na kuugua kwa muda mrefu.

Hoja hiyo kuhusu Haule aliyefika Bungeni akiwa mmoja wa wageni waalikwa Jijini Dodoma, leo November 9 2023, ilitolewa na Mbunge Aida Khenani, ikaungwa mkono na Joseph Musukuma kisha Wabunge wengine nao wakaunga mkono.


Musukuma: Huu mwaka wa mwisho kutudanganya, Waziri ukija na swaga tutazinguana
Akizungumzia kuhusu maboresho ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Musukuma amesema “Licha ya kuwa ni uwanja wa pili kuingiza mapato mengi Nchini lakini bado kuna kigugumizi cha maboresho ya kuufanya kuwa Uwanja wa Kimataifa, bajeti ijayo ije na hela ya maboresho ya uwanja huo.”

 
Mbunge wa Nkasi Aida Kenani aliomba mwongozo wa Spika kama Wabunge wanaweza kuchangia Prof Jay ambapo kila Mbunge atoe tsh 50,000.

Naye Dr Msukuma wa Geita vijijini akapendekeza kila Mbunge achangie tsh 200,000 ambapo tsh 100,000 apewe Prof Jay mwenyewe na tsh 100,000 iingizwe kwenye Foundation yake.

Spika Dr Tulia PhD amekubali na kusema lila Mbunge achangie kiasi atakachoweza na amewaagiza Wahudumu wa bunge kukusanya michango Hiyo Leo na Kesho.

Mungu wa mbinguni mfanyie Wepesi Prof Jay

Source: Ayo TV
 
Waje na huku wawachangie watoto wa wanyonge walionyimwa mikopo ya kusoma vyuo vikuu.
 
Back
Top Bottom