MUONGOZO: Mambo ya kuzingatia unaponunua gari lililotumika ndani ya Tanzania

BREVIS imetulia sana barabarani kwa safari ndefu hasa ukiwa una mwendo (zaidi ya 100 kph, tatizo tochi/faini) pia zinabugia mafuta mithili ya PRADO. Xtrail jiandae kwa kukusanya namba za mafundi magari angalau 10.

Ko X trail ni kimeo yaani
 
Ko X trail ni kimeo yaani
Mimi mtu akiniambia xtrail ni kimeo sikubali. yupo mtu ninayemfahamu anaitumia huu mwaka wa nne na route zake ni arusha tanga. ukweli watu hatujui kuzitunza. rejeta wanatia maji, oil siyo iliyokuwa prescribed na manufacturer lazima ife.
 
Mimi mtu akiniambia xtrail ni kimeo sikubali. yupo mtu ninayemfahamu anaitumia huu mwaka wa nne na route zake ni arusha tanga. ukweli watu hatujui kuzitunza. rejeta wanatia maji, oil siyo iliyokuwa prescribed na manufacturer lazima ife.
Xtrail vs RAV 4 je?
 
wabongo hawajui magari. Wengi wananunua kisa eti plate number. Hawaangali mileage ya gari,ubora hapana ilimradi inaonekana vizuri nje.

hawa madalali ni kuwapiga marufuku.
 
Sorry kama nitakuwa nje ya mada, endapo nikiwa na 4M ninaweza kuagiza Vitz Japan? Au itabidi ninunue tu used za hapa TZ?
 
Ni bora nitoboke mfuko ila mimi huwa sipendi vitu used... huwa napenda sana kumenya karatasi ya vitu vipya tu... usafiri wangu ni daladala ila gari yangu ya kwanza lazima ni zame showroom ni menye mwenyewe....

Yote kwa yote pongezi kwa kutujuza! Safi
 
Aisee asante sana kwa ushauri wako muruwa yaani huwezi amini wiki hii yote natafuta gari lakini kwa style niliyoiona ya madalali ni usanii mtupu,huu uzi wako ni kama umeniona mimi jinsi ninavyotafuta gari bila mafanikio

Mungu akubariki
 
Mkuu RRONDO Mungu akubariki sana kwa huu Uzi, mi natafuta Harrier old model, vipi unanishauri nini na labda bei zake kwa hapa TZ inaendaje? Thanks in advance
 
Naomba nifahamishe kuhusu Toyota Alphard 2400cc ulaji mafuta kwa long Safari na mizunguko ya mjini. Weakness zake na ubora wake.
 
Kwa kuwa inaonekana wabongo wengi wanapotaka kununua magari yalotumika ndani ya bongo kitu kikubwa wanachoangalia ni mileage ambayo gari imetembea basi nawaasa ndugu zanguni kuweni makini sana,kuna huu utapeli wa kurudisha km za maga, na wengi hurudisha nyuma chini ya km laki moja na nusu au chini ya laki moja!Cha kufanya: Zingatia zaidi uzima wa injini kwa kuwa gari ni injini asikudanganye mtu,ukitaka kununua tafuta mtu mwenye weledi wa magari akukagulie gari,kuna gari zimetembea km nyingi lkn ziko well maintained na kuna gari zina km ndogo lkn vimeo!Pia km gari unalotaka kununua huyo mmiliki aliliagiza mwenyewe toka nje,mwambie akuoneshe inspection document zilizokuja na gari huwa zinaonesha gari imeingia ikiwa inasoma km kadhaa,hivyo km amebadilisha km utajua!Kila la kheri wanunuzi!
 
Unalolisema ni kweli kabisa. Wabongo sio waaminifu kabisa. Unakuta mtu anakwambia anauza gari yake, alilinua toka Japan likiwa used miaka zaidi ya mitano iliyopita, lakini leo anapotaka kuliuza anasema limetembea Km chini ya laki moja!!
 
Hebu nielekeze jinsi ya kuzipunguza.
 
Labda hzo odometer isiwe digital
Lakini kama ni digital hata ukirudusha nyuma ukitembea umbali flan zina retain kwenye original milage mkuu hapo ndo utamkamata mwizi wako.
Wazungu sio wajinga.
 
Labda hzo odometer isiwe digital
Lakini kama ni digital hata ukirudusha nyuma ukitembea umbali flan zina retain kwenye original milage mkuu hapo ndo utamkamata mwizi wako.
Wazungu sio wajinga.
Una amini katikati digital?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…