MUONGOZO: Mambo ya kuzingatia unaponunua gari lililotumika ndani ya Tanzania

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
51,719
107,770
1585381624980.png

Baada ya kusikia watu wengi 'wakiumizwa' na 'kupigwa' wakiwa kwenye harakati za kutafuta usafiri uliotumika nchini, nimeona sio mbaya nikitoa ushauri ni jinsi gani unaweza kuepuka majanga kwenye zoezi hilo.

Naandika kama mnunuzi au muuzaji wa aina hio ya magari, kwahio siegemei upande wowote na ninachokiandika hapa sio sheria naweza kuwa sahihi au nisiwe sahihi ila ni imani yangu lipo litakalosaidia baadhi ya watu.

Njia muhimu za kufuata ili kupata gari unalotaka ni kama ifuatavyo:

1. Fanya utafiti mdogo juu ya gari unalolitaka: Uliza ujue gari unalolitaka linauzwa kiasi gani[makadirio]. Ukiweza kujua bei ya showroom au ukiagiza mwenyewe Japan halafu linganisha na bei utakayopewa hapa. Hili ni muhimu kwa sababu nimeshuhudia watu wananunua magari yaliyotumika Tanzania kwa bei ambayo ukiagiza mwenyewe unalipata kutoka japan au ukiongeza kidogo tu unapata la showroom.

2. Usiwe na haraka: Usiwe na haraka kabisa kwenye kutafuta gari. Utaletewa kila aina ya gari na usipokuwa makini utanunua gari bovu. Angalia taratibu angalau magari matano tofauti kwenye chaguo lako ndipo uamue, madalali watakusumbua ili mradi tu wapate cha juu.

3. Epuka madalali: Kama unaweza epuka madalali. Tafuta gari kwa kuuliza watu ulio karibu nao, ndugu jamaa na marafiki au unaofanya nao kazi au biashara. Hii ni nzuri chochote kikitokea una pa kuanzia. Madalali wengi hawajali maslahi yako wala ya muuzaji cha muhimu kwao ni cha juu tu. Gari la 4m dalali atakuuzia 5-6m.

4. Tafuta Fundi: Ukilipenda gari lolote tafuta fundi akusaidie kulikagua, hata kama una ujuzi(idea) na magari kuna vitu hutaviona ila fundi atakusaidia. Kuwa makini kuna mafundi huwa wanabonyezwa wakufiche hitilafu halafu baadae wanarudi kupewa chao ukishauziwa kanyaboya.

5. Epuka gari lililopigwa rangi: Epuka gari iliopigwa rangi siku chache kabla ya kuwekwa sokoni, wazoefu wanajua gari za aina hio ndio umuhimu wa fundi unapokuja. Gari inaweza kuwa imegongwa hivyo imenyooshwa na wanakuzuga kwa rangi inayong'aa. Siku hizi rangi hata 200,000 unapiga gari nzima ila ukinunua hilo baada ya mwezi rangi inababuka yote.

6. Epuka gari lililooshwa engine: Ukikagua gari ukiona limeoshwa engine ogopa sana. Mara nyingi magari yanaoshwa engine kuficha 'leakage', yaani oil na vitu vingine vinavyovuja kutoka sehemu mbalimbali za engine.

7. Jaribu gari wewe mwenyewe: Ni muhimu kuendesha na kuijaribu gari wewe mwenyewe hata ukienda na fundi. Ipitishe njia mbovu usikie jinsi ilivyo chini, chochote kinachogonga kuwa makini, usisikilize ukiambiwa ni tatizo dogo, kwanini hakurekebisha. Ingawa yapo matatizo madogomadogo ila kuwa makini.

8. Usiangalie plate Namba: Usibabaishwe na namba, eti hii C, D etc. Kuna gari namba A ziko vizuri kuliko namba C. Muhimu ni hali ya gari husika kwa muda huo.

9. Nenda TRA kujiridhisha: Ni muhimu kujua ukweli na status ya gari na mwenye gari. Jiridhishe anaekuuzia ndio mwenye gari. Akuonyeshe nyaraka zote halisi hata za kodi aliolipia.

10. Mwisho kabisa ukilipenda gari fanyeni makabidhiano kwa kuandikishana kwa mwanasheria. Ukiweza lipia benki na ubaki na risiti kama ushahidi wa malipo kupitia akaunti yake. Epuka kubeba cash kumpelekea muuzaji mahali alipo.

Haya machache naamini yanaweza kuwa msaada kwa watu wanaonunua magari yaliyotumika nchini,wengine mnaweza kuongezea mawili matatu na kurekebisha nilipokosea.

BAADHI YA MICHANGO ILIYOTOLEWA NA WADAU WA JF
Uzi mzuri kaka.

Ila kuliko kusumbuka na kadhia zote hizo bora uagize la kwako toka japan moja kwa moja. Atleast kule una guarantee kuwa unapata kitu cha uhakika.

Pia umesahau swala la usafi, kuna magari ndani machafu kinoma, viti vinanuka utadhani walipanda mbuzi huko ndani.

Pia, angalia service history ya hilo gari na aina ya service inayofanywa kwenye hilo gari. Kuna magari yanaenda service yakiharibika tu na si wakati wowote. Kama gari lina service ya kila baada ya muda au kilometa litakuwa na uhakika wa kuwa zima pale unapotaka kulinunua.

Unaweza kuangalia hilo gari lilikuwa linatembelea barabara za aina gani, kuna wale watumiaji wa upanga posta au wao ni full lami mwanzo mwisho. Hawa magari yao yanakuwa nazima kidogo hasa kwenye pysical part ya nje kuliko yale ambayo mwanzo mwisho ni "all weather road"

Usisahau kuchukua chasis namba kwenda polisi au interpol kuangalia kama hilo gari halijaibiwa au la. Manake unaweza kukuta gari limeibiwa zimbabwe na kuja kuuzwa bongo ukawa umeingia mkenge.

Na hakikisha huyo anayekuuzia hiko chombo una mawasiliano yake au ukawa na details zake zote, ili ikitokea umepata matatizo na hilo gari alilokuuzia unaweza ukamtafuta akakupa ABC za hilo gari lake.

CC RRONDO & mshana jr
---

asanteni kwa uzi,

kuna baadhi ya vitu huwa navifanya na kuna baadhi ya vitu umenifunza mkuu, kwa mfano nimewah kununua gari three times but muda wote nalipaga cash mkononi, hili la benk ni gud idea umenipa mkuu.

pili...huwa nikitaka kununua gari nazunguka yard si chini ya 3 hadi 4 kujua bei ya gari nilitakalo, kisha naenda kijiwen nawambia watu nataka gari kwa hiyo wanawapigia watu wenye gari nilitakalo nakagua kisha wanaondoka... then mwisho wa siku namuita au naelejea yard niliodhan ina gari nililiolipenda.

pamoja na kufanya yote haya....niligundua yard wana bei sana iko juu.
bt gari mbili kati ya hizo 3 nilinunua kidongo chekundu, baada ya kufanya research zote hizo.

sasa mdau aliesema pale wanapiga atuambie sehem nzuri yenye magari mazur na bei ilio rafiki.

bt km mdau alivyosema kutulia, kujipa muda wa kutosha wa kuzungukia, nk
.......
---
Yard nyingi wako straight. Ila taratibu kidogo nyepesi
1.angalia gari unayoitaka ukiagiza ni bei gani na ukinunua yard bei gani. Mara nyingi bei ya yard iko juu,sasa angalia kilichozidi kina worth time wasting na inconveniences za bandarini,tra etc?

2.nenda na fundi akague gari uitakayo kabla na baada ya kuilipia.

3.yard za kueleweka mara nyingi wanakupa akaunti yao ulipie benki baada ya hapo kesho take tu wanakupa gari na kadi yenye jina lako.

Epuka vi yard vyenye gari mbili tatu!
---
Hatua za kufuata kwanza za kufuata

1. Kujua mahitajibya gari unalotaka kulichukua

2. Jiridhishe kwa kwenda ofisi za TRA kuangalia je anayekuuzia gari ndiye mmiliki wa gari hilo kwa kukupa vielelezo ambavyo ni vivuli copy

3. Tafuta fundi mwaminifu akusaidie kukagua gari ikiwa ni pamoja na kuliendesha ili kugundua udhaifu wake.

4.shauriana na fundi baada ya kutoka kulikagua gari

5.Tafuta ofisi yamwanasheria akuandalie mkataba wa mauziano ya gari

6.usilipe cash muombe acount umuwekee hela na vielelzo ubaki navyo au piga photo copy mkabidhi
Nendeni kwa mwanasheria mkakabidhiane na yeye aweke sahihi na muhuri wake

7.ukikamilsha ndani ya 3 jitahidi uanze process za kubadilisha jina la umiliki katika kadi ya gari

Ni hayo tu ninayojua mengine utaongezewa na wengine

sent from HUAWEI
 
Kuna watu niliwa mention kwenye hii thread. Ni watu ambao wana michango mizuri sana hasa inapokuja suala la magari. Lakini @Moderaor Invisible whoever has the power/authority kafuta hayo majina,sijajua nini lengo lake au siruhusiwi ku mention mtu kwenye thread!
 
Last edited by a moderator:
Uzi mzuri kaka.

Ila kuliko kusumbuka na kadhia zote hizo bora uagize la kwako toka japan moja kwa moja. Atleast kule una guarantee kuwa unapata kitu cha uhakika.

Pia umesahau swala la usafi, kuna magari ndani machafu kinoma, viti vinanuka utadhani walipanda mbuzi huko ndani.

Pia, angalia service history ya hilo gari na aina ya service inayofanywa kwenye hilo gari. Kuna magari yanaenda service yakiharibika tu na si wakati wowote. Kama gari lina service ya kila baada ya muda au kilometa litakuwa na uhakika wa kuwa zima pale unapotaka kulinunua.

Unaweza kuangalia hilo gari lilikuwa linatembelea barabara za aina gani, kuna wale watumiaji wa upanga posta au wao ni full lami mwanzo mwisho. Hawa magari yao yanakuwa nazima kidogo hasa kwenye pysical part ya nje kuliko yale ambayo mwanzo mwisho ni "all weather road"

Usisahau kuchukua chasis namba kwenda polisi au interpol kuangalia kama hilo gari halijaibiwa au la. Manake unaweza kukuta gari limeibiwa zimbabwe na kuja kuuzwa bongo ukawa umeingia mkenge.

Na hakikisha huyo anayekuuzia hiko chombo una mawasiliano yake au ukawa na details zake zote, ili ikitokea umepata matatizo na hilo gari alilokuuzia unaweza ukamtafuta akakupa ABC za hilo gari lake.

CC RRONDO & mshana jr
 
Last edited by a moderator:
Usijali kaka sometimes nao ni binadamu kuna kupitiwa kwa hapa na pale, nk
Pia ni vema huu uzi ukajitegemea usije ukaunganishwa na ule unaohusu magari kule kwakuwa hii nayo ni mojawapo ya nyuzi ambazo zina faida kubwa kwa mtumiaji yeyote wa JF
Uliichoandika kina msaada kwa kila mmoja mwenye ndoto ya kumiliki gari lakini vilevile hata kwa kumshauri ndugu jamaa au rafiki
Binafsi nikupongeze RRONDO kwa Uzi huu murua

pamoja mkuu tulisongeshe...
 
bulldog,
Sahihi kabisa ila shortcut ya documents ni TRA INVESTIGATION DEPARTMENT FLOOR NO 4 ROOM NO 1 TRA HEADQUARTERS, binafsi nina kesi inaendelea hapo ila sitaweka details zozote mpaka itakapokwisha.

Kupitia kesi yangu hii nimejifunza mengi sana, ndio maana nikasema huu uzi una faida tupu kwa wale watakaosoma na kuzingatia kila mchango
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu niliwa mention kwenye hii thread. Ni watu ambao wana michango mizuri sana hasa inapokuja suala la magari. Lakini @Moderaor Invisible whoever has the power/authority kafuta hayo majina,sijajua nini lengo lake au siruhusiwi ku mention mtu kwenye thread!

Labda hukuwaomba ruhusa
 
Last edited by a moderator:
asanteni kwa uzi,

kuna baadhi ya vitu huwa navifanya na kuna baadhi ya vitu umenifunza mkuu, kwa mfano nimewah kununua gari three times but muda wote nalipaga cash mkononi, hili la benk ni gud idea umenipa mkuu.

pili...huwa nikitaka kununua gari nazunguka yard si chini ya 3 hadi 4 kujua bei ya gari nilitakalo, kisha naenda kijiwen nawambia watu nataka gari kwa hiyo wanawapigia watu wenye gari nilitakalo nakagua kisha wanaondoka... then mwisho wa siku namuita au naelejea yard niliodhan ina gari nililiolipenda.

pamoja na kufanya yote haya....niligundua yard wana bei sana iko juu.
bt gari mbili kati ya hizo 3 nilinunua kidongo chekundu, baada ya kufanya research zote hizo.

sasa mdau aliesema pale wanapiga atuambie sehem nzuri yenye magari mazur na bei ilio rafiki.

bt km mdau alivyosema kutulia, kujipa muda wa kutosha wa kuzungukia, nk
.......
 
Sahihi kabisa ila shortcut ya documents ni TRA INVESTIGATION DEPARTMENT FLOOR NO 4 ROOM NO 1 TRA HEADQUARTERS, binafsi nina kesi inaendelea hapo ila sitaweka details zozote mpaka itakapokwisha
Kupitia kesi yangu hii nimejifunza mengi sana, ndio maana nikasema huu uzi una faida tupu kwa wale watakaosoma na kuzingatia kila mchango

very useful....naomba ruhusa kuchukua mstari kwenye hii post.
 
wiseboy,
kila mahali kuna watu wema na wabaya. sio wote wapigaji pale kidongo chekundu. inabidi tu kuwa makini na yeyote anaekuuzia gari,zingatia yote ambayo wadau wameyasema kwenye hii thread.
 
na pia naomba kujua mkuu, hivi ni kwel wale wafunga miziki kwenye magari vile vifaa ni aghali sana au nao ni wezi tu. wapi wanafunga mziki kwa bei reasonable kwenye gari.
 
uko sahihi mkuu. ila sometimes bajeti inabana inabidi 'umvue' mtu hapa hapa mjini.....ukilenga unatoka na kitu cha uhakika,just be patient....kuna watu wanauza magari kwasababu ya shida mbalimbali.

Kuna mdau fulani anahusika sana na magari aliniambia kama unataka gari ya kununua hapa bongo bora ununue kwa wahindi au waarabu wa kkoo. Wale jamaa wanatunza sana magari yao halafu pia hayapati dhoruba sana kama haya mengine. Utakuta gari inazunguka hapohapo kkoo au posta na upanga.

Na pia hao jamaa wanauza gari nzuri sana kwa bei chee kwasababu wanataka kuleta nyingine mpya zaidi.
 
119 Reactions
Reply
Back
Top Bottom