Dalili za injini inayoelekea kufa na namna ya kuilinda injini ya gari yako ili iwe na maisha marefu

geranteeh

JF-Expert Member
May 21, 2015
266
618
Sote tunajua engine ndio kitu cha msingi zaidi kwenye gari kwani kupitia injini ndo tunapata mjongeo wa gari na sehem nyingine kufanya kazi. Watu wengi humiliki magari bila kujua namna bora ya kuitunza injini, kumbuka gharama za kurekebisha ama kufufua engine ya gari yako ni kubwa sana au gharama za kununua engine mpya ni kubwa kuliko pengine kifaa chochote kwenye gari. Ningependa leo nielezee namna ya kujua endapo injini inakuhitaji au inaumwa so inataka kukwambia kitu.

Kumbuka gari yako unapoiwasha inatakiwa kuwe na sauti tatu tu na si vinginevo. Sauti ya kwanza ni Engine ya gari ya pili ni Sauti za vifaa vya burudani kama vile redio mziki na zauti ya tatu ni honi pindi ukipiga honi.. (Tofauti na hapo si sauti tena bali ni kelele)

Unapowasha gari yako ni vema hata kwa sekunde kumi usikilize mwa makini mlio wa injini yako je unalia unavotakiwa? Ukisikia sauti nyingineyo basi jua engine ina shida na inahitaji kutatuliwa.

Endapo unawasha gari na kusikia kelele za ko ko ko hata kwama ni kwa mbali jua basi kuna shida na kiufupi kwenye thread zilizopita nimeelezea sana kuhusiana na swala la Oil ya gari yako (kama hujapitia ni bora uzisome upate elim)

Watu wengi huwa wanapitisha service za gari zao either kwa kusahau au kwa kipato (wazee wa i know my car).
Katika vitu unatakiwa kuwa makini ni service ya gari lako yani kumwaga oil na kuweka mpya pamoja na kubadili filter.

Endapo utazidisha muda wa service hakika oil itakuwa umepoteza ubora na vike viambata vyake vinakuwa vimechoka hivo kupelekea msuguano wa vifaa vilivyomo ndani ya engine kusuguana na hapo lazima utasikia tu milio ambayo si mizuri pindi uwashapo gari.

Taa za check engine na oil endapo sensa ya gari yako inafanya kazi vema basi pindi engine ikiwa na shida basi mojawapo au zote lazima ziwake japo inaweza kuwa ni kwasababu zingine lakini katika hili taa ya check engine ikiwaka inamaana kuna tatzo kwenye engine lakini hii ya chsck oil ina sababu Nne

1. Sababu ya kwanza ni kwamba gari inavuja oil kwahiyo oil haipo ya kutosha au gari yako inakula oil hivo unatakiwa uongezd oil

2. Sabab ya pili ni oil pressure haiko vema ndani ya engine kwa maana uwiano wa oil kwenye kupandisha na kushuka unatakiwa uwe normal na unapokua hauko kawaida taa lazima iwake.

3. Sababu ya tatu ambayo inahusiana na hii mada ni kuisha kwa ubora wa oil yako hivo basi inatakiwa kubadilishwa na mara nyingi hutokea unapopunguza speed labda unavuka tuta au umekanyaga breki gari ikasimama hii taa huwa inawaka na kuzima (blinking) ama inawaka straight

4. Sababu ya mwisho ni filter ya oil kutokufanya kazi vizuri. Kumbuka kila unapomwaga oil ya gari yako ni lazima ubadili na filter ya oil na pia fundi anapoifunga filter mpya anatakiwa ailoweshe kidogo tu na oil then aifunge. Sasa kwasababu ya ubahili au kugokujua ama fundi kufanya uhuni ukabadili oil bila filter basi lazima taa ya oil ifanye ku blink.

Binafsi naamini kama umeamua kumiliki gari basi lazima uwe na mapenzi na gari kama huna mapenzi basi jali gari yako kwa kuipeleka kukaguliwa kila baada ya muda fulani. Hakika chombo cha moto ni kitu unahitaji kuwa nacho makini mda wote maana lolote laweza tokea mda wowote hivyo tahadhari ni muhimu sana.
 
KWanza ya yote .serikali itaki kuweka barabara zenye kiwango. Gari zinataka barabara si vungine.
Japani unapata gari ya mwaka 1993 lakini unaweza kusema mpya.

Hiyo 1993 kama hipo tanzania unaweza kusema chuma chakavu sababu imekufa kwa barabara mbovu
 
KWanza ya yote .serikali itaki kuweka barabara zenye kiwango.gari zinataka barabara si vungine.
Japani unapata gari ya mwaka 1993 lakini unaweza kusema mpya.
hiyo 1993 kama hipo tanzania unaweza kusema chuma chakavu sababu imekufa kwa barabara mbovu
Ukweli ambao wengi hawataki kuusikia mkuu ila miundombinu ni mojawapo wa chanzo cha ubov wa magari na ajali nyingi
 
Asante mkuu kwa elimu, naomba kuuliza kitu gani kinapelekea gari kuwaka taa ya over speed bila kuwasha na ikishawaka gari inapobadili gear inastuka. Aina ya gari ni Toyota Passo.
 
Asante mkuu kwa elimu, naomba kuuliza kitu gani kinapelekea gari kuwaka taa ya over speed bila kuwasha na ikishawaka gari inapobadili gear inastuka. Aina ya gari ni Toyota Passo.
Boss kwa uwelewa wangu hiyo taa ni warning light kwamba gari imeover speed hivo unatakiwa uwe makini sasa kweny gear kustuka pia nataka kupata uhakika je mwanzoni ilikua inafanya hivyo?
 
Boss kwa uwelewa wangu hiyo taa ni warning light kwamba gari imeover speed hivo unatakiwa uwe makini sasa kweny gear kustuka pia nataka kupata uhakika je mwanzoni ilikua inafanya hivyo?
Taa inawaka yenyewe bila kuminya ile burton, lakini pia mwanzo haikua hivyo
 
Taa inawaka yenyewe bila kuminya ile burton, lakini pia mwanzo haikua hivyo
I think kuna shida kwenye mfumo boss
Usikubali kubumba bumba hasa kwa gari za kisasa
Tafta mtu wa mashine ujaribu kuifanyia diagnosis
 
Back
Top Bottom