Sababu zinazopelekea engine ya gari yako kuzima ghafla

geranteeh

JF-Expert Member
May 21, 2015
266
620
Kuna mengi sana yanapita katika kichwa cha dereva anaeendesha gari alafu ikazima ghafla bila ya yeye kuizima na mbaya zaidi itokee hivyo ikiwa geji ya mafuta inaonesha mafuta yapo ya kutosha kwenye gari yako. Hakika kama si mjuzi wa gari unaweza kulia pale unapojaribu kuiwasha na ikagoma kuwaka na hapo sisemei gari imekuzimikia katika mazingira gani, Kwa hakika ni wakati mbaya ambao hakuna anaetamani kukutana nao. Katika makala hii utajifunza kutokuwa na wasiwasi kwani yawezekana ikawa ni katika matatizo haya nitakayoyaelezea hapa chini na kumbuka si kwa gari za kizamani tu hata gari mpya inaweza kukutokea ni vema ukakumbuka ni chombo cha moto pale unapokiendesha basi tegemea lolote kutokea wakati wowote.

1. INJINI KUPATA MOTO SANA (OVERHEAT)

Sababu kubwa ni hii kwani wengi wetu huwa hatuna utamaduni wa kukagua mfumo wa kupoza injini za magari yetu kama vile Maji kwenye rejeta, Mfuniko kuhakikisha umeufunga vema wa rejeta ama feni endapo inafanya kazi. Ukichana na yote hata ule mshale wa Joto uliopo kwenye Dashboard je upo sawa? wengi wetu akitia gia ni kuangalia mbele tu akicheki dashboard basi ni kuangalia mafuta ama speed anayotembea.Gari huzima pindi joto linapozidi kupita kiwango hivo ni vema kuangalia ili kujua endapo kuna tofauti katika joto la injini yako kabla gari haijafikia kiwango cha kuzima lenyewe.

2. KUZIBA KWA KIBUYU CHA MASEGA

Nimekuwa nikipata malalamiko ya wateja ambao wao masega ya gari zao hayajaibiwa bali yameziba. Kumbuka masega nayo yana kiwango cha maisha cha kutumiwa kwenye gari yako baada ya huo muda yanatakiwa kubadilishwa,Kumbuka gari tunazozitumia zinakuwa tayari zimekwisha kutumika huko zilipotoka hivyo basi inawezekana imefikia kiwango cha kuhitaji kubadilishwa kubuyu cha masega na mmiliki kutokujua. Hii huja na dalili nyingi lakini kubwa zaidi ni Gari kutumia mafuta mengi kuliko inavyohitajika, Gari kukosa nguvu na pia muungurumo au mtetemeko kuwa mkubwa sana kwani hakika unakua imezima mfumo wa exhaust.

3. OIL LEVEL KUWA CHINI YA GEARBOX (TRANSMISSION FLUID)

Watu wengi wanakumbwa na shida ya gari kuzima kutokana pia na wamiliki wengi kutokuwa na tamaduni ya kuangalia kiwango cha transmission fluid kwenye gearbox. Katika sababu zinazopelekea gari kuzima ghafla hasa kwa gari za kisasa ni kushuka kwa kiwango cha transmission fluid na hii inatokana na sababu nyingi lakini kubwa ni kuigunga sample hasa kwa gari zilizo chini na kupelekea kuvuja kwa kimiminika.

4. MATATIZO YA UMEME/KUKATIKA KWA FUSE

Gari iwe ya zamani au ya kisasa ina mfumo wake wa computer na wa umeme ambao upo programmed hivyo unapobugudhiwa hupelekea gari kuzima, Nasema kubugudhiwa kutokana na tabia zetu za kuongeza vitu kwenye magari kama vile vifaa vya muziki, Mataa na vinginevyo kwa mafundi wa uchochoroni ambayo hupelekea kwa fuse kuungua. Kwa gari nyingi dalili za computer kuwa disturbed huwa ni taa ya check engine. Hakika hatutakiwi kupuuza hii taa.

5. TATIZO LA ALTERNATOR YA GARI KUTOFANYA KAZI

Altenator ni chanzo kikuu cha umeme katika gari yako na betri ni chanzo namba mbili cha umeme katika gari. Betri ya gari yako hufanya kazi mbili kubwa. Moja ni kuwasha gari alafu baada ya hapo gari hujitengenezea umeme wake yenyewe kwa kutumia altenator na kazi namba mbili ya betri ni kufanya kazi pindi gari inapokuwa imezimwa kama vile kuhakikisha computer ya gari yako kuwa na kumbukumbu sawia hata kama gari ikiwa imezimwa hivyo gari huwa na kumbukumbu wakati wote bila kupotea na ndiyo maana unapochomoa terminal gari ikiwa imezimwa basi na kumbukumbu zote hupotea mfano mzuri ni saa yako kupoteza majira lakini kazi nyinginezo ni unaweza tumia Hazard light kipindi cha matatizo hata gari ikiwa imezimwa ama kuzikiliza radio, Kuwasha Taa na vinginevyo. Kazi ya Alternator ni kuhakikisha umeme upo wa kutosha kipindi unapowasha gari yako na kumbuka matumizi ya betri ya gari yako huisha pale tu unapowasha gari kazi yote hupokewa na alternator na ndiyo maana gari nyingi ukiwasha gari unaweza chomoa betri na gari isizime na still ukaendelea kufanya vyote kwenye gari yako, hapo nadhani umeelewa kwanini nimesema Alternator ni chanzo kikuu na hapo bila kusahau jua kwamba betri ya gari yako inachajiwa na alternator. Sasa basi pindi hii alternator inaposhindwa kufanya kazi basi jua upo kwenye shida kubwa kwani utakuwa unatumia umeme wa betri pekee hivyo betri ikiisha nguvu automatically gari yako itazima. Dalili za alternator kutokufanya kazi ni pindi unapoona kwenye dashboard taa ya alama ya betri imewaka. Binafsi ilishawahi nitokea nikiwa safarini ambapo betri yangu ilikuwa iko vizuri na ilikuwa asubuhi sana, Ilinichukuwa kilometa 10 kumpata fundi ambaye alinirekebishia. Kumbuka hii inaweza kukutokea wakati wowote sababu kwenye alternator kuna vi brush ambavyo vikiisha basi unatakiwa kubadilisha hivyo ikikutokea hutakiwi ku panic.

NINI CHA KUFANYA ENDAPO INJINI YA GARI YAKO IMEZIMA GHAFLA?

Kikubwa cha kufanya ni kuangalia usalama wako ulio nao na pia wa mali zako kwa kujitahidi kuiegesha gari pembezoni mwa barabara alafu ukae kwa muda kidogo uangalie nini tatizo kwa maana ya kama shida ni coolant hiyo unaweza kuirekebisha kwa kuongeza mwenyewe lakini kama shida ni kubwa zaidi ni vema ukawasiliana na fundi wako ila kama kabla ya gari yako kuzima kuna dalili uliziona katika hizo nilizozitaja hapo juu basi utakuwa ushajua tatizo litakuwa ni nini na kama una dalili kama za hapo juu basi peleka gari yako kwa fundi kukaguliwa ama subiri matokeo hasi kukupata.....
 
Back
Top Bottom