MUONGOZO: Mambo ya kuzingatia unaponunua gari lililotumika ndani ya Tanzania

kinjumbi one

kinjumbi one

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Messages
1,557
Points
2,000
kinjumbi one

kinjumbi one

JF-Expert Member
Joined May 27, 2015
1,557 2,000
Toyota brand kwa bongo sijawahi kuona eti imepaki kwa ubovu ama kukosa spea...VITZ ni sawa kama ni DISMINDER (usiejali dhihaka za watoto was mjini) wenyewe wanaziita "FREEZER"
Hahahaha haya bhana mkuu, sema wanazoziita Freezer ni passo bhana.
 
E

enstein1

Member
Joined
Jul 14, 2009
Messages
66
Points
95
E

enstein1

Member
Joined Jul 14, 2009
66 95
Ushauri mzuri sana, utasaidia wengi! Kuna watu wakipata hela wanakuwa na papara sana!
 
E

enstein1

Member
Joined
Jul 14, 2009
Messages
66
Points
95
E

enstein1

Member
Joined Jul 14, 2009
66 95
Kuna watu niliwa mention kwenye hii thread. Ni watu ambao wana michango mizuri sana hasa inapokuja suala la magari. Lakini @Moderaor Invisible whoever has the power/authority kafuta hayo majina,sijajua nini lengo lake au siruhusiwi ku mention mtu kwenye thread!
Hawataki ku-promote biashara ya mtu! Labda uilipie
 
Mlandege

Mlandege

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Messages
1,134
Points
1,500
Mlandege

Mlandege

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2012
1,134 1,500
BREVIS imetulia sana barabarani kwa safari ndefu hasa ukiwa una mwendo (zaidi ya 100 kph, tatizo tochi/faini) pia zinabugia mafuta mithili ya PRADO. Xtrail jiandae kwa kukusanya namba za mafundi magari angalau 10.
Ko X trail ni kimeo yaani
 
galindas

galindas

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2013
Messages
982
Points
1,000
galindas

galindas

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2013
982 1,000
Ko X trail ni kimeo yaani
Mimi mtu akiniambia xtrail ni kimeo sikubali. yupo mtu ninayemfahamu anaitumia huu mwaka wa nne na route zake ni arusha tanga. ukweli watu hatujui kuzitunza. rejeta wanatia maji, oil siyo iliyokuwa prescribed na manufacturer lazima ife.
 
joshua_ok

joshua_ok

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Messages
9,627
Points
2,000
joshua_ok

joshua_ok

JF-Expert Member
Joined Jun 27, 2012
9,627 2,000
Mimi mtu akiniambia xtrail ni kimeo sikubali. yupo mtu ninayemfahamu anaitumia huu mwaka wa nne na route zake ni arusha tanga. ukweli watu hatujui kuzitunza. rejeta wanatia maji, oil siyo iliyokuwa prescribed na manufacturer lazima ife.
Xtrail vs RAV 4 je?
 
aminiusiamini

aminiusiamini

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Messages
3,593
Points
2,000
aminiusiamini

aminiusiamini

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2011
3,593 2,000
wabongo hawajui magari. Wengi wananunua kisa eti plate number. Hawaangali mileage ya gari,ubora hapana ilimradi inaonekana vizuri nje.

hawa madalali ni kuwapiga marufuku.
 
Jodoki Kalimilo

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Messages
10,073
Points
2,000
Jodoki Kalimilo

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2012
10,073 2,000
Uzi unaoishi huu ...unafaa kama rejea once unapotaka kununua gari
 
joshua_ok

joshua_ok

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Messages
9,627
Points
2,000
joshua_ok

joshua_ok

JF-Expert Member
Joined Jun 27, 2012
9,627 2,000
Kununua gari TZ hakikisha bei iwe nusu vs unayoiona kwenye mtandao
 
Kasu

Kasu

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2012
Messages
347
Points
250
Kasu

Kasu

JF-Expert Member
Joined May 3, 2012
347 250
Sorry kama nitakuwa nje ya mada, endapo nikiwa na 4M ninaweza kuagiza Vitz Japan? Au itabidi ninunue tu used za hapa TZ?
 
bbwaoy

bbwaoy

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2015
Messages
468
Points
500
bbwaoy

bbwaoy

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2015
468 500
Ni bora nitoboke mfuko ila mimi huwa sipendi vitu used... huwa napenda sana kumenya karatasi ya vitu vipya tu... usafiri wangu ni daladala ila gari yangu ya kwanza lazima ni zame showroom ni menye mwenyewe....

Yote kwa yote pongezi kwa kutujuza! Safi
 
pureView Zeiss

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2016
Messages
2,803
Points
2,000
pureView Zeiss

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2016
2,803 2,000
Aisee asante sana kwa ushauri wako muruwa yaani huwezi amini wiki hii yote natafuta gari lakini kwa style niliyoiona ya madalali ni usanii mtupu,huu uzi wako ni kama umeniona mimi jinsi ninavyotafuta gari bila mafanikio

Mungu akubariki
 
Msingida

Msingida

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Messages
4,864
Points
2,000
Msingida

Msingida

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2010
4,864 2,000
Vipi kuhusu kilomita iliyotembea gari,nayo ni ya kukonsida?
 
mkemiamkuu

mkemiamkuu

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2014
Messages
343
Points
250
mkemiamkuu

mkemiamkuu

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2014
343 250
Mkuu RRONDO Mungu akubariki sana kwa huu Uzi, mi natafuta Harrier old model, vipi unanishauri nini na labda bei zake kwa hapa TZ inaendaje? Thanks in advance
 
MLA PANYA SWANGA

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Messages
4,384
Points
2,000
MLA PANYA SWANGA

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2015
4,384 2,000
Baada ya kusikia watu wengi 'wakiumizwa' na 'kupigwa' wakiwa kwenye harakati za kutafuta usafiri uliotumika nchini, nimeona sio mbaya nikitoa ushauri ni jinsi gani unaweza kuepuka majanga kwenye zoezi hilo.

Naandika kama mnunuzi au muuzaji wa aina hio ya magari, kwahio siegemei upande wowote na ninachokiandika hapa sio sheria naweza kuwa sahihi au nisiwe sahihi ila ni imani yangu lipo litakalosaidia baadhi ya watu.

Njia muhimu za kufuata ili kupata gari unalotaka ni kama ifuatavyo:

1. Fanya utafiti mdogo juu ya gari unalolitaka: Uliza ujue gari unalolitaka linauzwa kiasi gani[makadirio]. Ukiweza kujua bei ya showroom au ukiagiza mwenyewe Japan halafu linganisha na bei utakayopewa hapa. Hili ni muhimu kwa sababu nimeshuhudia watu wananunua magari yaliyotumika Tanzania kwa bei ambayo ukiagiza mwenyewe unalipata kutoka japan au ukiongeza kidogo tu unapata la showroom.

2. Usiwe na haraka: Usiwe na haraka kabisa kwenye kutafuta gari. Utaletewa kila aina ya gari na usipokuwa makini utanunua gari bovu. Angalia taratibu angalau magari matano tofauti kwenye chaguo lako ndipo uamue, madalali watakusumbua ili mradi tu wapate cha juu.

3. Epuka madalali: Kama unaweza epuka madalali. Tafuta gari kwa kuuliza watu ulio karibu nao, ndugu jamaa na marafiki au unaofanya nao kazi au biashara. Hii ni nzuri chochote kikitokea una pa kuanzia. Madalali wengi hawajali maslahi yako wala ya muuzaji cha muhimu kwao ni cha juu tu. Gari la 4m dalali atakuuzia 5-6m.

4. Tafuta Fundi: Ukilipenda gari lolote tafuta fundi akusaidie kulikagua, hata kama una ujuzi(idea) na magari kuna vitu hutaviona ila fundi atakusaidia. Kuwa makini kuna mafundi huwa wanabonyezwa wakufiche hitilafu halafu baadae wanarudi kupewa chao ukishauziwa kanyaboya.

5. Epuka gari lililopigwa rangi: Epuka gari iliopigwa rangi siku chache kabla ya kuwekwa sokoni, wazoefu wanajua gari za aina hio ndio umuhimu wa fundi unapokuja. Gari inaweza kuwa imegongwa hivyo imenyooshwa na wanakuzuga kwa rangi inayong'aa. Siku hizi rangi hata 200,000 unapiga gari nzima ila ukinunua hilo baada ya mwezi rangi inababuka yote.

6. Epuka gari lililooshwa engine: Ukikagua gari ukiona limeoshwa engine ogopa sana. Mara nyingi magari yanaoshwa engine kuficha 'leakage', yaani oil na vitu vingine vinavyovuja kutoka sehemu mbalimbali za engine.

7. Jaribu gari wewe mwenyewe: Ni muhimu kuendesha na kuijaribu gari wewe mwenyewe hata ukienda na fundi. Ipitishe njia mbovu usikie jinsi ilivyo chini, chochote kinachogonga kuwa makini, usisikilize ukiambiwa ni tatizo dogo, kwanini hakurekebisha. Ingawa yapo matatizo madogomadogo ila kuwa makini.

8. Usiangalie plate Namba: Usibabaishwe na namba, eti hii C, D etc. Kuna gari namba A ziko vizuri kuliko namba C. Muhimu ni hali ya gari husika kwa muda huo.

9. Nenda TRA kujiridhisha: Ni muhimu kujua ukweli na status ya gari na mwenye gari. Jiridhishe anaekuuzia ndio mwenye gari. Akuonyeshe nyaraka zote halisi hata za kodi aliolipia.

10. Mwisho kabisa ukilipenda gari fanyeni makabidhiano kwa kuandikishana kwa mwanasheria. Ukiweza lipia benki na ubaki na risiti kama ushahidi wa malipo kupitia akaunti yake. Epuka kubeba cash kumpelekea muuzaji mahali alipo.

Haya machache naamini yanaweza kuwa msaada kwa watu wanaonunua magari yaliyotumika nchini,wengine mnaweza kuongezea mawili matatu na kurekebisha nilipokosea.Naomba nifahamishe kuhusu Toyota Alphard 2400cc ulaji mafuta kwa long Safari na mizunguko ya mjini. Weakness zake na ubora wake.
 
NetworkEngineer

NetworkEngineer

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2012
Messages
1,818
Points
2,000
NetworkEngineer

NetworkEngineer

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2012
1,818 2,000
Hivi ukinunua gari kwa mtu gharama ya kulipa TRA wakati wa kutransfer kadi inakuwa kiasi gani..maana nimesikia ni 18% ya bei uliyonunulia gari, sasa mfano nimenunua IST milion 9 nikilipa na 18% ya transfer inafika milion 10.6 , sasa hapa si bora niagize Japan au ikoje hapa
 

Forum statistics

Threads 1,336,569
Members 512,660
Posts 32,543,782
Top