Muonekano mzuri wa Stendi mpya ya Mbezi umeharibiwa na Siasa zetu za kutafuta sifa kwa Wanyonge waliobatizwa Masikini

Umenikubusha mbali tulipokuwa tunachanganyika skuli kuna kabila lilikuwa linapanda juu ya vyoo vya kukaa tulikuwa tunapata tabu sana mpaka walipo elewa matumizi ya vyoo hivyo hivyo kwenye hili tutaelewana baada ya hasara
 
Hata ofisi za serikali waruhusiwe pia mpaka pembeni ya Ikulu
Ofsi sio sehemu inafanyika biashara

Stend ni sehemu ya watu kufanya biashara, ni haki ya kila mtu kufanya biashara, stend ni ya Watanzania wote maskini na tajiri, kama unaona huo ni uchafuzi na unakuboa, Jenga stend yako ama boresha nyumbani kwako pakuvutie ili uvinjali zaidi
 
Kama muonekano ule mzuri kuanzia Jengo zima na mandhari ya pale leo hii umeanza Kuharibiwa kwa Wanasiasa wetu Wanafiki wanaocheza na Uelewa mbovu wa baadhi ya Watanzania uliochanganyika na Ushamba wao kwa Kuwaruhusu hadi Wamachinga, Mama Lishe na Vibaka wajazane mule ndani Stendi hadi kuleta Kero naomba waruhusiwe pia kwenda pale JNIA Terminal III haraka sana.

Kama kweli Wanasiasa wetu nchini Tanzania wanawapenda kweli kweli Watu (Wananchi) wao hasa Masikini ( Walalahoi ) basi wasiishie tu kutafuta Sifa za Kiumaarufu kwa Kuwaruhusu waingie ndani kabisa ya Stendi mpya ya Mbezi Kufanya Biashara zao bali wawaruhusu pia kuingia JNIA Terminal III, KIA na kama kweli tunawapenda basi waruhusiwe kuingia hadi Ikulu Magogoni na Chamwino.

Inakera!
Tupia tupichapicha! Tujadili kwa hoja na uhalisia
 
Jna nimerudi toka safari mule ndani ya stendi
Ilikuwa vurugu tupu kitendo cha kuwqruhusu wamachinga,wauza mayai ya kuchemsha,mama ntilie sijui kama stendi ile itadumuu
Cha ajabu mule ndani wapiga debe kama kawa wapo

Ova
20210228_075937.jpg
 
Nasikia Mzee karuhusu watu wapange mbogambonga ile nyia ya kwenda feri toka lango kuu la IKULU hadi kwenye pantoni.... sababu pale ferry wamebanana sana - cha msingi tu wawe na vitambulisho.
 
Tuacheni wanyonge tutumie fursa hii kutoa huduma kwa wasafiri. Na bado kwenye reli iendayo kasi mtatuona pia
Stand ya ma bas ya mkoani sio sawa na airport, msilinganishe hivyo
Hiyo mindset mlivyokuwa nayo ndy inawaletea
Kasumbaa .....hiyo stendi muda si mrefu itakuwa kama ya zamani ubungo pale
Kama umeamua kufanya vitu ki standrad kila kitu endesha hivyo

Ova
 
Wanyongeeeeee....hili jina linanikera sana
Inakua kama yan nakuita wew hapo “Mnyonge wa hii nchi”.... “Umeteseka sana” 😬😬😬 Nataman kujua maana halisi ya hao wanyonge. Kwa nini wasiitwe tu Watanzania. Kuna ulazima gani wa kuwaita wanyonge/maskini? Miaka 10 someone calling you Mnyonge dah na hakuna hata dalili ya wewe kutoka huko unyongeni
 
Punguza stress ndugu yangu!!
Punguza chuki zako dhidi ya serikali na wananchi wanaoipenda au kuifurahia serikali yao.
Punguza hasira na wamachinga,mamalishe na wengine wanaopambana kupata tonge.

Pita nchi nzima,machinga na mama ntilie biashara zao wanafanya stendi ama pembezoni mwa barabara....ama mahali popote penye shughuli zinazofanya watu kupatikana kwa wingi...mfano viwandani na maeneo yanapopatika wanachuo au hata ndani ya fensi za baadhi ya shule za msingi na sekondari.

Ni upumbavu kutaka watu waruhusiwe kufanya shughuli hizo kwenye viwanja vya ndege au ikulu. Na pia,natiliashaka uelewa wako wa mambo. Jaribu kuwa na akili ya ziada kwenye kupambanua mambo.

ACHA HASIRA NA CHUKI.
Morogoro hawaruhusiwi au morogoro sio Tanzania. Na pale huwezi kuibiwa. Anaekaa sehemu ya wageni ndani ni mtu mwenye tiketi ina maana zile 200 za kuingilia stand machinga wataonyesha vitambulisho au vipi
 
Morogoro hawaruhusiwi au morogoro sio Tanzania. Na pale huwezi kuibiwa. Anaekaa sehemu ya wageni ndani ni mtu mwenye tiketi ina maana zile 200 za kuingilia stand machinga wataonyesha vitambulisho au vipi
Wanaouza mikate na maepo pale Msamvu ni kina nani?
Au pale Singida wenye zile frem ni akina nani?
Au wewe mfanyabiashara mdogo ni nani?
 
Hiyo mindset mlivyokuwa nayo ndy inawaletea
Kasumbaa .....hiyo stendi muda si mrefu itakuwa kama ya zamani ubungo pale
Kama umeamua kufanya vitu ki standrad kila kitu endesha hivyo

Ova
Lazima kutakua na usimamizi
Hakuna uhuru bila taratibu
 
Hawauzi ndani ya stendi Mg. Na kuingia ndani kuna geti kibao unalipa. Acha uongo.
Pale utauziwa mikate ndani.....nenda tu mfano kwenye coater za Turiani.....utaleetewa mpaka chips take away. Labda kama wewe huwa unapita kwa ndega.
 
Inakua kama yan nakuita wew hapo “Mnyonge wa hii nchi”.... “Umeteseka sana” 😬😬😬 Nataman kujua maana halisi ya hao wanyonge. Kwa nini wasiitwe tu Watanzania. Kuna ulazima gani wa kuwaita wanyonge/maskini? Miaka 10 someone calling you Mnyonge dah na hakuna hata dalili ya wewe kutoka huko unyongeni
Si ni brainwash Tu ili kuhalalaisha maamuzi mabovu na ukurupukaji anaofanya
 
Si ni brainwash Tu ili kuhalalaisha maamuzi mabovu na ukurupukaji anaofanya
Mim binafsi sipend kutumia maneno kama masikini, mnyonge, tajiri, ninapomjali mtu yyte. Sasa kumruhusu mtu kufanya kazi ndan ya stand ndo iwe kigezo cha kumuita mnyonge au masikini? Hiyo ni sawa kumsimanga na kumu-under estimate uliemsaidia, it’s like dhihaka.

Kama ndo hivo bas hata hawa wazungu wanaotuletea misaada wakianza kusema hao ni Maraisi wa wanyonge sijui itakuaj
 
Back
Top Bottom