Muonekano mzuri wa Stendi mpya ya Mbezi umeharibiwa na Siasa zetu za kutafuta sifa kwa Wanyonge waliobatizwa Masikini

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,734
Kama muonekano ule mzuri kuanzia Jengo zima na mandhari ya pale leo hii umeanza Kuharibiwa kwa Wanasiasa wetu Wanafiki wanaocheza na Uelewa mbovu wa baadhi ya Watanzania uliochanganyika na Ushamba wao kwa Kuwaruhusu hadi Wamachinga, Mama Lishe na Vibaka wajazane mule ndani Stendi hadi kuleta Kero naomba waruhusiwe pia kwenda pale JNIA Terminal III haraka sana.

Kama kweli Wanasiasa wetu nchini Tanzania wanawapenda kweli kweli Watu (Wananchi) wao hasa Masikini ( Walalahoi ) basi wasiishie tu kutafuta Sifa za Kiumaarufu kwa Kuwaruhusu waingie ndani kabisa ya Stendi mpya ya Mbezi Kufanya Biashara zao bali wawaruhusu pia kuingia JNIA Terminal III, KIA na kama kweli tunawapenda basi waruhusiwe kuingia hadi Ikulu Magogoni na Chamwino.

Inakera!
 
55 Reactions
Reply
Back
Top Bottom