Mungu aliumba jinsia mbili, mwili moja ni kujamiana, kwanini makanisa yanatumia maneno haya kulazimisha ndoa ya mke moja kinyume na utaratibu wa Mungu

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Ukweli huwa haubadiliki hata watu wengi wakiamini uongo ama kudanganywa bila kujua.

Suala la makanisa kutumia hayo maneno ni upotoshaji mkubwa

Mungu alimuumba mwanaume na mwanadamu, Hapo kinachozungumziwa ni jinsia alizoumba, hakukuwa na jinsia ya tatu, hapa sioni kama kuna valid point inayoingia ndoa ya mke moja.

Suala la kuwa mwili moja ni kitendo cha mwanaume na mwanamke kukutana kimwili, mnapounganika mnakuwa mwili moja na hapa ndio maana uzinzi unapigwa vita, uzinzi unaweza kukuhamishia kwako gonjwa la mliekutana na maroho machafu ya wengine waliopita. kwenye 1: wakorintho 6 : 16 "Maana, kama mjuavyo, anayeungana na kahaba huwa mwili mmoja naye--kama ilivyoandikwa: "Nao wawili watakuwa mwili mmoja." nashangaa makanisa yanapaza sauti kuashiria mwili moja kuhusiana na mke moja.

Yesu hakuzungumzia chochote kuhusu polygamy bali aligusia divorce pekee

Musa alioa mke zaidi ya moja
Wafalme karibu wote wa israel walioa zaidi ya mke mmoja, Solomon akiwa kinara

Lets Discuss: maoni yako ni yapi kwenye suala la makanisa kupindisha maandiko ?
 
Uzuri wa dini ni UHIYARI wa mtu, yaani hakuna lazima. Ukiona dini fulani inakuzingua unaachana nayo, unatafuta inayoendana na akili zako.
Hilo ndio jambo la msingi kama wewe unaamini kuwa mwanaume ameumbwa kuoa zaidi ya mke mmoja wewe fanya hivyo, acha kuandika nakala ili uwashawishi na wenzeko wasioamini hivyo
 
Hilo ndio jambo la msingi kama wewe unaamini kuwa mwanaume ameumbwa kuoa zaidi ya mke mmoja wewe fanya hivyo, acha kuandika nakala ili uwashawishi na wenzeko wasioamini hivyo
kwani kuna ubaya gani kulijadili hili?
Nadhani ni vyema mwenye kupinga apinge kwa kusimamia mistari ya biblia ili na sisi wavivu wa kusoma tuweze kujifunza
 
Umejielimisha vya kutosha kuhusu ndoa imechorwa vipi katika biblia kwa kila agano ?
1 Timothy 3:2, 12
Mathew 19:4-5
John 8:28
Nashukuru kwa mchango wako kwani nimejifunza jambo.
Ila hapo Timothy and Mathew naona inawazungumzia maaskofu na sio waumini wa kawaida
 
Nashukuru kwa mchango wako kwani nimejifunza jambo.
Ila hapo Timothy and Mathew naona inawazungumzia maaskofu na sio waumini wa kawaida
Mkuu even wewe ni mtumishi na Bible ikisema askofu is iende nayo moja kwa moja kuwa ni askofu Hiyo ni lugha ya picha.
1wakolintho 7:2
 
Wanaume ni wabinafsi sana. Ubinafsi unafanya wahalalishe mambo yanayowaumiza Wengine.
Yesu alisema: "Basi, mambo yote mnayotaka watu wawatendee ninyi, lazima ninyi pia mwatendee vivyo hivyo." Mathayo 7:12.

Mungu mjuzi wa yote alimpa Adam mke mmoja tu, licha ya kwamba kulikuwa na idadi ndogo ya watu.
 
Back
Top Bottom