Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,040
- 4,080
Hakuna sehemu yoyote ambayo Mungu alikataza hata manabii ama wafame waliomtumikia kuoa mke zaidi ya moja, ukimya wake katika jambo hili ni sawa na sisi wazazi tunapoona mtoto anafanya mambo kwa usahihi tunakuwa hatuna haja ya kumwambia anakosea.
Ni kweli kwamba mwanaume akiondoka kwao yapendeza aende kuanza maisha na mke wake kupata uzoefu wa ndoa lakini baada ya hapo anaweza kuongeza mwengine ndio maana hata manabii waliomtumikia Mungu waliweza kuongeza.
Hata Yesu alizikuta hizo ndoa zikiendelea na hakuwahi kuzikemea wala kuchukizwa nazo, katika mafundisho yake alitumia mfano wa mabikra kumi (10) kuolewa na mwanaume moja
Kuhusu suala la Adam na Eva huo ulikuwa ni uumbaji tu wala sio ndoa, hata Tetea kwa upande wa kuku aliumbwa moja tu na hata kwenye safina ya Nuhu aliingia Tetea moja tu na jogoo moja lakini haikuwa na maana jogoo awe na tetea moja
Mwanaume na Mwanamke kuwa mwili moja sio mwanaume kuwa na mke moja bali ni miili ya kiroho panapo makutano ya mwanaume na mwanamke hata katika uzinzi, hata mwanaume akitembea na kahaba huo tayari ni mwili moja, yapendeza miili hiyo iwe ya wanandoa si ya kizinzi, hata Sisi binadamu tuko wengi lakini mahusiano ya kila mwanadamu na Mungu ni roho moja takarifu na ndivyo ilivyo hata kwa mwanaume akiwa na wake wengi kila mwanamke atakuwa na mwili moja... 1 Wakorintho 6: 16-17- Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. 17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.