Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Dada valentina sio lazima wenye ndoa ndo watoe ushauri bali hata wewe naamini unaweza kumshauri vilivyo zaidi hata ya walio kwenye ndoa.Mkasa mzima umeusikia jitahidi kumsaidia mwanamke mwenzio.
Amepata shauri nyingi zenye busara naamini akizingatia atavuka. Nikiongeza nitakua napunguza utamu[emoji17]
 
Dah,sidhani kama wataacha kukumbushia mara moja moja hata kama ukimsamehe mumeo.Mambo ya ndoa hayahitaji sana ushauri wa watu wa nje maana utamu wa mumeo wewe ndo unaujua.tunaweza kukushauri uachane naye halafu baadae mkipatana utaanza kumwambia kuna wapumbavu walikushauri uachane naye.
 
Pole Leah!
Ni wazi kuwa unapitia kipindi kigumu.
Siku hizi kesi za namna hii ni nyingi sana.
 
Leah2

Tambua kuwa hapo hakuna ndoa tena. Mme wako ameshavunja misingi ya ndoa kwa:
(1) Kufanya uasherati
(2) Kuzaa mtoto nje ya ndoa.

Ingelikuwa tayari nyie mna watoto, ungelisema ngoja tuendelee kuishi pamoja kwa ajili ya kulea familia/watoto.

Watoto hamna, je unachotaka kukivumilia ni kipi?
Naunga mkono hoja..
 
Bora hujazaaa mama tafuta mwanamme mwingne sepa y ujiumize wakati hakuna hata mtoto wa kusema itakua ngum... Chapa mwendo
 
Sijaon

sijawahi ona ushauri pumba kama huu, nyie wanaume wenyewe sikuhizi mnataka kuhudumia familia sawa na wanawake. Mwanaume anayeshindwa kukuheshimu miaka miwili wakati wewe mwanamke unasota Na kitabu for better future basi huyo mwanaume atakuletea watoto kila mwaka
Ndugu yangu ili donda aliweza kupona wazee wa zamani waliweza kuvumilia wakisema wanapata matunzo wewe inaonekana ni braid winner kwenye familia yako so unamvumilia nini just let him go

Oh yes!! Ndipo nilipofikia mwisho wa kufikiria ndugu yangu. Kama ushauri wako unauona wa maana sana uandike hapo.
 
Hii solution umefanya reference kwenye kitabu gani au kesi gani. Hakuna mtu duniani anayezuiwa kulea mtoto wake. huo ni ukiukaji wahaki za binadamu. baba anatakiwa kisheria kutoa matunzo kwa mtoto wake aliyesababisha atokee duniani.

Tembea uone, watoto kibao wanatunzwa na wazazi wasio wao "biologically" hivi mnafikiri kupanda mbegu ndiyo inakufanya kuitwa mzazi? au kuingia labour ndo inakufanya kuwa mzazi?? Uzazi its more of a relationship than the biological involvement. Matunzo....!!!
 
Wewe sio mwanaume ila fedhuli unaetetea upumbavu, mwanamke kusoma ndo mashauzi, mke wangu ana PhD mimi form 6 tunapendana tunaishi vizuri elimu yake haiadhiri biashara zangu huyo jamaa ni mshenzi mpige chini
Sijui nikupe nini jaman, maana umemaliza kila kitu
 
Duh Shepherd Hivi unajifanya hujaelewa kwamba mume amevunja mkataba wa Ndoa sio Kwa kuzini tu ila kuzini Na mdogo wake.
Halafu unaandika TALAKA sio suluhisho?
Dadayangu anza maisha yako bila ya mume msaliti Na dogo jinga Na ujaaliwe sanaaaaa tu
mkuu, watu wengine ni wagumu sana wa kuelewa na wanalichukulia hili suala kwa WEPESI usiokuwa wa kawaida. sijui tuongeeje ndipo waelewe...WANAAMBIWA DADA KATO.MBEWA MDOGO WAKE NA SI HILO TU, PIA KAPACHIKWA MIMBA (NA MAGONJWA YA ZINAA?) lakini bado wanalazimisha MSAMAHA. hili suala limekaa vibaya sana na HALISAMEHEKI 7x70, full stop.
 
Kama ni kweli sioni kama kuna ishu hapo. Mimba itolewe fasta shughuli iishe, na ubaki na mume wako. Kwanza bora kamgegeda mdogo ako unaemfahamu vizuri kuliko angechepuka kwa malaya nje. Nimemaliza
ushauri wa KISHETANI kabisa. unashauri kuua kiumbe kisichokuwa na hatia? muuaji mkubwa!
 
POLE SANA, MIMI NIKUAMBIE USIACHANE NA MUMEO... TENA INAWEZEKANA YEYE ANA AFADHALI KACHUKUA MDOGO AKO, CHA MSINGI WASAMEHE KISHA MDOGO WAKO ARUDISHWE NYUMBANI.

ILA UMESHA FANYA MAAMUZI, UMESHASEMA HUJISIKII KUISHI NA MWANAUME HUYO, UNADHANI SISI TUTAKUSHAURI NINI?
 
Poleh, ila kwa nini hutaki kuzaa hadi sijui shule iishe,walau upate mtt mmoja afu zijazo ndo uzuie kuzaa,ona sasa yalotokea
Na kuiacha ndoa yako nayo unayeloose ni wewe,umesalitiwa na ndoa unapoteza
Nakushauri beba mimba,mdogo wako akizaa watoto wote alee baba yao
ushauri gani wa kipumbaFU huu? unahalalisha mzinzi kuzaa na shemejiye? acha hizo mkuu.
 
Hili kwa kweli ni gumu sana. Nakuhurumia sana. Lakini cha kufanya hapo sikiliza moyo wako unakwambia nin. Lakini, huyo mumeo na mdogo wako, waache waendelee na maisha yao mapya ya ''ndoa''. Walee mimba na kasha mototo atayezaliwa.
 
Maamuz ya kwel yatatoka moyon kwako maana weye ndo unamfaham huyo mumeo we kaa utulie then toa maamuz ...
Usitegemee ushauri outside maana utapotea bure!!!
 
Kwani lengo la mumewe kutembea na mdogo wake lilikua mtoto au tamaa tuu,
Km ni mtoto kwanini alikua anamlazmisha atoe mimba??

Swala la leah kusoma ni makubaliano yake na mume.

Na swala la mume kutembea na mdogo mtu ni tamaa tuu.

Usimuhukumu,

Nakwambia kitu kwa faida yako,

Kati ya wanaume 10, ni mmoja tu atakayeacha kutembea na shemeji yake kama wakipewa uhuru ambao dada mtu aliutoa.

Hata mimi naamini hiyo vita na shetani nisingeishinda kamwe.
 
Mbaya sana hii. Mlifunga ndoa ya aina gani?

Kama ya kikristo, ningekushauri suala zima uliamua kwa kufauata imani ya kikristo......"msamaha". Usiposamehe, unatajiumiza maisha yako yote. Wao wataendelea na maisha yao lakini wewe utaendelea kuteseka kwa maisha yako yote.

Wakristo wanayo sala hii ya muhimu sana:
"Baba Yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe; Ufalme wako ufike, Utakalo lifanyike Duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku, Utusamehe makosa yetu, Kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, Lakini utuopoe maovuni. Amina."

Kwa hivyo, msamaha ni msingi muhimu katika ukristo. Majaribu yatakuja mengi tu na hili la sasa ni mojawapo katika hayo mengi.
 
Back
Top Bottom