Aah mimi ni nani hadi nikusamehe mpendwa, me mwenyewe nahangaika kuomba misamaha daily uwii. Ujue uzinzi ni mgumu sana kuushinda, ndo maana tumeambiwa kabisa "IKIMBIENI ZINAA ". Sema wanaume mnafanya uzinzi ni kama haki yenu ya msingi, kwamba ikitokea tu nafasi ya kuzini, basi hata mtu ahangaiki kujisogeza, chance imepatikana.
You spoke well, kwamba tunahitaji muongozo wa Mungu kuushinda uzinzi (na sio tu uzinzi ila dhambi zote). Niliquote ulivyoongea pale juu kwamba hata ingekutokea wewe umepewa huo uhuru wa kuwa na mke wa mdogo wako, ungefanya kama mume wa Leah. Ndo tunarudi pale pale kwamba mnaona uzinzi kama ni suala la kawaida na haki. Huo uhuru ungepewa na mdogo ako wa kike, ungezini pia? Why not, si uhuru umepewa jamani. Kama tunategemea muongozo wa Mungu basi tusiglorify dhambi kiasi hicho. BTW Mchungaji, mlokole, kiongozi yeyote wa dini, anabaki tu kuwa binadamu kama binadamu wengine. As a matter of fact wote Tumesamehewa Dhambi na si Majaribu, tena wao ndo wanajaribiwa kuliko hata sisi. Mwisho wa siku kila mtu atasomewa hukumu yake na huwezi kusema kwa sababu fulani alifanya hivi na mimi nilifanya.