How old are you?
Partly kabla ya kuanza kumlaumu mumeo nitakulaumu na wewe.
- Kutokuufwatilia kwa karibu uhusiano kati ya mdogo wako na shemeji yake. Mbali na kuwa ni ndugu yako wa damu,utakuwa unajua tabia zake na ni mwanamke kama wanawake wengine.
- Hilo la kuchelewa kumzalia mumeo mtoto. Inaweza kuwa lilikuwa jambo lako tuu na namna alivyokubali inaweza kuwa kutokana na sababu zako ila je? mliridhiana pasipo shaka kwamba atakubali wewe umalize kusoma ndio umzalie mtoto?
Wanaume ni wadhaifu being a man I know this, na wanahitaji kufuatiliwa kwa ukaribu sana hasa kwenye mambo kama haya yanayohusisha hisia. Ki mtazamo sijui namna mambo unavyoyaendesha nyumbani kwako ni maoni yangu kuwa unaipa sana kazi yako na masomo as priority kuliko mume wako (sisemi usithamini kazi) to me, family comes first. Na hiyo weakness shetani ndio akapitia hapo hapo.
Bottom line: Fuata ushauri wa wazazi, dogo arudi kijijini ajifungue mtoto, mtoto akiwa mkubwa, aje hapo nyumbani, kaeni kikao cha kifamilia mdogo wako na mumeo waombe msamaha kwa jambo lililotokea na mzungumzie utaratibu wa matunzo ya mtoto. Life goes on. Ukishindwa hilo. File for a divorce ukaolewe na mtu atakayekusubiria umalize shule (tena Masters, unga na PHd kabisa) ndio ukubali kumzalia mtoto.