Asante mamiiPole sana!! I can feel your pain.
Wakati huu unamhitaji Mola zaidi ya mwana Adam yoyote, Sali kila mara, muombe Muumba wako akupe wepesi wa kusamehe maana najua ni ngumu sana. Kamwe husijilaumu wala husijute kwa makosa ya mumeo na mdogo wako kumbuka "kila nafsi itabeba mzigo wake yenyewe", waache wahangaike na dhambi yao nawa uchafu wao katika nafsi yako, najua ni ngumu ila inawezekana!
Husiogope kuanza upya, huna makosa na Mola pekee ndie mpangaji wa kila jambo, sisi binaadam ni watekelezaji tu wa mipango yake huwezi kujua kwanini ndani ya hiyo dhambi atazaliwa kiumbe hasiye na hatia, Mshukuru Mola kwa kila jambo ila kumbuka utakufa na kuzikwa peke yako!!
Pole sana.
Kwanza dada pole,lakini huu uamuzi uliouchukua sio sahihi;na wala hakuna atakayekulaumu ila mkasa wako ni sawasawa na mbunge mmoja aliyezaa na mdogo wa mke wake.Sasa nitakupm nikupe full stori ya huyo mbunge uone jinsi huyo mkewe alivyosolve huo mkasa.Habari za asubuhi wanajamvi,
Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.
Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.
Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.
Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.
Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.
Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.
Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.
Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.
Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.
Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.
Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.
Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..
Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.
Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.
Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.
Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..
Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.
Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.
Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.
Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?
Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.
Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.
Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.
Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.
Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..
Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.
Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,
Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.
Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..
Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.
Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.
Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.
Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..
Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.
Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.
Wameondoka na sijui walipo kwenda.
Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.
Najiuliza heshima yangu iko wapi?
Jamii inanionaje?
Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?
Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.
Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.
Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.
Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
Ushauri bora zaidHow old are you?
Partly kabla ya kuanza kumlaumu mumeo nitakulaumu na wewe.
Wanaume ni wadhaifu being a man I know this, na wanahitaji kufuatiliwa kwa ukaribu sana hasa kwenye mambo kama haya yanayohusisha hisia. Ki mtazamo sijui namna mambo unavyoyaendesha nyumbani kwako ni maoni yangu kuwa unaipa sana kazi yako na masomo as priority kuliko mume wako (sisemi usithamini kazi) to me, family comes first. Na hiyo weakness shetani ndio akapitia hapo hapo.
- Kutokuufwatilia kwa karibu uhusiano kati ya mdogo wako na shemeji yake. Mbali na kuwa ni ndugu yako wa damu,utakuwa unajua tabia zake na ni mwanamke kama wanawake wengine.
- Hilo la kuchelewa kumzalia mumeo mtoto. Inaweza kuwa lilikuwa jambo lako tuu na namna alivyokubali inaweza kuwa kutokana na sababu zako ila je? mliridhiana pasipo shaka kwamba atakubali wewe umalize kusoma ndio umzalie mtoto?
Bottom line: Fuata ushauri wa wazazi, dogo arudi kijijini ajifungue mtoto, mtoto akiwa mkubwa, aje hapo nyumbani, kaeni kikao cha kifamilia mdogo wako na mumeo waombe msamaha kwa jambo lililotokea na mzungumzie utaratibu wa matunzo ya mtoto. Life goes on. Ukishindwa hilo. File for a divorce ukaolewe na mtu atakayekusubiria umalize shule (tena Masters, unga na PHd kabisa) ndio ukubali kumzalia mtoto.
Wala siwezi kuumia Joyce waache waendelee, sina chakunirudisha nyuma.Kama ndani ya moyo wako bado kuna hisia za upendo kwa mumeo msamehe...utaumia zaidi wakati utakapo achana naye halafu akamuoa mdogo wako utaumia zaidi...ni ushauri ila maamuzi unayo ww sbb unamjua zaidi mumeo na maisha yenu...ila pole sana inauma
Wala siwezi kuumia Joyce waache waendelee, sina chakunirudisha nyuma.
Dah... chief usijichanganye, masharti yalikuwa ni yeye kutokuzaa hadi amalize masomo yake, hii habari ya mdogo wake haimo kabisa [emoji4]Pole sana dada Leah 2,
ushauri wangu, kama yeye ameshavunja masharti nawe hauna bud ya kuendelea nae, kaa pebeni,. Endelea kumuomba Mungu akusaidie upate mme mwenye busara na anae jitambua.,
Hahahaha poleee mambo mengine ni mgumu lakini kayataka mwenyeweIikuwa imebaki kidogo nikupe like,ila hapo uliposhauri familiya ikubaliane mimba itolewe imesababisha uikose like yangu mkuu.
Imeandikwa samehe saba mara sabini, sisi wanaume ni mbwa.
Hii solution umefanya reference kwenye kitabu gani au kesi gani. Hakuna mtu duniani anayezuiwa kulea mtoto wake. huo ni ukiukaji wahaki za binadamu. baba anatakiwa kisheria kutoa matunzo kwa mtoto wake aliyesababisha atokee duniani.Dada angu, African culture is male dominant! Hujui kuwa "Kuchapiwa ni siri ya ndani"? kama ninampenda, i'll keep it silent till I die na wataniheshimu kwa hilo. Huyo mtoto atakuwa ni mwanangu na ole wake mtu anyanyue mdomo (That is IF I love her na alinipa sababu za kueleweka ilikuwaje akazaa na ndugu yangu, huenda ni uzembe wangu,).
Pole sana ,,futa kwanza hiyo video uliyorekodi,,,Habari za asubuhi wanajamvi,
Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.
Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.
Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.
Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.
Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.
Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.
Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.
Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.
Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.
Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.
Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.
Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..
Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.
Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.
Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.
Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..
Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.
Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.
Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.
Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?
Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.
Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.
Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.
Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.
Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..
Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.
Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,
Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.
Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..
Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.
Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.
Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.
Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..
Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.
Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.
Wameondoka na sijui walipo kwenda.
Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.
Najiuliza heshima yangu iko wapi?
Jamii inanionaje?
Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?
Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.
Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.
Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.
Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
Rudi kwa yule aliyewaungisha ndoa atakupa jibu sahihi nini cha kufanya kwa Padri au Mchungaji, nasikia kukuambia nimapema mno kuvunja ndoa yako, nakutalikiana siyo suluhisho la hilo Tatizo.
Huyo dogo akigoma kutoa je?.sioni kama ndo best solution mkuu.Kama ni kweli sioni kama kuna ishu hapo. Mimba itolewe fasta shughuli iishe, na ubaki na mume wako. Kwanza bora kamgegeda mdogo ako unaemfahamu vizuri kuliko angechepuka kwa malaya nje. Nimemaliza