Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Dada yangu polepole tena sana kwa matatizo yalikukuta ukisikia duniani kuna mitihani ya maisha ndio hiyo cha msingi fanya jambo lifuatalo

Kwanza Jiulize katika nafsi yako kuwa wanadamu hapa duniani wanafanya madhambi kiasi gani mbele ya Mola wao wapo wanaojiuza tena kinyume na maumbile, wapo wanauwa wenzao imma kwa ujambazi ,uchawi au kutoa mimba lakin dhambi zote hizi mtu akitubu na kuacha Mwenyezi Mungu humsamehe iweje Mimi na wewe pindi tunapofaniwa makosa makubwa kama haya ukiwa ni mtu wa kiiman utanielewa vizuri

Kisha Ukisema usimsamehe utengane naye uyo mumeo

Angalia Faida na Hasara utazopata kuwa nje ya Ndoa Tena naomba ufikirie vizuri ukiwa umetulia bila Shaka utaona kuvumilia kidonda hiki huenda kukawa na nafuu kuliko kupata kidonda chengine cha kutoka nje ya Ndoa ( kuachika) na kukosa Mume

Tafadhali Dada Angalia sana na ufanye maamuzi sahihi siku hizi waume wenyewe wapo wapi wakuoa?

Chakufanya Mrudishe mdogo wako kwenu Kisha Endelea maisha na Mumeo naamini baada ya mwezi tu utasahau yaliyotokea baina yenu!!!
 
Leah2,nyamaza kimya jawabu litatoka kwa Mungu.nyamaza usije fanya vitu vitakavyo kuumiza,hakua na hamu ya mapenzi mpaka kulala na mdogo wako.
Unaweza ukaamua kwa hasira kumuachia mume mdogo wako kumbe bado unampenda roho itakuuma tena,
Maadam una kazi yako basi nyamaza kwanza urekebishe mood yako,
Kunyamaza kutawafanya wajiulize mambo mengi hiyo ni adhabu tosha
 
Leah2,nyamaza kimya jawabu litatoka kwa Mungu.nyamaza usije fanya vitu vitakavyo kuumiza,hakua na hamu ya mapenzi mpaka kulala na mdogo wako.
Unaweza ukaamua kwa hasira kumuachia mume mdogo wako kumbe bado unampenda roho itakuuma tena,
Maadam una kazi yako basi nyamaza kwanza urekebishe mood yako,
Kunyamaza kutawafanya wajiulize mambo mengi hiyo ni adhabu tosha
Asante..
 
Mara nyingi ushauri wa kweli huwa ni mgumu ktk akili ya mshauriwa, na ndo maana hata mawazo ya wazazi bado kwako ni magumu, matatizo yeyote ktk maisha yanatikiwa yapate suluhsho ambalo haliharibu kilichopo bali kukijenga! Nionavo mimi, kumfukuza mumeo pamoja n mdogo wako nyumbani kwako, umekosea" ona sasa hujui wako wapi na wanafanya nn! Ki ukweeli ni kama umeongeza tatizo, jikubali kama mwanamke, rudi kwenye mstari "upande wa wazazi" na umsamehe mumeo maisha yaendelee, hakuna maisha yasiokuwa na mitihani, wanawake ni vivutio kwa wanaume bila kujali ni mdogo wako au ni shangzi! Na wanume ni dhaifu kwa wanawake bila kujali ni jenerali w jeshi au mkulima! Usipomlinda watamteka tu! Ki msingi hili swala lako limenikumbusha miaka kadhaa iliopita alikuja mdogo wake na wife, alitakalo dem mwanaume hachomoi" lakini tuliyamaliza. Kuwa makini na wadogo zako wa kike, ni sawasawa na mashoga zako tu! Kwani nao ni wanawake, mpigie mumeo umuokoe huko alipotekwa" usinielewe vibaya, nipo dodoma carnival nimetekwa ntaenda home baadae saana"
Kweli sijui walipo na pia sihitaji kujua walipo maana naweza kuishi bila wao, wala sijutii maamuzi yangu kbsa
 
Bora huyu aliyejutia kosa lake kama umemsoma vizuri Leah mmewe haoneshi kujutia kosa lake Na wala haombi msamaha Bali alimwambia yaishe tu simple tu kiasi hicho????
Ni bora hata angeonyesha kujutia labda angesamehewa,angekua mtu mwingine hiki kipindi alicho mpisha mkewe ndo kingekua kipindi kizuri cha kumlilia mkewe amsamehe kwa msg,kutuma watu Na calls kuomba asamehewe
Lakini mwanaume wapi kakauka utafikiri alichokifanya ni kizuri,kua kamwuweza mkewe,kamkomoa aaaah hapana aisee Leah samehe huyu mtu harafu tupilia mbali aendelea Na safari .
Mungu mwema,usichoke kumwomba,kumtolea zaka atakupa mtu aliyesahihi,mtu atakayefuta machozi yako.
Nimependa ushauri wako nao..naona uwepo wako katika wakati huu mgumu..naamini unaweza kuwa rafiki mzuri kwangu
 
Hakika huwez kuwa unafanya kazi ya kuajiriwa na kusoma tena masters kwa wakati mmoja halafu uwe na uwezo wa kuwajibika ipasavyo kwenye ndoa. Ninachokiona hapo ni kwamba ulikuwa busy sana na majukumu ya kazi na shule, kiasi kwamba majukumu ya nyumbani ulimwachia mdogo wako. hapo ndipo kwenye tatizo. Mumeo ana kesi ya kujibu, mdogo wako ana kesi ya kujibu, lakini na wewe pia kama mke una kesi ya kujibu tena kubwa maana kwa namna moja au nyingine wewe umetengeneza mazingira ya hili tatizo kutokea. Uamuzi upo mikononi mwako, lakini hakika umeibomoa ndoa yako kwa mikono yako mwenyewe.
Kwa upande fulani umeongea ukweli

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
Pole Dada Leah. Kwanza ninakusifu umahiri wako wa kutokupanic na kutulia siku uliposikia wakiongea pamoja. Kwa maoni yangu wewe ni mke mwenye busara sana kwa jinsi ulivyochukulia mambo. Kwa sasa ulivyofanya ni vizuri. Kwa ushauri wangu chunguza kwanza wamekwenda wapi. Kama wamekwenda kuishi pamoja kwa sasa basi wape uhuru uendelee na maisha yako. Lakini kama mdogo wako amekwenda kukaa na wazazi au anaishi sehemu tofauti basi tafakari na umsamehe mme wako. Kama ulivyosikia wanaume ni wadhaifu na inawezekana mdogo wako ndiye aliyeanza mambo haya ulipokuwa unamwaacha na mumeo. Ninakutakia kila la heri na mungu akusaidie katika kufikia uamuzi wako.
Asante mercycity , lkn siwezi tena mpa chance nyingine ya kuniumiza huyu mwanaume..Nina malengo mengi maishani mwangu..sitaki kuishia kwenye magonjwa yanayoletwa na stress
 
Follow your heart. Kama unaweza kumusamehe, ni vizuri tu. Kama unaona huwezi, no way out mpe go ahead. Zaidi mshirikishe Mungu kwenye hayo maamuzi yako.
 
kaka alitaka asome kwanza ndio azae ndoa ya nini?? angesoma hadi akamaliza madarasa yote kisha arudi kwenye ndoa ili akikaa ajue ni kugegedwa na kuzaa, minyodo ya kusoma imemtumbukia nyongo.
Hivi kumbe kusoma ni nyodo? Baadhi ya wanaume ni watu wa ajabu sana
 
Aisee haya ndio matatizo ya wasomi et nilikataa kuzaa mpaka niwe na mastars imagen mwanaume akusubili umalize masomo ndo umzalie wakati amesha kuoa umpe anachotaka sasa we endelea na PhD yy akae na mke wake walee familia yao
 
Asante mercycity , lkn siwezi tena mpa chance nyingine ya kuniumiza huyu mwanaume..Nina malengo mengi maishani mwangu..sitaki kuishia kwenye magonjwa yanayoletwa na stress
Dada Leah2 wewe ndio muamuzi wa mwisho hata tukikupa ushauri na nakuomba ufikirie kwa dhati kabla ya maamuzi yako ya mwisho. Alichokifanya mumeo na mdogo wako sio kitu kizuri kwakweli. lakini wasamehe ili usiwe na kinyongo moyoni mwako kwani kinyongo huondoa furaha na kuleta chuki. Pia nampa hongera mdogo wako kuwa mkweli kwako japo ukweli wake umekuja baada ya kutenda kosa. nadhani anastahiki msamaha ila muweke mbali na ndoa yako yeyote ile kwenye maisha yako, lakini endeleza udugu sio vizuri kuisusia damu yako. Kuhusu mumeo wewe ndio unamjua vyema wapi anakufurahisha na wapi anakukwaza. kama utaamua kuendelea nae kuweni wawazi kwenye maisha yenu na muambiane kila jema na baya ili msije kugombana kwenye ndoa yenu.
 
Pole sana!! I can feel your pain.

Wakati huu unamhitaji Mola zaidi ya mwana Adam yoyote, Sali kila mara, muombe Muumba wako akupe wepesi wa kusamehe maana najua ni ngumu sana. Kamwe husijilaumu wala husijute kwa makosa ya mumeo na mdogo wako kumbuka "kila nafsi itabeba mzigo wake yenyewe", waache wahangaike na dhambi yao nawa uchafu wao katika nafsi yako, najua ni ngumu ila inawezekana!

Husiogope kuanza upya, huna makosa na Mola pekee ndie mpangaji wa kila jambo, sisi binaadam ni watekelezaji tu wa mipango yake huwezi kujua kwanini ndani ya hiyo dhambi atazaliwa kiumbe hasiye na hatia, Mshukuru Mola kwa kila jambo ila kumbuka utakufa na kuzikwa peke yako!!

Pole sana.
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
Pole sana dada, pia nikusifu unahekima na uvumilivu wa Hali ya juu, ingekuwa mim yaani Ile nimesikia tu kasheshe ingeanzia hapo hapo ningewafanya kitu ambacho hakuna kati yao angesahau. Leah nakushauri huyo si mume ni lifisi vizia mizogo kaanalo mbali kbsa, mtu asikudanganye ndoa pasipo uaminifu si ndoa ni majanga, maradhi,stress na kupotezea muda, mshukuru Mungu hujazaa nae. Kuanzia Leo waambie huwahitaji wachukue time zao, hii mijianaume isiyejitambua inayolazimisha eti umsamehe mrudiane ipuuze na tupilia kule ushauri wao wa kimfumo dume, songa mbele mama..piga kitabu mengine yatajipanga mbele kwa mbele. Na pia nakushauri acha kulia vaa ujasiri, endelea kusoma usije feli bure.
 
Pole sana dada, pia nikusifu unahekima na uvumilivu wa Hali ya juu, ingekuwa mim yaani Ile nimesikia tu kasheshe ingeanzia hapo hapo ningewafanya kitu ambacho hakuna kati yao angesahau. Leah nakushauri huyo si mume ni lifisi vizia mizogo kaanalo mbali kbsa, mtu asikudanganye ndoa pasipo uaminifu si ndoa ni majanga, maradhi,stress na kupotezea muda, mshukuru Mungu hujazaa nae. Kuanzia Leo waambie huwahitaji wachukue time zao, hii mijianaume isiyejitambua inayolazimisha eti umsamehe mrudiane ipuuze na tupilia kule ushauri wao wa kimfumo dume, songa mbele mama..piga kitabu mengine yatajipanga mbele kwa mbele. Na pia nakushauri acha kulia vaa ujasiri, endelea kusoma usije feli bure.
Acha kumpotosha mdada wawatu, inaonekana nawewe unatabia za kifedhuri kama mjinga mwenzio
Dada @#leah2 sadaka pekee unayoweza mpa mumeo ni MSAMAHA. Rudisha picha nyuma uone ni kwa jinsi gani umekuwa ukimkosea mumeo...mmekoseana mangapi na kusameheana mangapi?! Kiimani hakuna dhambi kubwa na ndogo. Hukumu ya mzinifu na mlevi wa viroba ni moja kwa Mola wetu. Na kwaatubuye na kujutia dhambi zake atasamehewa.

Leah, paka moyo wako grease. Upake mafuta ya karafuu na mzeituni. Mfukize mumeo kwa moshi wa MSAMAHA. Labda nikwambie kitu my dear...yupo aliyafanya ya mumeo. Akajutia na mkewe akamsamehe. Mume hakuwa na amani. Hakutamani kumuona mtoto wake aliyezaa na mdogo wa mkewe.

Siku zikakimbia. Maisha yanasonga. Mapenzi yakarejea. Miaka ikakatika. Siku moja yule mtoto akawa anaenda kisimani huko kijijini kuchota maji. Ooh gosh..akatumbukia kisimani na kufa. Ilihuzunusha sana maana ni mwanadamu kafariki. Lakini chaajabu baba mtoto alifurahi sana na akawa na amani maradufu.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba..msamaha una faida. Gorgivenees pays. Je wewe utaishi milele bila kumkosea mtu? Hutatenda dhambi na kuomba upewe nafasi ya kusamehewa?! Je wewe umekamilika? yes, I do sympathise with you my dear... But think twice. Things happens and Never say Never. Cheers!!

Goodluck Mshana
 
Pole sana mami....Mungu akupe faraja na wepesi katika jambo hili mumeo amekubandika kovu kubwa ndani ya moyo wako....muombe Muumba wako wakujaalie kufikia maamuzi sahihi
Mwenzangu we acha tu, yaani najaribu kuvaa uhusika halafu nasikia hasira..yaani wangenitambua nadhan saa hizi ningekuwa jela zamaniii
 
Bora huyu aliyejutia kosa lake kama umemsoma vizuri Leah mmewe haoneshi kujutia kosa lake Na wala haombi msamaha Bali alimwambia yaishe tu simple tu kiasi hicho????
Ni bora hata angeonyesha kujutia labda angesamehewa,angekua mtu mwingine hiki kipindi alicho mpisha mkewe ndo kingekua kipindi kizuri cha kumlilia mkewe amsamehe kwa msg,kutuma watu Na calls kuomba asamehewe
Lakini mwanaume wapi kakauka utafikiri alichokifanya ni kizuri,kua kamwuweza mkewe,kamkomoa aaaah hapana aisee Leah samehe huyu mtu harafu tupilia mbali aendelea Na safari .
Mungu mwema,usichoke kumwomba,kumtolea zaka atakupa mtu aliyesahihi,mtu atakayefuta machozi yako.
Upo sahihi nao
 
Back
Top Bottom