Nakuunga mkonoBinafsi sitaweza kuishi nae tena nilitakupata justifications ya maamuzi yangu ndo maana nikaomba ushauri humu ndani
Watu wanaongea tu kirahisi nisamehe lkn hawajaribu kuvaa uhusika waone ilivyo ngumu
Wanasemaga shetani kanipitia hatari kweli hii huu ugomvi hauishagi.Haya mambo haya yapo sana ila watu hawajifunzi.
Acheni hizo. Kama alikuwa na haja sana na mtoto huyo jamaa angemwambia shemeji yake wakatoe mimba?si walikubaliana mke akasome?alikosa wanawake huko nje mpaka akapige shemeji?haya mambo mnayasema tu hapa kirahisi lakini hakuna justification ya cheating mkuu. Afu unajua mtu anayecheat iwe mwanamke au mwanamme afu anapiga dry huyo ni muuaji koz anaweza leta ugonjwa ndani. Duuh unaloweka kabisa dry hahahaha.Labda mumeo alikuwa anahamu sana na Mtoto ila wewe ukaweka maslahi yako ya kuto kubeba mimba yake mpaka umalize masomo unaweza kuachana nae leo ila elewa kuwa siku zote ukishakuwa ndiwe mwenye maamuzi ndani ya ndoa vitu kama hivyo tena na zaidi ya hivyo hutokea ushauri wangu ni kuwa rudisha moyo wako kwa mumeo najua yeye ni binadamu hatarudia tena huo ujinga mpaka hapo ameshajifunza vya kutosha.
Nimeamua kuquote ili uuone mchango wangu. Nionavyo Mimi jambo hili in gumu sana kuamua kwa utashi wa kibinadamu. Sifahamu imani yako au dini yako ni IPI.Habari za asubuhi wanajamvi,
Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.
Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.
Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.
Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.
Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.
Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.
Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.
Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.
Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.
Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.
Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.
Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..
Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.
Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.
Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.
Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..
Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.
Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.
Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.
Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?
Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.
Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.
Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.
Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.
Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..
Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.
Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,
Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.
Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..
Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.
Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.
Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.
Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..
Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.
Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.
Wameondoka na sijui walipo kwenda.
Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.
Najiuliza heshima yangu iko wapi?
Jamii inanionaje?
Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?
Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.
Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.
Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.
Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
Imeandikwa samehe saba mara sabini, sisi wanaume ni mbwa.
Huna akili,unaweza kuolewa mpango huo ukiwepo,haimaanishi usiendelee za ratiba yako,kwanini alimkubalia kama alikua anataka mtoto kwanza?pili huyo mwanaume sio malaika anamapungufu inamaana ambapo hamtoshelezi nae akalalwe nje?nae ambebee mimba mtu mwingine?over all women kaona mdogo wake?umalaya huoAisee haya ndio matatizo ya wasomi et nilikataa kuzaa mpaka niwe na mastars imagen mwanaume akusubili umalize masomo ndo umzalie wakati amesha kuoa umpe anachotaka sasa we endelea na PhD yy akae na mke wake walee familia yao
Hata sio kumpotosha angekua amefanyiwa dada zako usinge jaa povu hapa?au kwa sababu kafanyiwa mwanmke usiemjua sura?[emoji57]Acha kumpotosha mdada wawatu, inaonekana nawewe unatabia za kifedhuri kama mjinga mwenzio
Ningefanya mimi nikajirudi angenisamehe?vitu vingine kupima ni vizuri kabla ya kuchukulia poa hili laweza kumkuta yeyotenatamani wangekuwa wameshaitoa hyo mimba tayar sema wewe umewahi kuwaita wazazi[emoji1] [emoji15] halafu ndo nikushauri kama mmeo kajirudi na kukiri kwelikweli umsamehe na uishi naye kwa akili.
Kaka kuzaa na kufanya tendo la ndoa ni vitu viwili tofauti,huyu hakunyimwa tendo ila ulafi wake ndo umemfanya afanye hivyo,wengi wanaolewa hawana bikira na hawana watoto,kama kutia mtu ndo kuzaa basi masingle mother lisingekua shida kwenu maana wangezaa kil walipotiwaPole sana Dada kwa yaliokukuta. Ni kweli dhambi hii ni kubwa mno na ni vigumu kuibeba. Binafsi ninaamini kuwa mapenzi ni uaminifu, na uaminifu unapopotea basi hakuna haja ya kupenda tena. Assume uwasamehe afu itokee siku uwakute wanaongea hata maongezi ya kawaida tu, ni dhahiri utaumia saana. Nakushauri upige chini hiyo ndoa uanze upya.
Jambo lingine Dada angu, ulitengeneza mazingira mwenyewe ya dhambi hiyo kutendeka. Kama hukutaka kuzaa kabla ya kumaliza masomo yako, kwanini uliolewa kabla ya kumaliza masomo????
Ulimkaribisha shetani ww mwenyewe ndani ya nyumba yako na Leo amekuzodoa.
Naomba niwashauri wanawake wote mliobaki, kama hutaki kuzaa usifunge ndoa. Narudia tena kukupa pole.
Ferguson
Unadhan ni rahisi hivyo? By the way ndoa ni ya thamani kama itathamini na wahusika wote ikiwa ni pamoja na kutunza maagano,vingenevyo inakuwa ni ndoanonatamani wangekuwa wameshaitoa hyo mimba tayar sema wewe umewahi kuwaita wazazi[emoji1] [emoji15] halafu ndo nikushauri kama mmeo kajirudi na kukiri kwelikweli umsamehe na uishi naye kwa akili.
Wanaume wa Dasalamuu haoo.....MARIOFunzo kwa mwanaume yeyote mwiko kuishi kwa nyumba iyoijengamkeo/anayolipia mkeo/aliyopangishiwa na ofisi anayofanyia kazi mkeo.Likitokea lolote utafukuzwa nyumbani kama alivyofukuzwa mme wa Leah2 mbele ya baba na mama yake.
Wewe Gojaga Nize acha kupotosha maandiko, Yesu na Stefano walifanya vile kutetea imani na wala si kuitetea dhambi. Sote tumemshauri asamehe na asiwe na kinyongo nao lakn asikubali tena kuendelea na maisha ya ndoa ya maigizo, achane nao aendelee na ratiba zake, biblia imehalalisha kutenga pale inapotokea uasherati je kilichofanywa na mume wa leah2 si zaidi ya uasherati? Huyo mume wa leah2 na namuona kama kahaba na Malaya tu ni wa kukimbia kama ukoma. Leah Dada angu huo ukurasa ufunge na anza upya, usilie tena zinatosha sasa ni wakati wa kujifuta machozi na kuchukua hatua.Nimeamua kuquote ili uuone mchango wangu. Nionavyo Mimi jambo hili in gumu sana kuamua kwa utashi wa kibinadamu. Sifahamu imani yako au dini yako ni IPI.
Yesu akasema namna hii haiwezekani isipokuwa kwa kufunga na kuomba.
Kunawakati ili upate best solution ya nini kifanyike, jifanye mjinga, tubu kwa ajili ya kosa lililofanyika kwa machozi na kwa kumaanisha ikiwezekana kwa kufunga na kuomba. Beba hilo tatizo kana kwamba wewe ndio umelitenda na sio hao watu unaowaona.
Kumbuka nimesema jambo hili in zito ukitumia akili zako. Yesu akiwa msalabani alisema, Baba naomba uwasamehe hawa watu maana hawajui walitendalo, lakini mapenzi ya Mungu yatimizwe.
Stephano wakati anapigwa mawe, alilia akiomba akisema "Baba naomba usiwahesabie hukumu wala hatia watu hawa"
Mungu anajibu Dada yangu ukichukua mzigo na kuomba kwa kumaanisha. Usisahahu kusamehe, katika kusamehe utapata nini cha kufanya.
Kuna watu walibakwa na wazazi wao katika stage Fulani za maisha yao, lakini ilibidi wasamehe kwasababu katika hali ya kukaa bila kuachilia, kuna vitu vingi unavifunga, lakini pia unazuia utendaji wa Mungu katika maisha yako kwasababu unajiona una haki na hautaki kusamehe.
Kusamehe haimaanishi kunaiondoa hatia ya mkosaji mbele za Mungu la Bali unaiondoa hatia hii mikononi mwako Ila Mungu ndio awe mwamuzi.
Mungu akusaidie.