Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Samahani au wewe ndo mme wake...? Mbona unashadadia sana kuwa mwanamke ndo mwenye makosa? Kiukweli inawezekana mwanamke akawa amechangia kwa kiasi fulani sababu hakuna aliyekamilika ila halikuwa jambo jema mwanaume kumpa mimba shemeji yake....
Kuna baadhi ya wanaume ni chefu usipote muda kujibishana nao pengine baada ya kujua Bibi Dada anamalizia masters roho ya wivu imemkaba hana lolote kakomalia kweli ingekua ndo mkewe katiwa mimba Na kaka yake sijui angesemaje pfyuuu
 
Pole sana mami....Mungu akupe faraja na wepesi katika jambo hili mumeo amekubandika kovu kubwa ndani ya moyo wako....muombe Muumba wako wakujaalie kufikia maamuzi sahihi
 
Dada @#leah2 sadaka pekee unayoweza mpa mumeo ni MSAMAHA. Rudisha picha nyuma uone ni kwa jinsi gani umekuwa ukimkosea mumeo...mmekoseana mangapi na kusameheana mangapi?! Kiimani hakuna dhambi kubwa na ndogo. Hukumu ya mzinifu na mlevi wa viroba ni moja kwa Mola wetu. Na kwaatubuye na kujutia dhambi zake atasamehewa.

Leah, paka moyo wako grease. Upake mafuta ya karafuu na mzeituni. Mfukize mumeo kwa moshi wa MSAMAHA. Labda nikwambie kitu my dear...yupo aliyafanya ya mumeo. Akajutia na mkewe akamsamehe. Mume hakuwa na amani. Hakutamani kumuona mtoto wake aliyezaa na mdogo wa mkewe.

Siku zikakimbia. Maisha yanasonga. Mapenzi yakarejea. Miaka ikakatika. Siku moja yule mtoto akawa anaenda kisimani huko kijijini kuchota maji. Ooh gosh..akatumbukia kisimani na kufa. Ilihuzunusha sana maana ni mwanadamu kafariki. Lakini chaajabu baba mtoto alifurahi sana na akawa na amani maradufu.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba..msamaha una faida. Gorgivenees pays. Je wewe utaishi milele bila kumkosea mtu? Hutatenda dhambi na kuomba upewe nafasi ya kusamehewa?! Je wewe umekamilika? yes, I do sympathise with you my dear... But think twice. Things happens and Never say Never. Cheers!!

Goodluck Mshana
Bora huyu aliyejutia kosa lake kama umemsoma vizuri Leah mmewe haoneshi kujutia kosa lake Na wala haombi msamaha Bali alimwambia yaishe tu simple tu kiasi hicho????
Ni bora hata angeonyesha kujutia labda angesamehewa,angekua mtu mwingine hiki kipindi alicho mpisha mkewe ndo kingekua kipindi kizuri cha kumlilia mkewe amsamehe kwa msg,kutuma watu Na calls kuomba asamehewe
Lakini mwanaume wapi kakauka utafikiri alichokifanya ni kizuri,kua kamwuweza mkewe,kamkomoa aaaah hapana aisee Leah samehe huyu mtu harafu tupilia mbali aendelea Na safari .
Mungu mwema,usichoke kumwomba,kumtolea zaka atakupa mtu aliyesahihi,mtu atakayefuta machozi yako.
 
jana kulikuwa mada hapa inayosema MKE WANGU ANAJALI KAZI KULIKO FAMILIA wadada wengi walikandia jamani hata kama mumeo amekuita njoo angalau wkend njoo basi hata nikuone tu wewe hutaki sasa hiyo hali inakwenda mpaka mtu anajiuliza kwa nini niumizwe hisia zangu!mbona mke wangu anijali matokeo yake ndio haya akina dada ukiitwa nenda mwisho pole leah
 
Hakika huwez kuwa unafanya kazi ya kuajiriwa na kusoma tena masters kwa wakati mmoja halafu uwe na uwezo wa kuwajibika ipasavyo kwenye ndoa. Ninachokiona hapo ni kwamba ulikuwa busy sana na majukumu ya kazi na shule, kiasi kwamba majukumu ya nyumbani ulimwachia mdogo wako. hapo ndipo kwenye tatizo. Mumeo ana kesi ya kujibu, mdogo wako ana kesi ya kujibu, lakini na wewe pia kama mke una kesi ya kujibu tena kubwa maana kwa namna moja au nyingine wewe umetengeneza mazingira ya hili tatizo kutokea. Uamuzi upo mikononi mwako, lakini hakika umeibomoa ndoa yako kwa mikono yako mwenyewe.
 
Huu ushauri ni rahisi sana kuutoa kama Jambo halijakufika eti Yule mtoto aje Hapo seriously? Wanaume bana.
Mara nyingi ushauri wa kweli huwa ni mgumu ktk akili ya mshauriwa, na ndo maana hata mawazo ya wazazi bado kwako ni magumu, matatizo yeyote ktk maisha yanatikiwa yapate suluhsho ambalo haliharibu kilichopo bali kukijenga! Nionavo mimi, kumfukuza mumeo pamoja n mdogo wako nyumbani kwako, umekosea" ona sasa hujui wako wapi na wanafanya nn! Ki ukweeli ni kama umeongeza tatizo, jikubali kama mwanamke, rudi kwenye mstari "upande wa wazazi" na umsamehe mumeo maisha yaendelee, hakuna maisha yasiokuwa na mitihani, wanawake ni vivutio kwa wanaume bila kujali ni mdogo wako au ni shangzi! Na wanume ni dhaifu kwa wanawake bila kujali ni jenerali w jeshi au mkulima! Usipomlinda watamteka tu! Ki msingi hili swala lako limenikumbusha miaka kadhaa iliopita alikuja mdogo wake na wife, alitakalo dem mwanaume hachomoi" lakini tuliyamaliza. Kuwa makini na wadogo zako wa kike, ni sawasawa na mashoga zako tu! Kwani nao ni wanawake, mpigie mumeo umuokoe huko alipotekwa" usinielewe vibaya, nipo dodoma carnival nimetekwa ntaenda home baadae saana"
 
Pole sana sista but vipi kuhusu mdogo wako nini huruma yako kwake? REMEMBER DAMU NI NZITO KULIKO MAJI.
 
Huu ulimwengu ni fully shida, huwezi tatua tatizo kwa kulikimbia. Wanaume wote by nature Ni polygamists, uvumilivu tu ndio unatutofautisha.

Samehe piga maisha, mm bibi zangu waliolewa na mume 1 poa kbs mpk leo wanafurahia penz la mume wao
 
Achana nao! Endelalea na maisha yako... Hiyo ni dosari kubwa na wewe utakuwa kama house girl tu pindi mtoto atakapozaliwa... Anza upya... Kama ni mme utapata mwingine
 
Hili swala lako ni gumu sana kwangu kutoa neno. Kama ni mcha MUNGU tafadhali mpe Mwenyezi MUNGU nafasi akuoneshe njia; Yeye siku zote yupo sahihi wala hakosei. Funga na kuomba kwa masiku yote unayosubiri muongozo kutoka kwa Mwenyezi MUNGU..
 
Pole sana ila ujue ndo mambo ya dunia hayo maana dunia haina huruma; ushauri usivunje ndoa kwaajili ya hilo kosa, katereza atainuka na kusimama imara tena ebu jaribu kumsamehee, amekiri kosa msamehe chukua mda kutafakari maamuzi yako unayotaka kuchukua fikiria mara 2 angalia mbele na nyuma chukua mazuri yake sahau mabaya yake, Mungu atakupa hekima na maamuzi mazuri zaidi : usivunje ndoa yako kwaajili ya hili.
 
How old are you?
Partly kabla ya kuanza kumlaumu mumeo nitakulaumu na wewe.

[*]Hilo la kuchelewa kumzalia mumeo mtoto. Inaweza kuwa lilikuwa jambo lako tuu na namna alivyokubali inaweza kuwa kutokana na sababu zako ila je?

Wanaume ni wadhaifu being a man I know this, na wanahitaji kufuatiliwa kwa ukaribu sana hasa kwenye mambo kama haya yanayohusisha hisia.

Bottom line: Fuata ushauri wa wazazi, dogo arudi kijijini ajifungue mtoto, mtoto akiwa mkubwa, aje hapo nyumbani, kaeni kikao cha kifamilia mdogo wako na mumeo waombe msamaha kwa jambo lililotokea na mzungumzie utaratibu wa matunzo ya mtoto. Life goes on. Ukishindwa hilo. File for a divorce ukaolewe na mtu atakayekusubiria umalize shule (tena Masters, unga na PHd kabisa) ndio ukubali kumzalia mtoto.

Nimenukuu machache ya "Don Mangi", ambayo naamini yanawakilisha mawazo ya dunia tuliyomo ya mfumo dume.

Lakini la msingi ni jinsi wawili walivyokutana, wakakubaliana kuishi kama mme na mke. Hili wengi wetu huwa tunalisahau pale ambapo ndoa inapoanza kwenda mrama.

Ustawi wa ndoa ni jukumu la wote wawili, naamini. Mme atatembea na mfanyakazi wa ndani, mke vivyo hivyo. Huyu atatembea na mdogo mtu, yule vivo hivyo. Siri inabaki jinsi hao wawili walivyoanzana na wanavyoishi.

Leah 2 hatoweza kutueleza kwa undani maisha yake ya unyumba na mmewe. Wengi hili la kuridhishana unyumba majumbani mwetu hatujadiliana na wenzi wetu tukiisha oana.

Leah 2: fikiria kwa undani mchango wako katika kufanikisha mahusiano ya mdogo wako na mmeo. Hii itakusaidia kufanya uamuzi sahihi kwa faida yako mwenyewe kwenye maisha ya ndoa na pia kwa familia.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Hatauelewa kwa kipi mkuuu uuupsss Kwan ukisamehee haweZ kuhama mkoa???? Mm namaanisha ahakikishe anawasamehe na aondoke kuanza maisha mapya .sio kuanza maisha wakati bdo Una vifungo vya kuwasamehee watu Mungu hawez kumbariki kwa Hilo.
Katika ubora wako mama,nimeupenda huu Uzi watu wameutendea haki. Imenikumbusha MMU ya enzi zile katika ubora
 
Dada yangu polepole tena sana kwa matatizo yalikukuta ukisikia duniani kuna mitihani ya maisha ndio hiyo cha msingi fanya jambo lifuatalo

Kwanza Jiulize katika nafsi yako kuwa wanadamu hapa duniani wanafanya madhambi kiasi gani mbele ya Mola wao wapo wanaojiuza tena kinyume na maumbile, wapo wanauwa wenzao imma kwa ujambazi ,uchawi au kutoa mimba lakin dhambi zote hizi mtu akitubu na kuacha Mwenyezi Mungu humsamehe iweje Mimi na wewe pindi tunapofaniwa makosa makubwa kama haya ukiwa ni mtu wa kiiman utanielewa vizuri

Kisha Ukisema usimsamehe utengane naye uyo mumeo

Angalia Faida na Hasara utazopata kuwa nje ya Ndoa Tena naomba ufikirie vizuri ukiwa umetulia bila Shaka utaona kuvumilia kidonda hiki huenda kukawa na nafuu kuliko kupata kidonda chengine cha kutoka nje na Ndoa na kukosa Mume

Tafadhali Dada Angalia sana na ufanye maamuzi sahihi siku hizi waume wenyewe wapo wapi wakuoa?

Chakufanya Mrudishe mdogo wako kwenu Kisha Endelea maisha na Mumeo naamini baada ya mwezi tu utasahau yaliyotokea baina yenu!!!
 
Back
Top Bottom