Ndiyo, lakini mtu hawezi kuachwa kwa kufoji vyeti. Tatizo sio kufeli, tatizo ni udanganyifu, vilaza wanajifanya hawaelewi utofauti huu.
Kuua tajiri ukamuibia pesa na kuzigawa kwa maskini haikusafishi, wewe ni mhalifu tu, sawa na aliyeua tajiri kwa manufaa yake. Ndiyo maana ya the end doesn't justify the means. Hata kama mtu anapiga kazi, swala la udanganyifu level ile ni kosa kubwa lazima tupige kelele.
Alafu usikae unasema mtu hapimwi kwa vyeti, we utataka mtu awe profesa huku alipata Div IV? Au GPA second class? Tuache utani, kuna muda performance ya darasani ina maana kubwa sana.