Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,610
- 6,391
Kanuni za asili zinafuata sheria ya asili isiyokosea the law that doesn't err" . Hakuna kinachotokea bila sababu chanzi kwa sababu katika asili kila kitu ni sababu na matokeo. Mtu ni zao la sababu na matokeo yake.
Siyo lazima ulipwe wema kwa sababu ya matendo yako mema uyatendayo leo kulingana na kanuni hii. Unaweza ukatenda wema na ukalipwa mabaya. Kujua au kutokujua sababu hakuathiri utendaji wa sheria za asili kwa kuwa utendaji wake wote inatawaliwa na sababu na matokeo yake.
Kanuni hii huutangaza mwisho wa jambo mwanzoni kwa sababu haifungwi na wakati wala mipaka ya iifizikali. Inamtafsiri mtu kama nguvu ileile moja. Hivyo nguvu hiyo hubeba kila kitu cha kila mtu. Kuzaliwa na kufa siyo ni mipaka uwili endelevu wa kitu kilekile katika mawanda tofauti "sustainable dichotomy of the same thing".
Kupitia nguvu moja tu jamii kubwa ya watu leo imebeba matokeo yake. Tunakuja katika ulimwengu huu wa kifizikali tukiwa tayari na malipo/matokeo ya kila kitu chetu. Mazingira haya ndiyo yanayotanua uwanja wa unajimu na matumizi ya lugha ya asili ya ulimwengu ambayo ni namba (numerolojia).
Kwa kuwa mtu ni nguvu ni dhahiri kuwa kitu cha kuboreshwa ni utendaji wa nguvu hizo ili kutenda katika mawanda ya juu " to enhance our energy" siyo kukimbizana na muda tu ambao ni jambo la kufikirika lenye ukomo na mipaka katika ulimwengu wa vitu na muda "spacio-temporal / space-time world".
Kujifungia katika ulimwengu wa vitu na muda ni gereza la utumwa unatumiza zaidi. Tunaishi katika jamii ambayo nikama kila mtu ana vidoda mwili mzima na akiguswa kidogo tu anaumia. Ile vita ya asili ya kila mtu dhidi ya kila mtu "war of all against all" ni kama inatokana na sababu ya kila mtu kumuumiza kila mtu.
Tatizo kubwa la kileo ni kuwa kila mtu anaangalia anavyoumia yeye na kuona anayemuumiza ni mtu mwingine. Mtu anafundishwa kuwa anayemuumiza ni mtu mwingine na siyo utendaji wa nguvu zake. Hatuboreshi nguvu zetu - utu wetu kufanya kazi katika mawanda ya juu ila tunajikita kusukuma lawama na kuacha kujitawala.
Familia, vikundi mbalimbali na vyama vinaungana vikijiaminisha kuwa anayewaumiza ni wengine (familia, vikundi au vyama vingine) na siyo wao. Jamii inajiondolea uwajibikaji binafsi na kujifunza badala yake ni kizazi cha lawama. Ukweli ni kuwa tunajiumiza zaidi wenyewe na hatutaki kukubali.
Baadhi ya wahubiri wakubwa wa imani mbalimbali wamepanda elimu ya watu kuchukiana kwa kuwaaminisha sana kuwa adui wa mtu ni mtu mwingine huku wakiacha swali la uwajibikaji binafsi pembeni. Vipi kama adui wa mtu akawa ni mtazamo wake mwenyewe juu yake na wengine? Mtu wa aina hii akimexeshwa "dogma" ya kuchukia wengine unafikiri jamii itabeba mzigo gani?
Safari sahihi ya kujiponya haipo nje yetu ila unaanzia ndani yetu. Tunahitaji kujitibu ndani kwanza "inner engineering".