Mtu apimwe kwa utendaji siyo makaratasi

Ndiyo, lakini mtu hawezi kuachwa kwa kufoji vyeti. Tatizo sio kufeli, tatizo ni udanganyifu, vilaza wanajifanya hawaelewi utofauti huu.

Kuua tajiri ukamuibia pesa na kuzigawa kwa maskini haikusafishi, wewe ni mhalifu tu, sawa na aliyeua tajiri kwa manufaa yake. Ndiyo maana ya the end doesn't justify the means. Hata kama mtu anapiga kazi, swala la udanganyifu level ile ni kosa kubwa lazima tupige kelele.

Alafu usikae unasema mtu hapimwi kwa vyeti, we utataka mtu awe profesa huku alipata Div IV? Au GPA second class? Tuache utani, kuna muda performance ya darasani ina maana kubwa sana.
 
Nadhan ni wakati sasa kwa aliyekuja na wazo la kuhakiki vyeti achukuliwe hatua kwa kuliingizia taifa hasara na kutia hofu kwa kwa watumishi pasipo sababu za msingi kwa kuwa dhana ya cheti sio hoja ya msingi katika arena ya awamu ya tano.

Serikali iwarudishe wale wote waliofukuzwa au waliokimbia vituo vyao vya kazi kwa kutokuwa na vyeti halali vya kitaaluma kwa kuwa vyeti hivo sio tatizo kwao hata wangekuwa na sufuri lakin tutaangalia kama wana uwezo binafsi wa kutekeleza majukumu yao na sio vyeti tena.

Mwisho. Tusimamie yale tuliyo na uwezo wa kuyatekeleza.
 
Mambo
mambo ya GPA CV hayana tija kwa taifa. Vinginevyo tungekuwa mbali sana. Nchi hii inahitaji zaidi watu wenye maamuzi na kutekeleza mara moja bila kukawia.

Hayo ni maneno ya mtu ambaye hajasoma chochote, sawa na maneno ya maskini kukaa anajifariji kua wote kaburi ni moja huku ukweli uko wazi.

Mtu yeyote aliyeenda shule akachukukia serious elimu yake anajua umuhimu wa mambo yanayofundishwa shuleni. Ukienda kwa kukurupuka utaishia kuingia loss, una deal na watu smart utafunguliwa kesi uishie kulipa mabilioni kwa move moja tu ya kijinga. Mnajifanya hamuoni swala la IPTL watu wanalipwa 300million kila siku?

Usicheze na watu wanaotumia ubongo na wewe unatumia moyo, utafeli tu, chukulieni na mfano wa Zimbabwe, yule mzee anajifanya akisema yanatekelezwa bila pingamizi, oneni hali yao sasa, kununua mkate kwa bilioni. Watu ambao hamjasoma tafadhali msiwe mnatoa comment kuhusu elimu maana hamkuipata hamjui umuhimu wake zaidi ya story za vijiwezi mlizolishwa. Hakuna kitu kitaiokoa Tanzania kama elimu.
 
Huu ni ulimwwengu wa ACTIONS. Siyo maneno. Mtu apimwe kwa uwajibikaji siyo cv. Mambo ya cv yamepitwa na wakati..Tubadilike.
Mkuu uko serious au unatania? Hebu sikiliza, kuna nurse mmoja katika hospitali kubwa tu hapa Dar alikuwa anafanya kazi labor ward, kiukweli alikuwa ni tegemeo kubwa sana kutokana na ufanisi wa hali ya juu katika kusaidia wamama wajawazito kujifungua. Uhakiki wa vyeti ulipopita akagundulika hakuwa na vyeti vya kumuwezesha kufanya ile kazi, amepigwa chini na sasa hivi ni jobless hana kazi na hana kipato japo alisaidia sana kuzalisha wamamawajawazito pale hospitali. My point ni hii, msiwe na double standard katika kudeal na hivi vitu kama kuna mahali mtu amekosea awajibike kulingana na makosa yake sio mnakuja kulialia hapa inapokula kwenu. Hii habari ya vyeti imekosesha ajira watu wengi sana ambao walikuwa wanaumuhimu sana jwa jamii kuliko hao unaojaribu kuwatetea.
 
Hapa kasi tu, weka mziki hatutaki maneno. Wenye vyeti kama ndo wanaoharibu akitokea mmoja hana cheti lakini akaonesha kutuvusha itabidi tukubali atuvushe. Kuna wakati wa knowledge na kuna wakati wa wisdom, ni vitu viwili tofauti na vinakidhi mahitaji mawili tofauti.

Alfajiri njema!
 
Hayo ni maneno ya mtu ambaye hajasoma chochote, sawa na maneno ya maskini kukaa anajifariji kua wote kaburi ni moja huku ukweli uko wazi.

Mtu yeyote aliyeenda shule akachukukia serious elimu yake anajua umuhimu wa mambo yanayofundishwa shuleni. Ukienda kwa kukurupuka utaishia kuingia loss, una deal na watu smart utafunguliwa kesi uishie kulipa mabilioni kwa move moja tu ya kijinga. Mnajifanya hamuoni swala la IPTL watu wanalipwa 300million kila siku?

Usicheze na watu wanaotumia ubongo na wewe unatumia moyo, utafeli tu, chukulieni na mfano wa Zimbabwe, yule mzee anajifanya akisema yanatekelezwa bila pingamizi, oneni hali yao sasa, kununua mkate kwa bilioni. Watu ambao hamjasoma tafadhali msiwe mnatoa comment kuhusu elimu maana hamkuipata hamjui umuhimu wake zaidi ya story za vijiwezi mlizolishwa. Hakuna kitu kitaiokoa Tanzania kama elimu.
Nimesoma. Nina MA/MASTERS MBILI.NA SASA NAFANYA PHD. IT IS OUT OF MY PILOT RESEARCH.
 
Hata madaktari,waalimu, mapolisi na watafiti wote wapimwe kwa actions bwana sio makaratasi..... Makaratasi ya kazi gani sasa... Yani hata wauguzi ni mwendo wa actions tu...... WTF citizens!!

Shangaa mtu anatumia makaratasi ya mwingine..... Ya nini sasa....

Na bado mnajisifu na elimu bure hadi kidato cha nne........ Actions mwanzo mwisho"kazi tu"....hata neno dakta tulitoe pale.

Only in TZ
 
Back
Top Bottom