SoC02 Mtihani wa darasa la saba kisiwe kipimo cha mwisho cha uwezo wa akili kwenye elimu

Stories of Change - 2022 Competition
Jul 21, 2022
11
3
Ninachukua wasaa huu kuzungumza na nyinyi ndugu zangu kupitia andiko hili, suala la kupima uelewa wa mtu katika elimu isiwe kwa mitihani hasa kwa elimu ya msingi ambayo Watoto bado wanakuwa na umri mdogo. Kwa hiyo wengi wao wanakuwa hawajatambua ni njia gani watumie katika kusoma ili kufanya vizuri kwenye masomo yao. Mfano Halisia ni mimi mwenyewe na hiki ndicho kilichotokea.

Mwaka 2002 nikiwa na umri wa miaka sita nilianza safari yangu ya elimu na nilianza moja kwa moja darasa la kwanza katika shule inayoitwa Kambarage iliyoko Karagwe mkoa wa Kagera. Darasa la kwanza mpaka darasa la tatu lilipita tukafika darasa la nne ambapo huwa ni darasa la mtihani wa Taifa. Tulifanya mitihani mingi ikiwemo mtihani wa kata, wilaya na mkoa kabla ya mtihani wa taifa, kwa ujumla mimi nilitimiza wajibu wakufanya mitihani sikuwa najali kuwa nitakuwa wa ngapi au nahitaji nifikishe wastani kiasi gani.

Punde si punde uliwadia wakati wa mtihani wa taifa na tulifanya mtihani tukafunga mapema shule na kwenda mapumziko tukiwa tunasubiri matokeo ya mtihani wa taifa. Mwezi wa 12 mwaka 2005 matokeo yalitoka na hapo nilijiua na kuanza kuelewa kidogo nini maana ya wastani. Namshukuru Mungu Pamoja na kuwa sikuwa nasoma sana nilifaulu kwa wastani wa kuchechemea. Niliendelea na masomo mpaka mwaka 2009 nilipoingia darasa la saba na hapo nilikuwa mtahiniwa tena. Shuleni walimu wetu walijitahidi sana kutupa mazoezi na mitihani ya kutosha kwa ajili ya kutuandaa na mtihani wa mwisho.

Mnamo tarehe mbili mwezi wa tisa mwaka 2009 tulifanya mtihani wa taifa na tukahitimu elimu ya msingi kwa furaha ikiambatana na mahafali. Baada ya miezi miwili kupita matokeo ya mtihani wa taifa yalitoka, na kubandikwa kwenye mbao za matangazo halmashauri ya wilaya. Hakika siku hii ni sku ambayo siwezi kuisahau kamwe katika Maisha yangu. Asubuhi na mapema sana nilisindikizwa na mdogo wangu wa kiume kwenda kuangalia matokeo tukiwa tumeagizwa na mama mzazi. Tuliondoka na kuelekea sehemu husika, wakati tunawasili pale, tulikuta watu wengi sana waliowahi kuangalia matokeo, wakiwemo watu wa darasa langu, na wengine walikuwa wakipongezana na kuambiana kila mmoja amechaguliwa shule gani.

Ghafla kundi moja la wavulana niliosoma nao waliokuwa pale waliponiona ,walikonyezana na kusema kwa sauti ya chini” yule binti mdogo wa darasa jina lake halipo, hajafaulu.” Nilijisikia vibaya sana baada ya kusikia maneno hayo. Lakini sikutaka kuonesha usoni kama nimesikia kwa sababu nilikuwa nimeambatana na mdogo wangu. Nilitembea kwa ujasiri mpaka kwenye mbao za matangazo na kuanza kutafuta jina langu ilihali nikijua halipo, niliangalia wenzangu wamechaguliwa shule gani na baada ya hapo nikamchukua mdogo wangu turudi nyumbani maana na yeye alitafuta jina langu hakuliona kabisa.

Wakati tunarejea nyumbani nilipanga na mdogo wangu tusimwambie mtu yeyote hata mama mzazi kuhusu suala hili Kusudi tusipoteze furaha ya mama sababu alikuwa anapenda nisome na nilikuwa mtoto wa kwanza katika familia. Sababu nyingine iliyotupa kiburi tusiseme kuna shule binafsi nilkuwa nimeshafanya mitihani na kupata nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari. Baada ya kuwasili nyumbani tulimwambia mama nimefaulu na tukaendelea na maandalizi ya kuanza kidato cha kwanza.

Nilipoanza kidato cha kwanza kwenye shule ya sekondari ya wasichana Hekima iliyoko Bukoba, Kagera nilikuwa nimeazimia kusoma kwa bidii sana. Bila kujali kuwa nimefeli darasa la saba ,nilijiona nimepata fursa ya dhahabu kwangu kujaribu tena katika masomo. Bahati nzuri tulivyoanza masomo tulikuwa na miezi mitatu ya “English Course” kwa ajili ya kutusaidia sisi tuliotoka shule za serikali. Darasa letu lilikuwa na wanafunzi wengi waliotoka shule binafsi, baada ya kugundua hilo nilianza kurudi nyuma kimawazo na kujiona nikiwa wa mwisho darasani. Niliamini kuwa sina uwezo wa kupambana na kuwashinda watu waliotoka shule binafsi waliosoma kwa lugha ya Kiingereza.

Wakati wa mitihani ya nusu muhula uliwadia na tukafanya mtihani, matokeo yalitoka na nikawa mtu wa 50 kati ya wanafunzi 120. Hakika siku hii nilijiona kuwa nina akili sana , maana niliwashinda wanafunzi 70 wakiwemo wale waliotoka shule binafsi. Niliwaza pia kuwa mimi niliyeshindwa darasa la saba nimewashinda waliofaulu darasa la saba , nilipata nguvu Zaidi ya kusoma. Tulivyotoka sehemu ya mkutano tulipokuwa tunapewa matokeo ,nilipata rafiki ambaye anaitwa Avelina, alinifuata na kunieleza mbinu nyingi sana za kuijsomea lakini muhimu Zaidi alinisisitiza na kusema” rafiki yangu wewe na mimi tuna akili sana labda tu hatujajua jinsi ya kujisomea. Lkn pia nafasi ya kwanza haijawekewa mtu mmoja tu. Kila mtu ana haki na anastahili kuwa wa kwanza kinachotakiwa ni juhudi ili kuifikia”. Maneno haya yaliniongoza daima katika masomo yangu na yalinipa motisha.

Safari yangu ya elimu ilizidi kupamba moto maana nilijikuta kila nianavyozidi kupanda darasa nafanya vizuri Zaidi. Nilichukua masomo ya sayansi na nilifaulu vizuri kidato cha nne, nikafanikiwa kuendelea kidato cha tano na mpaka sasa nimehitimu Chuo Kikuu cha kikatoliki cha Afya na Sayansi Shirikishi (BUGANDO) kozi ya Famasia. Wakati ninasoma niliweza kutambua karama mbalimbali nilizonazo zikiwemo, uongozi, uimbaji, uandishi na upambaji. Ndoto ya kujiendeleza bado ninayo hasa katika kada yangu na kada nyingine ninazozipenda iwapo nitapata fursa kwa sababu napenda kujisomea , na ninaamini pia “elimu haina mwisho, na kila siku tunajifunza, hata ile siku ya mwisho duniani tutajifunza namna ya kukata roho japo hatuwezi kurudi kusimulia.

FUNZO

  • Nilichojifunza katika safari yangu ya elimu ni kuwa kushindwa mtihani wa darasa la saba sio kuwa hauna uwezo katika elimu. Watoto wengi wamekuwa wanasoma mpaka darasa la saba na wakifeli wazazi wao wanawaambia elimu sio fani yao, huo sio ukweli.
  • Nimetambua kuwa kadri unavyosoma unapanua uwezo wa kufikiri na unakuwa na wigo wa kujua mambo mengi yenye manufaa katika maisha yako, ikiwemo utambuzi wa vipaji vyako elimu ya primari haitoshi kukusaidia kujua ni nini unaweza.
Ni sawa siku hizi tunasoma na ajira ni vigumu kupata lakini tukiwa na wanajamii walio na elimu ya sekondari ngazi ya chini tutapunguza asilimia kubwa ya matatizo ya kimaisha yanayoendelea katika jamii zetu, tutakuza uchumi wa nchi kwa sababu kila shughuli za kiuchumi zitaendeshwa kisomi na mengine mengi. Zaidi ninaiomba Serikali izidi kuwekeza kwenye elimu kuanzia ngazi ya chini mpaka elimu ya juu ili tutoe wasomi walio bora na wenye fikra zamabadiliko chanya kwa ajili yetu. Mazingira bora, maktaba na vitabu vya kutosha pamoja na walimu wa kutosha mashuleni huchochea uwepo wa Elimu bora na si Bora Elimu.

ELIMU HAIMTUPI MSOMI KAMA JEMBE LISIVYOMTUPA MKULIMA.
 
Wapedwa habari za majukumu? Naombeni kura zenu na mchango wa mawazo juu ya mada hii.Nitafurahi sana nikipata mawazo na marekebisho kutoka kwa wanafamilia wa Jamii forum. KURA YAKO NI MUHIMU SANA na COMMENT yako katika safari yangu ya uandishi.🤝
 
Ninachukua wasaa huu kuzungumza na nyinyi ndugu zangu kupitia andiko hili, suala la kupima uelewa wa mtu katika elimu isiwe kwa mitihani hasa kwa elimu ya msingi ambayo Watoto bado wanakuwa na umri mdogo. Kwa hiyo wengi wao wanakuwa hawajatambua ni njia gani watumie katika kusoma ili kufanya vizuri kwenye masomo yao. Mfano Halisia ni mimi mwenyewe na hiki ndicho kilichotokea.

Mwaka 2002 nikiwa na umri wa miaka sita nilianza safari yangu ya elimu na nilianza moja kwa moja darasa la kwanza katika shule inayoitwa Kambarage iliyoko Karagwe mkoa wa Kagera. Darasa la kwanza mpaka darasa la tatu lilipita tukafika darasa la nne ambapo huwa ni darasa la mtihani wa Taifa. Tulifanya mitihani mingi ikiwemo mtihani wa kata, wilaya na mkoa kabla ya mtihani wa taifa, kwa ujumla mimi nilitimiza wajibu wakufanya mitihani sikuwa najali kuwa nitakuwa wa ngapi au nahitaji nifikishe wastani kiasi gani.

Punde si punde uliwadia wakati wa mtihani wa taifa na tulifanya mtihani tukafunga mapema shule na kwenda mapumziko tukiwa tunasubiri matokeo ya mtihani wa taifa. Mwezi wa 12 mwaka 2005 matokeo yalitoka na hapo nilijiua na kuanza kuelewa kidogo nini maana ya wastani. Namshukuru Mungu Pamoja na kuwa sikuwa nasoma sana nilifaulu kwa wastani wa kuchechemea. Niliendelea na masomo mpaka mwaka 2009 nilipoingia darasa la saba na hapo nilikuwa mtahiniwa tena. Shuleni walimu wetu walijitahidi sana kutupa mazoezi na mitihani ya kutosha kwa ajili ya kutuandaa na mtihani wa mwisho.

Mnamo tarehe mbili mwezi wa tisa mwaka 2009 tulifanya mtihani wa taifa na tukahitimu elimu ya msingi kwa furaha kubwa ikiambatana na mahafali. Baada ya miezi miwili kupita matokeo ya mtihani wa taifa yalitoka, na kubandikwa kwenye mbao za matangazo halmashauri ya wilaya. Hakika siku hii ni sku ambayo siwezi kuisahau kamwe katika Maisha yangu. Asubuhi na mapema sana nilisindikizwa na mdogo wangu wa kiume kwenda kuangalia matokeo tukiwa tumeagizwa na mama mzazi. Tuliondoka na kuelekea sehemu husika, wakati tunawasili pale, tulikuta watu wengi sana waliowahi kuangalia matokeo, wakiwemo watu wa darasa langu, na wengine walikuwa wakipongezana na kuambiana kila mmoja amechaguliwa shule gani.

Ghafla kundi moja la wavulana niliosoma nao waliokuwa pale waliponiona ,walikonyezana na kusema kwa sauti ya chini” yule binti mdogo wa darasa jina lake halipo, hajafaulu.” Nilijisikia vibaya sana baada ya kusikia maneno hayo. Lakini sikutaka kuonesha usoni kama nimesikia kwa sababu nilikuwa nimeambatana na mdogo wangu. Nilitembea kwa ujasiri mpaka kwenye mbao za matangazo na kuanza kutafuta jina langu ilihali nikijua halipo, niliangalia wenzangu wamechaguliwa shule gani na baada ya hapo nikamchukua mdogo wangu turudi nyumbani maana na yeye alitafuta jina langu hakuliona kabisa.

Wakati tunarejea nyumbani nilipanga na mdogo wangu tusimwambie mtu yeyote hata mama mzazi kuhusu suala hili Kusudi tusipoteze furaha ya mama sababu alikuwa anapenda nisome na nilikuwa mtoto wa kwanza katika familia. Sababu nyingine iliyotupa kiburi tusiseme kuna shule binafsi nilkuwa nimeshafanya mitihani na kupata nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari. Baada ya kuwasili nyumbani tulimwambia mama nimefaulu na tukaendelea na maandalizi ya kuanza kidato cha kwanza.

Nilipoanza kidato cha kwanza kwenye shule ya sekondari ya wasichana Hekima iliyoko Bukoba, Kagera nilikuwa nimeazimia kusoma kwa bidii sana. Bila kujali kuwa nimefeli darasa la saba ,nilijiona nimepata fursa ya dhahabu kwangu kujaribu tena katika masomo. Bahati nzuri tulivyoanza masomo tulikuwa na miezi mitatu ya “English Course” kwa ajili ya kutusaidia sisi tuliotoka shule za serikali. Darasa letu lilikuwa na wanafunzi wengi waliotoka shule binafsi, baada ya kugundua hilo nilianza kurudi nyuma kimawazo na kujiona nikiwa wa mwisho darasani. Niliamini kuwa sina uwezo wa kupambana na kuwashinda watu waliotoka shule binafsi waliosoma kwa lugha ya Kiingereza.

Wakati wa mitihani ya nusu muhula uliwadia na tukafanya mtihani, matokeo yalitoka na nikawa mtu wa 50 kati ya wanafunzi 120. Hakika siku hii nilijiona kuwa nina akili sana , maana niliwashinda wanafunzi 70 wakiwemo wale waliotoka shule binafsi. Niliwaza pia kuwa mimi niliyeshindwa darasa la saba nimewashinda waliofaulu darasa la saba , nilipata nguvu Zaidi ya kusoma. Tulivyotoka sehemu ya mkutano tulipokuwa tunapewa matokeo ,nilipata rafiki ambaye anaitwa Avelina, alinifuata na kunieleza mbinu nyingi sana za kuijsomea lakini muhimu Zaidi alinisisitiza na kusema” rafiki yangu wewe na mimi tuna akili sana labda tu hatujajua jinsi ya kujisomea. Lkn pia nafasi ya kwanza haijawekewa mtu mmoja tu. Kila mtu ana haki na anastahili kuwa wa kwanza kinachotakiwa ni juhudi ili kuifikia”. Maneno haya yaliniongoza daima katika masomo yangu na yalinipa motisha.

Safari yangu ya elimu ilizidi kupamba moto maana nilijikuta kila nianavyozidi kupanda darasa nafanya vizuri Zaidi. Nilichukua masomo ya sayansi na nilifaulu vizuri kidato cha nne, nikafanikiwa kuendelea kidato cha tano na mpaka sasa nimehitimu Chuo Kikuu cha kikatoliki cha Afya na Sayansi Shirikishi (BUGANDO) kozi ya Famasia. Wakati ninasoma niliweza kutambua karama mbalimbali nilizonazo zikiwemo, uongozi, uimbaji, uandishi na upambaji. Ndoto ya kujiendeleza bado ninayo hasa katika kada yangu na kada nyingine ninazozipenda iwapo nitapata fursa kwa sababu napenda kujisomea , na ninaamini pia “elimu haina mwisho, na kila siku tunajifunza, hata ile siku ya mwisho duniani tutajifunza namna ya kukata roho japo hatuwezi kurudi kusimulia.

FUNZO

  • Nilichojifunza katika safari yangu ya elimu ni kuwa kushindwa mtihani wa darasa la saba sio kuwa hauna uwezo katika elimu. Watoto wengi wamekuwa wanasoma mpaka darasa la saba na wakifeli wazazi wao wanawaambia elimu sio fani yao, huo sio ukweli.
  • Nimetambua kuwa kadri unavyosoma unapanua uwezo wa kufikiri na unakuwa na wigo wa kujua mambo mengi yenye manufaa katika maisha yako, ikiwemo utambuzi wa vipaji vyako elimu ya primari haitoshi kukusaidia kujua ni nini unaweza.
Ni sawa siku hizi tunasoma na ajira ni vigumu kupata lakini tukiwa na wanajamii walio na elimu ya sekondari ngazi ya chini tutapunguza asilimia kubwa ya matatizo ya kimaisha yanayoendelea katika jamii zetu, tutakuza uchumi wa nchi kwa sababu kila shughuli za kiuchumi zitaendeshwa kisomi na mengine mengi. Zaidi ninaiomba Serikali izidi kuwekeza kwenye elimu kuanzia ngazi ya chini mpaka elimu ya juu ili tutoe wasomi walio bora na wenye fikra zamabadiliko chanya kwa ajili yetu. Mazingira bora, maktaba na vitabu vya kutosha pamoja na walimu wa kutosha mashuleni huchochea uwepo wa Elimu bora na si Bora Elimu.

ELIMU HAIMTUPI MSOMI KAMA JEMBE LISIVYOMTUPA MKULIMA.
Hongera sana kwa hatua uliofikia, pia mtihani ni mtihani tu mtoto anaweza kufeli darasa la saba na wazazi kumkatia tamaa na kumbe uwezo anao, na wapo wengi walishindwa kufaula darasa la 7 lakini baada ya kupelekwa private walifanya vizuri kuzidi hata wale waliofaulu, mzazi au mlezi anatakuwa kuwa mstari wa mbele kusimamia elimu ya mtoto bila kumsahau MUNGU.
 
Back
Top Bottom