Mwanafunzi wa darasa la Saba alikatishwa masomo kwa ajili ya ndoa

Shining Light

JF-Expert Member
Jan 8, 2024
214
288
Nilipokuwa darasa la Saba mwaka 2011, tulishuhudia mwanafunzi mwenzetu akisitishwa masomo ili arudi nyumbani Skonge kwa ajili ya ndoa. Hii ilikuwa mshangao mkubwa kwetu sote, hasa ikizingatiwa kuwa tulikuwa tunakaribia mitihani ya mwisho ya NECTA na wazazi wake tayari walikuwa wamemlipia ada yote, hivyo angekuwa na uwezo wa kumaliza masomo ya shule ya msingi.

Binti huyo alikuwa akilia sana kwa sababu hakutaka kuolewa, lakini hakuwa na uwezo wa kufanya chochote na hivyo alilazimika kurudi nyumbani kwao kwa ajili ya ndoa.

Tukio hilo lilikuwa ni ishara ya dhahiri ya ukatili kwa watoto. Kuacha mwanafunzi kusitishiwa masomo na kufanyishwa ndoa wakati bado anatakiwa kuendelea na elimu yake ni kinyume cha haki za binadamu na linakiuka haki za mtoto kwa elimu na uhuru wa kuchagua mustakabali wake mwenyewe.

Je, Ni visa gani vya ukatili kwa watoto umeshawahi kushuudia? Na ulifanya ninii?

Kisa kama hiki husikitisha sana na kwenda kinyume na haki za msingi za binadamu, hasa haki za mtoto na haki ya elimu. Kwa hali kama hii, hatua mbalimbali zina wza kuzingatiwa;

Kwa watoto walio katika hatari ya kufanyishwa ndoa, serikali na mashirika ya kiraia yanaweza kutoa msaada wa kisaikolojia na kisheria, pamoja na kutoa makazi salama kwa watoto hao ili kuepuka ndoa za utotoni. Ila zoezi hili huenda linaweza lisiwe rahisi kwa sababu ya jinsi watu hawashtaki kuhusu mambo kama haya.

Kuna haja ya kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ndoa za utotoni kwa wasichana na umuhimu wa elimu kwa watoto wote kujua haki zao ni muhimu. Elimu inaweza kufanywa kupitia mikutano ya jamii, vipindi vya redio na televisheni, mabango, na njia zingine za mawasiliano.

Kuwashirikisha wazazi, viongozi wa dini, na jamii kwa ujumla katika kuzuia ndoa za utotoni. Kwa kufanya hivyo, inawezekana kujenga uelewa na mabadiliko ya kitamaduni yanayohitajika kuheshimu haki za watoto na kukuza elimu kama kipaumbele haswa kwa mtoto wa kike.
 
Back
Top Bottom