Mtihani wa utimilifu darasa la saba

Aug 30, 2023
86
111
Habari za leo ndugu,

Jamaa, wazazi pamoja na marafiki, tunategemea kuwa na mtihani wa utimilifu wa darasa la saba, utakaofanyika jumatano na alhamisi katika shule zetu zote za umma pamoja na za binafsi zilizosajiliwa na baraza la mitihani la taifa.kuzingatia umuhimu wa mtihani huu nilikua na maombi hasa kwa wazazi wenye watoto wanaohitimu darasa la saba,

Kwanza kuachana na mila potofu za kuwashawishi watoto kuangalizia, kufanya mtihani vibaya ili wafeli wawasaidie kazi za nyumbani au waoelewe, kufanya hivi unamuharibia mtoto maisha yake na unaikandamiza haki yake ya msingi pamoja na mojawapo ya mapaji ya roho mtakatifu ,

Pili kuanzia sasa tuhakikishe tunamlinda mtahiniwa asiweze kuwaza jambo lolote ambalo linaweza kumfanya awaze nje ya mtihani mfano unyanyasaji, kubugudhiwa, kuadhibiwa , kutopewa huduma za msingi, kutamkiwa maneno mabaya nk. Tatu, tujitahidi watoto wetu wawe na vifaa vyote vya mitihani ikiwemo rula, penseli pamoja na kalamu zinazoandika , watoto wetu wawahi mapema kwenye maeneo yao ya kufanyia mtihani, Mwisho tusisahau kuwaombea na kuwatia Moyo wanapotoka nyumbani kuelekea katika mtihani huu.

Kwa wale watakaohitaji shule nzuri za pre form one, na form one mikoa ya Kagera, Kilimanjaro, arusha pamoja na Dar es salaam.msisite kuwasiliana na Mimi kwa namba 0743567159. Ahsanteni na nawatakieni usiku mwema.
 
Huku bado usiku haujafika.Naruhusiwa kusubiri hadi ufike huo usiku halafu nisome hayo maneno uwe umenitakia usiku mwema?
 
Back
Top Bottom