Mtanzania na unafki ni sawa na tumbo na msosi..

Its Pancho

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
14,238
22,673
Wakuu

Kwa watu wa mataifa mbalimbali wana sifa zao kila taifa..
Mathalani ukienda India aslimia kubwa ni uchafu,
Ukienda China wao wanakula kila kitu kinachotembea ardhini na kupaa.

Ukienda Jamaica wao wanasifika kwa matumizi makubwa ya mmea (bangi).

Hivyo hivyo inakwenda kwa wabongo ambao sifa yetu kubwa ni unafki wa kiwango cha Juu sana.

Twende taratibu,

Ukienda mitaani au hata hapa jf utakuta hill jambo, nitagusia mfano wa mambo haya ya entertainment hasa muziki.

Kuna yule baunsa mkenya anarap anaitwa khaligraph Jones ..!
Kwa kweli jamaa amebarikiwa kipaji lakini uchanaji wake ni ule umejaa slang za kikenya na kiswahili fasaha ni kidogo Sana,

Kiasi kwamba kwa mbongo ni ngumu kumuelewa anachorapa kwa undani , lakini wabongo kwa unafki na kufuata mkumbo utaskia
"Aaah mwamba anajua sanaa, kuliko Nikki mbishi"
Au utaskia.
*bongo hamna rapper kama khaligraph kuna takataka"

Sasa huu ni nini kama sio unafki? Ukiuliza hizo nyimbo zake anachana ninj utaishia kupewa blah blah tu oooh "respect the og" basi .

Tuachane na huo mfano.

Ingawaje kingereza ni lugha muhimu kwa sasa duniani hata wasanii wetu nao wamejaribu kwenda na beat (kwenda na matumizi ya kingereza).

Wanaija wanafanikiwa sababu ya matumizi ya lugha hiyo japokuwa wanatumia sana slang ukiachana na factors zengine..

Sasa akiimba kingereza diamond au harmonize zile slang kama za wanaija zile za "I go die for u"
Kwa wabongo basi watapondwa maskini mpaka basi na watanzanja wenzao ambao walipaswa kuwasapoti in generally..

Twende sasa ..
Ila hapo hapo akiimbia davido hizo "ago chop yo money" basi utaskia wabongo

*aaaha davido mwamba sana anajua mpaka anakera hapa nimerudia hii ngoma tangu juzi"
Au
"Wizkid huyu mwamba anajua na nusu, lazima achukue BET"
Mwengine atakwambia

"Burna boy mwamba kajaza 02 arena ndio msanii Wangu pendwa"

Ukiuliza wanaimba vizuri sawa je mashairi yao unayaelewa kisawa sawa?
Utaishia kupewa tu jibu " bandana ngoma ya moto wewe"

Hivi kuna msanii wa hovyo kama Asake? Ana tofauti gani na chinno kid?

Si bora chinno ambaye kibongo bongo anaeleweka anachoimba? Anasumbua kwa lugha yetu? Sasa mbongo alivyo mnafki atakwambia Asake ni wa moto kuliko dogo chinno ingawaje haelewi anachoimba Asake ..UNAFKI ..!

Mifano ni mingi sana.
Amapiano asili yake ni sauzi sawa ..
Hiyo haizuii nchi zingine wasiimbe amapiano , ingawaje wabongo wanajaribu kuimba amapiano lakini ubora upande wa sound hauwezi kufikia ule wa wenye huo mziki (wasauzi).

Tunakuja pale pale asilimia kubwa ya wasauzi wanaimba kizulu na lugha zao za asili sijui kixhosa ,
Hivyo kwa mbongo wa tandahimba au manzese ataelewa nini? Zaidi ya kusikiliza beat tu?

Msanii kama ntoshi gazi anaimbaga nini yule.wimbo mzima kelele? Ila wabongo watakwambia jamaa anajua bhana , ni unafki tu.

Hapo hapo wanakwambia
"Amapiano za bongo ni takataka me sisikilizagi uchafu"

Wakati kimsingi jamaa wetu wanajitahidi kutuburudisha na zaidi wanaimba kwa lugha yetu ya kiswahili lakini wanaambulia disappointment kutoka kwa wabongo wenzetu..!

Hii sio sawa hata kidogo tupende vyetu , unadhani wanaija kama wasingependa vyao hizo show za majuu huko wakina davido wangemuimbia nani kama sio hao hao naija diaspora???

Wabongo mpaka majuu wana tabia hizo za unafki na majungu utaskia "diamond amepiga show sebleni kwa mtu huko USA"

Kimsingi tunajimaliza wenyewe kwa unafki wetu..

Unamsomesha mtoto wa jitani na wako haendi shule kweli?
 
Asante kwa kuwachana Wabongo Mkuu.

WAMEKUSIKIA, NA WAMEAHIDI HAWATORUDIA TENA.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Nimefurahi sana nakumbuka nikiwa nafanya usaili kigoma wa NS yalinikuta badae kidogo kuja kwenda Tpdanga hapo pakawa zaidi huwa nacheka sana nikikumbuka kiuhalisia siyo wa Tanzania ni sisi waafrika.

Ngoma kama hizi hazina wachangiaji na tukichangia tunaambiwa WANAA.

Respect to all maroon beret.
 
Nimefurahi sana nakumbuka nikiwa nafanya usaili kigoma wa NS yalinikuta badae kidogo kuja kwenda Tpdanga hapo pakawa zaidi huwa nacheka sana nikikumbuka kiuhalisia siyo wa Tanzania ni sisi waafrika.

Ngoma kama hizi hazina wachangiaji na tukichangia tunaambiwa WANAA.

Respect to all maroon beret.
Me nyimbo za kibongo zinaniboa hasa kuanzia mwaka 2009 kuja juu, ila naioenda Rush kaimba yule binti
 
Back
Top Bottom