PharaohMtakatifu
JF-Expert Member
- Jul 3, 2023
- 659
- 1,074
Wasalam,
Mimi kama Pharaoh Mtakatifu nashangaa sana na baadhi ya ndugu zangu Watanzania kwanini, hatupendani kwanini tuna wivu na kwanini ni wavivu kiasi hiki!
Sijawahi enda nje ya nchi kikazi la hasha naogopa dhambi au uongo, lakini nimefanya kazi na watu wa mataifa mbalimbali baadhi nayaorodhesha hapa; Waaustralia, Canada, Philipino, China, South Africa, Misri, Burkinafaso, Ghana, Mali, Zambia, Malawi nk.
Nimefanya nao kazi za migodini kwa muda mrefu sana, wengine hata kibiashara, nakiri wazi jamaa wanapendana kuliko sisi wabongo.
Kwanini mbongo akiona mbongo mwenzie kapandishwa cheo au kamzidi kwa lolote aisee anainua majungu na fitina hatari, lakini hali ni tofauti kabisa na mataifa mengine kama Ghana. Mwezao akipandishwa cheo tegemea watamfanyia party ya kumpongeza hata kama wasipofanya lakini utaona wazi kabisa wanampa sapport kubwa sana mwenzao.
Hata hawa Waarabu, Wamisri na mataifa mengine hufanya hivyohivyo lakini kwetu sisi ni toafuti. Ikitokea inafanywa party basi jua kabisa hiyo party umehusika wewe asilimia %99.99 japo watakuja kula na kunywa kwa unafiki tu huku wakizuga kucheza, lakini kwa chini chini utasikia hapo hapo kwenye party watu wanapiga misumari na kula umewalisha! Tubadilike ndugu zangu.
Wabongo ni wavivu sana, ni ukweli usiopingika. Mtanzania atakuja kuomba kazi huku mikono ikiwa mbele tena kwa nidhamu na heshima ya juu sana lakini pindi akipata tu hiyo kazi ndio utajua humjui!
Atakuonuesha kila aina ya mabaka yake na ruhusa zisizo na maana kabisa, akimaliza za kuuguliwa mke au watoto anaanza kuua ndugu zake kama mjomba kafariki nahitajika msibani, mara shangazi, mara mama mdogo kafa na ajari ndio alikuwa ananilea na visingizio vya ajabu ajabu ilimradi umpe ruhusa!
Hata akiwa kazini anafanya tu ili muda ufike arudi nyumbani. Mbongo yupo radhi alale muda wa kazi na akuambie angalia ukiona kiongozi anakuja au tochi/nisitue (kwa waliowahi fanya kazi za underground wataelewa) jambo ambalo kwa mataifa mengine ni ngumu sana kuliona.
Mbongo hajali kabisa muda wa kazi lakini muda wa kutoka kazini anajali kuliko kawaida, tena akichelewa siku 3 tu anadai alipwe lakini kuchelewa eneo la kazi ni kila siku.
Hawa Wazungu hasa wa Canada na Australia niliowahi kufanya nao kazi aisee hadi raha, wanakuelekeza kwa vitendo na kazi mnafanya wote, hawachagui, ukifika muda wa msosi ni msosi. Yaani ukienda nae site unajua kabisa hapa tunafika kwa wakati eneo la kazi na tutafanya kazi kwa wakati na kutoka kwa wakati na kitu kinaenda hivohivo.
Mbongo sasa umkute yeye anajua kitu fulani na wewe hukijui, utajuta! Atakupasha matusi mara wee umesoma kweli wewe, wakati yeye hata la saba hakumaliza!
Yaani hii haipo kwa wengine, hao wote anakumbia hapa nitakufundisha kwa masaa 2 kwa leo tutaendelea tena kesho, ni raha tu mradi wewe uwe unajua lugha tu na hata usipojua kikubwa juhudi na heshima yako utaelewa hadi kimombo chenyewe!
Wabongo tunakera sana, kwanini tunashindwa kujifunza hata kwa Kafrika wenzetu kama watu wa Mali na Malawi, Ghana nk?
Akiona unataka kuchomoza tu mbongo anaenda kukusagia kunguni kwa boss ili ufukuzwe kazi, hapo ndio raha ya mbongo. Sasa kwa wenzetu ni huzuni sana mwenzao akifukuzwa kazi!
Najiuliza tunafeli wapi sisi? Mimi au yule akifanikiwa wewe utapungukiwa na nini? Kwanini uwe mvivu basi? Kazi zenyewe tunapeana kwa kujuana, ukabila upo juu sana bongo hii.
Ni mengi acha mimi Pharaoh Mtakatifu niishie hapa.
Tubadilike.
Ahsanteni.