Mtanzania mwenye matatizo ya akili kurejeshwa nchini toka Afrika ya Kusini

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
20240215_142351.jpg

Ubalozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Afrika Kusini unawashukuru kwa dhati watu wote waliotusaidia kuwapata ndugu wa Bw.Karim, Mtanzania mwenzetu mwenye matatizo ya akili hivi sasa, ambaye aliondoka nchini Tanzania mwaka 1998 kwa ajili kuja Afrika Kusini (Bondeni), kutafuta fursa za Kimaisha.

Aidha, Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umempeleka Hospitali Bw. Karim, kwa ajili ya kumcheki afya yake ya mwili na akili, ili pia kupata Cheti cha Daktari kitakachoonesha kuwa anaweza kusafirishwa kwa Ndege kurudi nchini Tanzania bila ya yeye kuwa hatari kwake mwenyewe na kwa abiria wengine. Kupatikana kwa Cheti hicho, kutauwezesha Ubalozi kumrejesha nyumbani Tanzania ili aungane na familia yake.

20240215_142418.jpg

Bw. Karim akiwa hospitali jana mchana sambamba na Maafisa wa Ubalozi waliofika kumjulia hali na kupata taarifa ya maendeleo yake. Pichani, Bw. Karim akizingumza na Mama yake Mzazi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 26 ya familia kutofahamu iwapo angali hai au alikwishafariki.
 
View attachment 2904941

View attachment 2904943

Madhara ya uga hayo, hata hapa nyumbani wengi wapo, bora apelekwe rehabilitation centre au Milembe hapa ni hatari zaidi.
 
Kwa uzoefu wangu wa ubalozi wa Tz nikiwa nje kwa asilimia kubwa hiyo pesa hawajatowa wao msaada wao ni wa kidplomasia kupata docs za kusafiria, huo ubalonzi hawana fungu la kusaidia watanzania kwa pesa.....
Mimi nimewasifu kwa msaada wao wowote ule walioutoa wala sijasema kuhusu pesa,mpaka hapo ni msaada mkubwa sana walioutoa japo hata wewe huna uhakika kua pesa ya kumsafirisha mwana mpotevu imetoka wapi,pengine hata hiyo pesa imepatikana baada ya ubalozi kuanza kushughulikia hiyo issue.
 
View attachment 2904941

Ubalozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Afrika Kusini unawashukuru kwa dhati watu wote waliotusaidia kuwapata ndugu wa Bw.Karim, Mtanzania mwenzetu mwenye matatizo ya akili hivi sasa, ambaye aliondoka nchini Tanzania mwaka 1998 kwa ajili kuja Afrika Kusini (Bondeni), kutafuta fursa za Kimaisha.

Aidha, Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umempeleka Hospitali Bw. Karim, kwa ajili ya kumcheki afya yake ya mwili na akili, ili pia kupata Cheti cha Daktari kitakachoonesha kuwa anaweza kusafirishwa kwa Ndege kurudi nchini Tanzania bila ya yeye kuwa hatari kwake mwenyewe na kwa abiria wengine. Kupatikana kwa Cheti hicho, kutauwezesha Ubalozi kumrejesha nyumbani Tanzania ili aungane na familia yake.

View attachment 2904943
Bw. Karim akiwa hospitali jana mchana sambamba na Maafisa wa Ubalozi waliofika kumjulia hali na kupata taarifa ya maendeleo yake. Pichani, Bw. Karim akizingumza na Mama yake Mzazi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 26 ya familia kutofahamu iwapo angali hai au alikwishafariki.
Hongera sana Ubalozi wetu huko South Africa!Mungu awatangulie katika kila jambo pia msisahau kuwatafutia Scholarships Watanzania wenye nia ya kuja huko.Barikiwa sana sana Ubalozi wetu!!!
 
Madhara ya uga hayo, hata hapa nyumbani wengi wapo, bora apelekwe rehabilitation centre au Milembe hapa ni hatari zaidi.
Acha kuhukumu. Wapo ambao wamechanganyikiwa kwa maisha tu kwenda kinyume na matarajio yao. Namkumbuka somebody Zinga kule UK jamaa alitoka Tz akiwa na div 1 ya juu form six akiwa na ndoto za kujisomesha chuo UK lakini maisha ya UK yalimchanganya hadi kupata tatizo la afya ya akili. Sijui yuko wapi sasa hivi huyu mtu.
 
Ubalozi umefanya jambo la utu sana na unastahili pongezi.
Chama cha watanzania waishio Africa kusini (mabaharia) ndio wanastahili hizi pongezi. Wao ndio waliomuibua huyo ndugu, waliochanga fedha mpaka kufanikisha zoezi hilo kukamilika. Na sio huyo tu wameshasaidia wengi wenye uhitaji
 
Ubalozi wapo busy kuuza hati za kusafiria hata kwa wadogo wasio na kitu...
 
Back
Top Bottom