Mtangazaji wa ITV Hemed Kivuyo, atosha

Mtangazaji wa ITV Hemed Kivuyo, atosha

Huyo alitakiwa awe mchunga mbuzi siyo mtangazaji, hovyo kabisa. Mithali hizo hizo Kila siku hazina uhusiano na anachotaka kukisema, wengine tunapata kichefuchefu kumsikiliza.

Mithali= Methali...kwanini msikubali tuu mpewe shule..??
 
Mi kwakweli huwa napenda kumsikiliza na kiswahili chake kinanifurahisha.Keep it up Kivuyoooo.
 
Kwa mimi ananifurahisha sana ikiwa Yanga.Simba.Azam raha sanaa
 
Kivuyoooo.... "Kenda haiko mbali na kumi".... Ikiwa utamsikiliza kwa mara ya kwanza, unaweza toka kapa!! Kama utajenga chuki siku hiyo, basi huto msikiliza tena. Ila ukipendezewa siku ya kwanza, hakika huta diriki kumkosa isipo kua kwa sababu maalum.
Nilichogundua siku akionekana basi siku hiyo jua mbwembwe hazita sheheni. Ila kama akisikika kwenye "background" hapo ndio mta mtambua kama yeye ni mzee wa riwaya na mjukuu wa Shaaban Robert.
 
Naomba niseme kitu kimoja,
Mimi binafsi nina asili ya mikoa iliyoanza kuzungumza Kiswahili miaka ya nyuma sana. Nakiri mtu hawez zungumza Kiswahili cha aina yoyote nisimuelewe.
Hemed Kivuyo anatumia tashbiha sana na methali nyingi katika utangazaji wake. Ni kitu kizuri na kinavutia ila watu wengi hasa walioanza kujifunza Kiswahili shuleni wanapata tabu kumuelewa. Ushahidi ninao huku kanda ya ziwa, maneno mengi ya Kiswahili hawayajui. Wengi walianza kuongea Kiswahili walipoanza shule.
Ishu sio kumponda Kivuyo ishu ni kwamba watu wajifunze Kiswahili waache kulalamikia vitu visivyo na msingi. Kumbukeni session inaitwa michezo na burudani. Yale maneno ya Kivuyo nayo burudani. Big up Kivuyo. Keep it up.

"Unamlilia nani maisha umeyakosea mwenyewe" Mbwiga wa Mbwiguke wa Clouds

Huyu naye wengi hawamwelewi.

Kweli kabisa...! Na ndio muda muafaka wa kununua Kamusi za TATAKI
 
Huyu bwana kwanza anahatibu kuswahili, nashangaa mamlaka husika zimekaa kimya, msikilizeni badala ya kusema moja anasema moya, ndio maadili ya utangazaji?
 
nimeamini uchambuzi wa mdau mmoja hapa jf aliesema watz wengi upeo wetu wa kuchanganua mambo ni mdogo sana na ndo maana hata comedy zetu ili walio wengi wacheke lazima mwanaume aigize sauti ya kike. au avae kikekike au aweke mandevu ya bandia na kitambi cha bandia..hapo ndo utaona watu wanacheeeekaaa daahhh...hivi kweli ntakaa nawewe sebuleni tuangalie vichekesho vya chris rock?? will smith..??...aahh sahau we subiri joti au kingwendu abadili sauti ndo utaelewa..how come humuelewi kivuyo???
 
Nilikuwa naangalia taarifa ya habari ya ITV upande wa michezo huyu mtangazaji badala ya kutuelezea mechi ya Taifa stars na Nigeria ilivyokuwa, yeye anatia mbwembwe kwa misemo yake isiyoeleweka.

Sio watazamaji wote walioshuhudia mechi hiyo ni vyema akasimulia kwa lugha ya kawaida watu waelewe badala ya misemo isiyoeleweka.

Kiukweli usomaji wake wa habari unaondoa kabisa ladha ya habari anayosoma..lakini simlaumu sana. Vyombo vyetu vya habari vipo nyuma sana ulinganisha na vya mataifa jirani
 
Hivi mpaka sasa bado anaripoti kwa staili ile???
 
Nimeona leo niongee japo kwa ufupi kuhusu huyu jamaa,tangu nimeanza kumsikia sikuwahi kuchoka na story zake hasa katika michezo,jinsi anavyoripoti aisee utatamani asimalize jamaa ana mbwembwe na misemo ya ajabu na kama kichwa chako kina upungufu wa madini hakika hutamuelewa,hua naweza kuchelewa kuangalia habari lakini si upande wa michezo niko makini sana hata nikjiskia kuangalia habari channel nyingine ikifika muda wa michezo natoka speed mpaka i.t.v yote hiyo kumsikiliza hemed kivuyo.hongera brother.
naamini humu nna wenzangu.
 
Ni kweli, huu ni ubunifu pia.
Michezo ni sanaa na sanaa imejaa ubunifu, mbwembwe na majigambo pia.
Nampongeza sana
 
Nilicompare alivokuwa anaongea nyuma ya camera na akiwa mbele ya camera kuna kautofauti wa misamiati.

Akiwa mbele ya camera hakuna misamiati, ila akiwa nyuma ya camera utasikia mashairi yote.
 
Nilicompare alivokuwa anaongea nyuma ya camera na akiwa mbele ya camera kuna kautofauti wa misamiati.

Akiwa mbele ya camera hakuna misiati, ila akiwa nyuma ya camera utasikia mashairi yote.
ni kweli.
 
Back
Top Bottom