Mtangazaji wa ITV Hemed Kivuyo, atosha

Mtangazaji wa ITV Hemed Kivuyo, atosha

watu wengine bwana ...yaani wewe had inafika SAA 2 hukuwa unajua Matokeo ya stars na Nigeria na ulitegemea ukajue ktk taarifa ya habari...kwani lazima uangalie ITV ? kwa taarifa yako wenzio tunajionea miutamu tu...na aongeze mbwembwe zaid na zaid ....kiswahili kinakosa wataalamu .....hata akitumia neno imma fa imma hujui maana yake ....na hata akisema hansini radhi sitini majinuni.......oyoooooooooooo

Eeeh bwana umenifurahisha sana mkuu, asante sana.
 
Kwakweli hakuna mtoa taarifa za habari za michezo ninayemkubali kama Kivuyo.
Ukifika muda wa ripoti kutoka kwake naongeza sauti ya juu kabisa ili nipate burudani vizuri.
Popote ulipo Hemed Kivuyo pokea pongezi zangu, Mungu akupe umri mrefu uzidi kutupa burudani.

Kweli kabisa,kila mtu anajijengea utambulisho wake kwenye jamii,Mimi hata nikiwa chooni huku taarifa ya habari za michezo inaendelea,akitangaza kivuyo namtambua vizuri
 
Keep it up br Kivuyo, much respect, hawa makanjanja walitegemea utangaze kwa huzun kisa wameshindwa tena nyumban, pia mabadiliko yanawapa presha + shule hakuna , shiiida.
 
Sasa amekosea nini pale au kusema watu walivyonyoosha vidole viwili juu.....ile ni misemo,nahau na methali...sasa kama hujasoma hizo akusaidiaje
 
Nilikuwa naangalia taarifa ya habari ya ITV upande wa michezo huyu mtangazaji badala ya kutuelezea mechi ya Taifa stars na Nigeria ilivyokuwa, yeye anatia mbwembwe kwa misemo yake isiyoeleweka, sio watazamaji wote walioshuhudia mechi hiyo ni vyema akasimulia kwa lugha ya kawaida watu waelewe badala ya misemo isiyoeleweka
anaboa sana huyo ripota.
 
Kwa msikilizaji yeyote mwenye weledi na ufahamu mkubwa wa kujua mambo huyu jamaa ni kifaa! Lakini kwa bahati mbaya asilimia kubwa ya hadhira inayomsikiliza haiko level hiyo.Ndio maana watu wengi wakisikiliza taarifa yake wanaishia kuulizana: kasema nini...? amesemaje..? Kwa maana hiyo generally hawezi kuitwa mtangazaji mzuri kwani anashindwa kufikisha ujumbe kwa watu wengi!
 
Naomba niseme kitu kimoja,
Mimi binafsi nina asili ya mikoa iliyoanza kuzungumza Kiswahili miaka ya nyuma sana. Nakiri mtu hawez zungumza Kiswahili cha aina yoyote nisimuelewe.
Hemed Kivuyo anatumia tashbiha sana na methali nyingi katika utangazaji wake. Ni kitu kizuri na kinavutia ila watu wengi hasa walioanza kujifunza Kiswahili shuleni wanapata tabu kumuelewa. Ushahidi ninao huku kanda ya ziwa, maneno mengi ya Kiswahili hawayajui. Wengi walianza kuongea Kiswahili walipoanza shule.
Ishu sio kumponda Kivuyo ishu ni kwamba watu wajifunze Kiswahili waache kulalamikia vitu visivyo na msingi. Kumbukeni session inaitwa michezo na burudani. Yale maneno ya Kivuyo nayo burudani. Big up Kivuyo. Keep it up.

"Unamlilia nani maisha umeyakosea mwenyewe" Mbwiga wa Mbwiguke wa Clouds

Huyu naye wengi hawamwelewi.
 
Kwakweli hakuna mtoa taarifa za habari za michezo ninayemkubali kama Kivuyo.
Ukifika muda wa ripoti kutoka kwake naongeza sauti ya juu kabisa ili nipate burudani vizuri.
Popote ulipo Hemed Kivuyo pokea pongezi zangu, Mungu akupe umri mrefu uzidi kutupa burudani.

Nyie wa uswazi ndo mnakubali,sisi wazee wa hd hatuoni cha maana,
 
Nyie wengi hamjagundua Ni nn kimepelekea huyu jamaa kumponda Kivuyo.Kwa uhakika mleta mada Inaonyesha Ni gamba hivyo Kivuyo alipochomekea kwamba watu walinyosha vidole viwili kuashiria mabadiliko baada ya kupewa ofana Makamba hili jambo limemkera na Si Vinginevyo.Nazidi kukuhabarisha kwa sasa mnatakiwa kusoma alama za nyakati .Watz wanahitaji mabadiliko.
 
Asiyejua maana haambiwi maana, kama huijui fasihi ya Kiswahili ni kweli utatoka sufri bin sufri.
 
Kwa kweli Hemedi kivuyo hunikosha sana akitangaza mleta mada una lako jambo kwa vile mashabiki walikua wanawwka peoples ndo mana ume mumind .
 
Kwa msikilizaji yeyote mwenye weledi na ufahamu mkubwa wa kujua mambo huyu jamaa ni kifaa! Lakini kwa bahati mbaya asilimia kubwa ya hadhira inayomsikiliza haiko level hiyo.Ndio maana watu wengi wakisikiliza taarifa yake wanaishia kuulizana: kasema nini...? amesemaje..? Kwa maana hiyo generally hawezi kuitwa mtangazaji mzuri kwani anashindwa kufikisha ujumbe kwa watu wengi!

Gud explanation
 
Back
Top Bottom